CHADEMA kuishitaki serikali kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuishitaki serikali kwa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Dec 12, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  na Asha Bani  MKURUGENZI wa Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema serikali bado haijawashughulikia mafisadi na kwamba wanaendelea kuitafuna nchi na kuwaacha Watanzania wengi wakiendelea kutaabika.
  Mnyika alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara ya Operesheni Sangara inayoanza leo mkoani Tanga.
  Alisema Operesheni Sangara inafanyika kwa lengo la kuishitaki serikali kwa wananchi wa mkoa huo kutokana na kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi hao pamoja na kuwatumikia wananchi.
  Mnyika alisema mkoa huo ulikuwa maarufu kwa ukuaji wa viwanda, lakini sasa vimekufa kutokana na kuwa na usimamizi mbovu.
  “Ni lazima tuishitaki serikali kwa wananchi kwa kuwa umma ndio waamuzi na ndio ambao wanataabika kwa hali hii iliyopo sasa, ikiwa hata viwanda vyetu vinashindwa kusimamiwa na kufia mikononi mwa serikali inayoongozwa na CCM,” alisema Mnyika.
  Alisema Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi hivi karibuni ilitafakari hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba taifa linaendelea kufilisika kutokana na mafisadi kuendelea kutamba.
  Mnyika alisema operesheni hiyo itaambatana na kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kuichagua CHADEMA katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika hivi karibuni.
  Naye Mkurugenzi wa Oganaizeshi na Mafunzo Taifa wa chama hicho, Benson Kigaila alisema katika ziara hiyo kutakuwa na vikosi viwili katika kuwafikishia ujumbe wananchi. Alivitaja kuwa ni kikosi cha anga kitakachoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na kikosi cha ardhini kitakachoongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willbrod Slaa. Alisema kwa siku itafanyika jumla ya mikutano 34 ambapo kikosi cha anga kitafanya mikutano 18 na kikosi cha ardhi 16.
   
 2. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Safi sana Chadema kurejesha operesheni sangara. Muda wa malumbano umeisha na sasa mjizatiti kwenye kukijenga chama.
   
 3. i

  ishuguy Member

  #3
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Chadema ni chama pekee kinachaonesha kuwa na strategies nzuri.
  Sijawahi kusikia chama chochote cha upinzani kikifanya operesheni mara kwa mara na kuwaelimisha wananchi,CCM huwafikia wananchi wanapoona maji yamekuwa ya shingo.
  Hawa jamaa inaweza kuwachukua mda mrefu kuona reaction ya wananchi,lakini watafanikiwa.
  Endelezeni mapambano chadema, vita ya ufisadi huwa haishi huwa inapata break tu.
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Baada ya operation kama hizo wanafarakana maana per-diems, and other allowances zinawafikia wachache na viongozi wakuu (wenye chama) wanaweka bill kubwa za kuwa wamefund operation chama kina achwa na madeni makubwa sana!
  cost-benefit analysis ya chadema ni almost zero kwa shughuli kama hizi halafu hakuna ajenda nyingine zaidi ya ufisadi na JK..lol how about elimu, afya wanatafanyeje tofauti na ccm?
   
Loading...