Chadema: Kuendeleza ukoloni wa tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Kuendeleza ukoloni wa tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LUKAZA, Dec 1, 2010.

 1. LUKAZA

  LUKAZA Senior Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 136
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Assalaam Alaaykum,

  AMANI YA BWANA IWE NANYI

  YAA NIPO NA NTASEMA KWELI TU NAJUA NI MWIBA ILA NDO HALI POKEENI
  WANA JAAMII WALA MSIWE NA WAC WAC MALARIA ZANZIBAR IMEKWISHA
  Wazee Wetu, Ndugu Zetu,
  UMO JA, UHURU, UADILIFU
  Qauli ya Umoja wa Wazalendo

  Kukhusu Mbinu za CHADEMA Kupinga – Maamuzi ya Zanzibar Kwamba “Zanzibar ni Nchi”.

  Tanganyika Wanahakikisha Kuwa Zanzibar ni Koloni lao
  Yeyote atakaejaaliwa kuisoma kwa utulivu hii (hapo chini) maqala ya CHADEMA hatashindwa kugundua kwa uchungu na khasira kabisa jinsi Tanganyika wanavyoendelea kuamini na kuthibitisha nia yao kwamba Zanzibar lazima iendelee kuwa koloni lao kwa hali yoyote ile.
  Wazanzibari Wathibitisha Kuwa “Zanzibar ni Nchi”.
  Qauli ya Mhishimiwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, Bwana Pinda; kwamba “Zanzibar si Nchi”; ni pigo kubwa kwa Wazalendo wa Kizanzibari. Zaidi, qauli hii ilithibitisha kwamba Tanganyika juuyakuwa Zanzibar wamewapa imani yao, badala yake wao Tanganyika wamekhini amana hii na daima kupanga mbinu ovu, kufika kuifanya “Zanzibar si Nchi”. Wakati huohuo, qauli hii ya Mhishimiwa Waziri Mkuu, na khasa pale aliposisitiza kwa kusema “kwa mujibu wa katiba “Zanzibar si Nchi” Wazalendo wa Kizanzibari walitambuwa wajibu wao juu ya kushikamana kwa rahaka ili kuokowa nchi yao. Machungu haya yaliinua hisia za kizalendo na kujenga Umoja na Mshikamano madhubuti kabisa, khasa pale ulivyonadiwa na Mhishimiwa Rais Aman Abeid Aman, akiwa ni Rais wa Zanzibar wakati huo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe kila kheri.

  Awamu ya Rais Aman Imefufuwa Uzalendo wa Kizanzibari
  Katika miaka ya mwisho ya awamu ya Rais Aman, Alhamdulillah; Zanzibar ilishuhudia na kushirikiana katika harakati muhimu kabisa za Kizalendo. Miongoni mwa harakati hizo ni:
  Ø Wazalendo wa Kizanzibari walisherehekea Uhuru wa Zanzibar siku ile ya Disemba Kumi – 2008 na 2009.
  Ø Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) kwa sauti moja walipasisha kwamba mafuta, gesi na maliasili ya Zanzibar, ni milki khaasa ya Zanzibar.
  Ø Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) kwa qauli moja walipasisha kwamba “Zanzibar ni Nchi”, na kusainiwa na Rais wa Zanzibar, Mhishimiwa Aman Abeid Aman kuwa ni sharia ya Nchi.

  Tanganyika Wanashindwa Kuficha Ukoloni Wao
  Katika kipindi hiki na harakati hizi za Kizalendo, Tanganyika wameshindwa kuficha dhamiri yake ovu juu ya Zanzibar, dhimiri ya kuendeleza ukoloni wake kwa kutumia mbinu ya kikoloni, mbinu ya WAGAWE ILI UWATAWALE. Katika kutekeleza mbinu zake za kudumisha mfarakano kati ya Wazanzibari, Tanganyika walileta Zanzibar “Tume ya Mzee Mwinyi” kuja kuchunguwa kwanini Wazanzibari wanasimama begakwabega katika maslaha ya nchi yao. Tume hii haikufanikiwa, kwasababu Wazalendo wa Kizanzibari, yaani Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) walikataa kuhojiwa mmoja mmoja, qauli yao ilikuwa, ikiwa wao kuhojiwa, basi iwe kwa wote pamoja sio mmoja mmoja; hivyo tume hii ya Mzee Mwinyi ilirejea kwao mikono mitupu.

  Tanganyika Kudharau Maamuzi ya Zanzibar
  Tanganyika hawajazowea, bali khasa si maslaha yao kuona Wazanzibari wanasimama qauli moja kwa maslaha ya Nchi yao. Kutokana na uovu wao huo, kila uwamuzi wa Zanzibar, Tanganyika wanaona lazima wauzuie kwa hali yoyote ile usitekelezeke. Miongoni mwa hayo:
  Ø Walifikia muwafaka CCM na CUF kufanya sirikali ya pamoja, Dodoma / Butiama wakatoa amri kwamba lazima ifanywe kurayamaoni kuulizwa Wazanzibari “kama wanataka kusikilizana”.
  Ø Baraza la Wawakilishi, (Bunge la Zanzibar) limepasisha na kusainiwa na Rais wa Zanzibar kuwa “mafuta, gesi na maliasili ya Zanzibar ni mali khalisi ya Zanzibar”, Tanganyika wanakuja na sauti kwamba hivyo ni kinyume na katiba, (katiba ya Tanganyika); suala hili lazima lipasishwe na Bunge la Tanganyika.
  Ø Baraza la Wawakilishi, (Bunge la Zanzibar) limepasisha “Zanziba ni Nchi” na kusainiwa na Rais wa Zanzibar. Tanganyika leo hii – CHADEMA – wanazuka na kusema ni kinyume na katiba, (katiba ya Tanganyika) na kupanga kupeleka madai yao kwenye Bunge la Tanganyika kupinga maamuzi ya Zanzibar.
  Kutokana na yote haya, Bunge la Tanganyika linazidi kudhihiri kuwa ni chombo cha kuendeleza ukoloni wa Tanganyika juu ya Zanzibar. Wazanzibari kwa hali hii ndipo wanapojiuliza, “Ni kweli huu wenyekuitwa muungano” ni kwa maslaha ya Zanzibar?

  Vyama vya Siasa Visimame Qauli Moja
  Hizi mbinu za kikoloni za Bunge la Tanganyika, kufika hii leo kujitokeza CHADEMA kusimama mstari wa mbele, dhaahiri shaahiri; katika utekelezaji wa mbinu ovu hizi, ni lazima Wazalendo wa Kizanzibari kwa umoja wetu kusimama qauli moja na Baraza letu la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) na kupinga kwa sauti kuu kabisa hivi Bunge la Tanganyika kuwa daima ni pingamiza juu ya maamuzi ya Zanzibar. Vyama vya siasa, CCM, CUF, Jahazi Asilia, AFP, UPDP na vyenginevyo, watambue kuwa si uzalendo hata kidogo wao kunyamaza kimya na kuwacha uovu huu unatendeka. Mi muhimu na ni wajibu wao wadhihirishe uchukivu wao juu ya huu uovu wa Bunge la Tanganyika, na khasa hizi mbinu za CHADEMA, na kulitaka Bunge la Tanganyika liwache mtindo huu wa aibu, mtindo wa kudharau na kuwa ni pingamizi juu ya maamuzi ya Zanzibar. Mtindo huu hautilii nguvu, bali unazidisha kuvunja imani juu ya huu wenyekuitwa muungano.

  CHADEMA Wasitufanye Zanzibar “Mbuzi wa Muhanga”
  Iwapo CHADEMA wanayo madai yao, au hata kama wanazo tafauti zao, au hata kama wanayo mivutano yao na Bunge lao, au hata na Sirikali yao ya Tanganyika, tafadhalini wasitufanye Zanzibar kuwa ni “mbuzi wa muhanga”. Imani yetu ni kushirikiana katika ya maslaha yetu sote. Msingi wetu ni kutoridhia kwa hali yoyote ile kubomolewa maslaha yetu, ni wajibu wetu kulinda na kuhifadhi maslaha yetu kwa hali yoyote ile.

  Shukrani Zetu Kwa Rais Aman
  Kwa munasaba huu, Umoja wa Wazalendo unachukuwa fursa hii kueleza tena, shukrani zake za dhati kwa Rais Aman kwa juhudi zake za kujenga umoja na mshikamano. Vilevile shukrani zetu za dhati kwake yeye khaasa na kwa Wawakilishi wetu kwa khatuwa hii kubwa na ya kihistoria kupitisha sharia kuirejeshea Zanzibar hadhi yake kuwa ni Dola Kaamili kama vile ilivyokuwa pale ilipopata uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba 1963, na kuwa “Zanzibar ni Nchi”. Ni juu yetu kushikamana na kuhakikisha inaendelea kuwa “Zanzibar ni Nchi, kwa hali yoyote ile haitarajea tena vile kuwa “Zanzibar si Nchi”.
  Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Ta’aala atujaalie kila kheri na baraka na awajaalie viongozi wetu uwongozi wa kheri, uadilifu na baraka na siha na tawfiiq katika kila khatuwa za matengenezo ya nchi yetu, Aamyn.
  Wa Billahi Tawfiiq
  Umoja wa Wazalendo,

  Zanzibar
   
 2. s

  sharky New Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  What garbage! You should be in a slave sanatorium! Juzi tu mlikuwa watwana wa mwarabu leo mwataka kujifanya mabwana!
   
 3. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma lakini sijaelewa ulichoandika
   
 4. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Lawama nyingi dhidi ya CHADEMA, lakini nimesoma hadi mwisho hakuna sehemu yoyote ambayo umeonyesha chadema WALICHOSEMA AU KUFANYA hadi ufikie hatua ya kuwalalamikia.
  Hivi mtawala wa nchi hii ni nani? hujui kuwa ni ccm? na ndio inayotawala nahuko visiwani. Sasa cHADEMA wanaingiaje kuwafanyeni nyie koloni?
  Au kwa kuwa mmeungana na ccm na kwa vile mmezoweya kulalama kila kukicha, sasa mnatafuta wa kumltupia lawama.
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Asalaam aleykhum ustaadhi. Naomba nijuze ni nini kimekusukuma kuandika hivi, ndo huu umoja wa Wa...... Haya bwana, kuna magonjwa mengine tunapata shida kuyapatia jina. Anyway nadhani huu unaweza ukaawa ugonjwa wako mwenyewe na sio wa hao wana Umoja Wa.... wenzako. Nenda hospital halafu rudi tena u-dit kazi yako otherwize itanichukua muda kuelewa ugonjwa ulioandika
   
 6. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Imebidi nisome mara mbili mbili lkn sijaelewa unamaanisha nini??

  Haya malalamiko mbona hayana mifano na walichofanya CHADEMA, mpaka kuwahukumu hivyo.

  Ahaah.. Ustaadh wafanya fitina sasa hapa. hii ni toafauti na maagizo ya Allah. waswali kweli weye??

  Labda tuoseme CHADEMA kosa lao ni kuleta upinzani wa kweli kaw CCM, amcho nyie wana CUF hampendi ndugu yenu akosolewe.

  Au ndio kiapo chenu cha muafaka kwamba.. "ntaitetea, kulinda na kuitukuza CCM popote hata ikighalimu kuhalimu maisha ya wanznibar na masilahi ya Taifa, na kila takaipinga CCM ni najisi kwangu"

  okey okey kiapo kizuri sana hicho. lkn jueni waTZ siku hiz HAWADANGANYI
   
 7. n

  ngoko JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zenji ina haki ya kudai nchi yao , hata Rev. Mtikila kwenye kanda ya saa ya ukombozi analiunga mkono hilo 100%.
   
 8. n

  ngoko JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zenji ina haki ya kudai nchi yao , hata Rev. Mtikila kwenye kanda ya saa ya ukombozi analiunga mkono hilo 100%.
   
 9. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Qauli nyingine bana...

  Mzee Mwinyi anayelaumiwa kuchunguza kwanini wazenji wanakuwa bega kwa bega ni wa CCM,
  Pinda naye aliyenukuu Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa 'Zanzibar si nchi' ni wa CCM,

  Maamuzi unayolaumu (vikao vya Butiama na Dodoma) ni ya viongozi wa CCM chini ya Kikwete,
  Waliofuta siku ya 'uhuru' wa Zbar wa 1963 (10 December) ni vyama wazazi wa CCM.

  Vp waweweseka kwa kauli moja tu ya Chadema?

  Wabillah tawfiiq...
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Katika Kiswahili Fasaha tuna neno Maqala hizi Q zinatoka wapi??

  Ili Kujitegemea siyo lazima ujitenge kuwa na umoja si lazima uwe na muungano.

  Makala haieleweki.
  Nionavyo mimi kuna Hoja kubwa waiongeyayo huko mafichoni sasa wakija hapa Nuruni wanamung'unya kwa sababu wakisema wazi nia na madhumuni yao patakuwa hapakaliki.

  Kuna hoja ndani ya hoja zinazoashiria kwamba Sultan aliyepinduliwa na John Okello miaka 46 iliyopita Binamu wajomba shangazi na mashoga zake kule Zanzibar wamedhamiria ardishwe kwa gharama yeyote. Si unajua tena kule Oman aliondoka rasmi kwa kudhani Zanzibar ndo nchi yake ya Ahadi???
   
Loading...