CHADEMA kubadili gia angani kuhusu Sera ya maendeleo ya watu?

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,389
9,664
Kutokana na mwenendo wa kampeni ulivyo sasa. Ni dhahili kwamba watu bado wanahitaji maendeleo ya vitu kwa sana. Watu wanahitaji Maji, Umeme, Barabara, Reli, Ndege n.k na sio maneno maneno.

Na kutokana na kampeni zinavyoenda CDM imewakuwa ikiacha wapenzi wake njia panda bila kuonyesha hasa nini itawafanyia toafuti na kuponda tu aliyoya yafanya Rais Magufuli. Mpenzi wa kawaida ya CHADEMA amesikika akisema kwamba wapenzi wa CHADEMA wana Kiu sana ya Maendeleo lakini kwa hakika Magufuli ndie mwenye kuleta maendeleo hayo na sio Maneno tu ya Lissu.

Na kutokana na vyanzo mbalimbali hadi sasa Lissu imebidi nae abadili kampeni zake na kuendelea kuahidi kujenga Reli(Rukwa), Kujenga Barabara lakini bado hajasema sawasawa.

Ikumbukwe kwamba watu wengi hasa wa kijijini wanataka maendelo ya vitu ikiwemo, shule za karibu, Maji, barabara. n.k.

Je, CHADEMA kinabadili gia angani?.

Ushauri.. CHADEMA futeni sera ya madini inasumbua huku mtaani.
 
Na hasa ile sera ya kijambazi ya kuweka dhamana mali za nchi zisihamishika kweli chadema majanga. Leo hii Kenya wanastruggle kujiepusha na janga la bandari yao kwa mchina, Zambia anateseka kurudisha Airport aliyoweka dhamana.Lakini waafuasi wa Lissu hawaelewi kitu ni poyoyo kwa kutupwa.Chadema ni hatari kwa mstakabari wa nchi.Hata mchumi mbobezi Zitto kabwe huenda yuko mbali na huu upupu wa chadema
 
..unatakiwa u-balance.

..maendeleo ya watu vs maendeleo ya vitu.

..ukizidisha upande mmoja, na kupunja upande wa pili, utaingia kwenye matatizo.
 
Ni ujinga kuponda Sera ya vitu,kwani bila jembe huwezi kwenda kulima, na uspolima hupati mazao na usipopata mazao huli

Hapo chanzo nini, (Vitu) ambacho ndio nyenzo ya kukufanya upate maendeleo, ambalo ndilo, Jembe, inamana hawataki tuwe na jembe, Tutalimalimaje sasa? Wanataka kutupa pesa au siyo?

Huwezi kufika Mwanza Kwa haraka bila kutumia usafiri wa, Gar, Treni n.k

Na Gari haiwezi kwenda huko bila, barabara na njia ya Treni, na hivyo Vyote ni, Vitu!!!

Sasa unapokataa vitu, unakataa maendeleo,

Taifa hili linawatu wa ajabu mpaka inaboa
 
Mungu aliumba vitu kwanza ndio akamalizia kumuumba mtu ….. (hii ni sala ya mtumishi leo Kigoma akifungua mkutano wa kampeni)

Mungu aliumba (si kutengenza) na wala hakutumia kodi za malaika
Kama ni kutumia hoja ya mungu na nyie tumieni hela zenu kwanza
Usufananishe mipango ya mungu na binaadam
 
Ni mfano tu askofu katumia.

Daah,mkuu! Unapinga nini na unashauri nini Yani?
 
Na Gari haiwezi kwenda huko bila, barabara na njia ya Treni, na hivyo Vyote ni, Vitu!!!

Sasa unapokataa vitu, unakataa maendeleo,

Taifa hili linawatu wa ajabu mpaka inaboa

..Na hayo magari yanabuniwa na kuundwa na nani kama siyo watu, tena watu walioendelea?
 
Sio kwamba CDM hawatajenga reli, viwanja vya ndege na madaraja, watajenda sana ila vitakuwa bila upendeleo kikanda na bila ufisadi katika mikataba kama ilivyo sasa.
 
Hivyo vitu vyenyewe vimefuata utaratibu wa manunuzi ya umma? Mnatetea kwa sababu nyie mmo kwenye mfumo mnakula raha na familia zenu, mnaona wananchi wa kawaida hata wakiwa na maisha magum haiwahusu, siku wakichoka tutapoteza wote.
 
Sio kwamba CDM hawatajenga reli, viwanja vya ndege na madaraja, watajenda sana ila vitakuwa bila upendeleo kikanda na bila ufisadi katika mikataba kama ilivyo sasa.
Wasaidie waeleze hayo. La sivyo inakula kwao mapema sana.
 
Wasaidie waeleze hayo. La sivyo inakula kwao mapema sana.

..maendeleo ya vitu ni kama kujenga international airport ktk eneo ambalo wananchi hawana hata maji safi, kilimo chao ni cha kubahatisha.

..tukubaliane kwamba kuna a dis-connect kati ya maendeleo anayoyafanya Jpm, na hali ya uchumi na kipato ya waTz waliowengi.

..Jpm yuko too obsessed na mavitu makubwa-makubwa na amewasahau kabisa wananchi, na wakati mwingine anawatukana kwamba ni wavivu.
 
..unatakiwa u-balance.

..maendeleo ya watu vs maendeleo ya vitu.

..ukizidisha upande mmoja, na kupunja upande wa pili, utaingia kwenye matatizo.

Unasahau kuwa, viongozi makini ni viongozi wanajenga kwaajili ya kizazi kijacho. Uking'ang'ania kuendeleza kizazi cha leo, kizazi kijacho watakuta nchi iliyo tupu na haina maana yoyote. Huwezi kujitoa muhanga kujenga ili Tanzania ya kesho iwe na neema kuliko ya leo, na huku unajaribu balance vitu, "Mtaka yote hukosa yote".
 
Back
Top Bottom