Unaweka facts ikiwa kama unazungumzia Chama chenye kuonyesha uzalendo ,lakini hawa jamaa ni wajuaji kuliko unavyowafahamu ,na hizo facts za kuziangalia zipo tele ,kwa uchache angalia madai yao pale bungeni na yale majina yao waliyoyataja ya mafisadi kwenye majukwaa ya mikutano ni kupoteza wakati wa wananchi, jiulize madai yao yamefikia wapi ? Hawa huwaamsha wezi tu hio ndio kazi yao ,yaani wao ni kama indicators ,wabunifu wao CCM(CDM ni mtoto wa CCM) ,CCM waliiunda CDM kuwa chama mbadala au chama cha kuusambaratisha umma wa Taifa hili kama tuonavyo ,wezi wanapeta ,mafisadi wanatetewa na haohao Chadema ,si unamuona yule wanaemuta Zitto msaliti.Mkuu with respect huwezi kusema maneno yako bila kuleta facts, ni vizuri ungeweka grounds ambazo zingetusaidia kuweza kuijadili mada kwa marefu na mapana.
Du Mwiba yote uliyonena sawa kabisa lakini kutuwekea Salim Ahmed Salim halafu ukamkana kuwa sio mzanzibar na Mwinyi aliyetawala wawamu ya 2? Da bado kabisa ukampambanisha na Safari nimepata kizungu:roll:zungu
kumbe habari imetoka kwa mwana CCM ....basi habari hii ni propaganda
Yakhee ,Salim si mzanzibari aliwahi kusema yeye ni mnyasa pili hali kadhalika Mwinyi nae ndio kabsaa ni mzaramo wa hapo Kisarawe
Huyo Safari ndie mgombea kwa tiketi ya Chadema 2015 ,semeni kama hamjasikia maana wenyewe eti wanaifanya kuwa ni siri kubwa.
Dalili za mvua inasemwa ni mawingu japo wengine tunasema ni upepo ! Kigogo nilimhoji ni vipi Chadema itakufa wakati jamii kubwa ya WaTz wameidondokea ? Alinishangaza na kusema kwani huikumbuki CUF ambayo ni chama kilichokalia kivita kuliko vyama vingine vyote hapa Tanzania ? Nikajibu ni kweli CUF ni chama kisichokuwa na lelemama kimefanya kweli na kimeingia Ikulu lakini ndio kimeshuka chati ,hapo kigogo ndipo akaja juu na kusema na Chadema nayo itashuka ,baya zaidi kwa Chadema hata ikulu haitokanyaga.
Nani aliwaambia kama Salimu Ahamed ni Mzanzibari ? Wacheni uvivu tafuteni ,kuhusu kuanguka kwa Chadema hilo wandugu halina ubishi .CDM 2015 inakwenda na maji ,sawaswaa !
Jingine hivi niwaulize nyinyi na tarehe zenu ni lini Mzanzibari aliwahi kushika nafasi ya Uraisi wa JMT ??? Sasa niwasikiapo wengine wanaosema Wazanzibari tusahau kuupata uongozi wa juu wa SMT naona mtakuwa mna viherehere hamjui mnenalo!
inaongelewa hoja ingine unaleta utumbo, mseto wa cuf na ccm unahusika nanini hapa ktk mada hii?roho zitawauma sana mwaka huu,wazenj wanaenda mbele nyie kazi malumbano tu.Ubabe upi?
Wa Richmond, Dowans, Kagoda, IPTL, RADA, Muafaka wa vyama viwili kati ya vingi, hebu tueleze. CUF ni upinzani au chama Twawala.
CCM ambao hadi hapa tulipo wameshaanza kujenga mazingira ya ushindi na kujinyakulia ushindi mnono wa uchaguzi wa 2015 ,mgombea wa Chadema Safari ambae hakubaliki na jamii huenda akapambana na Salim Ahmed wa C
Naungana na wewe kumbe DOWANS na migomo ya kila siku ndo mazingira mazuri ambayo CCM inajijengea kuchukua ushindi wa Kishindo wa kuanguka 2015? safi sana pia ukumbuke kwa sasa hakuna Mzanzibar hata mmoja anayeweza kusimama kugombea nafasi ya Urais akashinda hasa kwa huku Tanganyika hilo msahau kabisa