CHADEMA kimesema kitampatia Mbowe wanasheria wa chama katika kesi ya kikatiba na madai dhidi RC

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitampatia Freeman Mbowe wanasheria wa chama katika kesi ya kikatiba na madai dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, RC Paul Makonda.
Februari 8 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitaja majina 65 kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya akiwamo Mbowe na kuwataka kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa.

Lakini siku moja baadaye Mbowe aliitisha mkutano na waandishi wa habari akiwa mjini Dodoma ambapo alieleza kutofika polisi kwa wito wa Makonda akisema hana mamlaka hiyo isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni aliweka bayana nia yake ya kumfungulia mashtaka ya madai Makonda kwa kumkashifu na kumchafulia jina.

Akitoa maazimio ya kikao cha kamati ndogo ya Kamati Kuu ya Chadema jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdalah Safari alisema kamati hiyo inaunga mkono hatua ya Mbowe kumfungulia kesi ya kikatiba Makonda.

“Katika hili tumejipanga kweli kweli…tutaungana na Mbowe katika kesi hii na tutampatia mawakili wa chama akiwamo mimi na tuko wengi,”alisema.

Profesa Safari aliwataka wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa kujihusisha na biashara au utumiaji wa dawa za kulevya wafungue mashauri mahakamani.

“Tunatoa wito kwa wale wengine wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa, kuchafuliwa majina na au kudhalilishwa wafungue mashauri mahakamani, kwani hii ndio njia pekee ya kuzuia wengine wasifanyiwe uonevu kama huu siku zijazo,”alisema Profesa Safari.

Pamoja na mambo mengine, Profesa Safari alisema tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu 2015 viongozi na wanachama wa Chadema wamekuwa wakikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kubambikiziwa kwa kisingizio cha uchochezi.

Alisema mpaka sasa jumla ya wanachama na viongozi 215 wamefunguliwa kesi zaidi ya 78 nchi nzima.

“Kati ya hao wengi wao wamenyimwa dhamana bila sababu za msingi huku wale ambao walipatikana na hatia walipewa adhabu za vifungo bila kupewa fursa ya faini.

“Kutokana na hilo, hivi sasa tunaandaa orodha kamili itakayoainisha kesi zote za jinai ambazo ziko mahakamani na kuonyesha aina ya mashtaka na vifungo vilivyotolewa ambayo itawekwa wazi kwa vyombo vya habari na taasisi za ndani na nje ya nchi kuthibitisha kuwa kuna mpango wa kuwafunga viongozi wa upinzani kwa kusudi ili kuwadhoofisha,”alisema Profesa Safari.

Katika hatua nyingine Profesa Safari aliwaomba marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu na majaji wastaafu kuzungumza na Rais John Magufuli kutokana na yanayoendelea na kwamba wasiogope kwani wao hawatatumbuliwa.

“Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wanaogopa nini? Kwanini wasimwambie Rais Magufuli kuwa na wao waliapa kuilinda Katiba ya nchi hivyo na yeye afanye hivyo.

“Mawaziri wakuu wako wapi? Cleopa Msuya, Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim huyu amekuwa kimya kabisa na alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Majaji wastaafu nao wako kimya. Tunaomba waache uoga wajitokeze wao hawatatumbuliwa,”alisema Profesa Safari.
 
Nguvu zote za nini?si aende akatowe ushirikiano tu mbona anakuwa na wasiwasi kama yuko clean shida iko Wapi?
 
Kwani aliitwa akatowe ushirikiano au aliitwa kwasababu na yéyé anatuhumiwa kwakuuza? Acha aende mahakamani maana huko ndiko kunahaki
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitampatia Freeman Mbowe wanasheria wa chama katika kesi ya kikatiba na madai dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, RC Paul Makonda.

ULAJI WA ruzuku kijanja na ulaghai kwa wana CHADEMA.Hakuna separation ya CHama na Mbowe binafsi. .CHAMA ndio Mbowe na mbowe ndio chama/Mbowe ana kesi binafsi ya madawa ya kulevya.Badala ya kushtaki kibinafsi atumie pesa zake binafsi kwa mambo binafsi ya kesi kaamua kuifanya kesi ni ya kichama ili atumie pesa za chama kulinda tatizo lake binafsi.

CHADEMA mnajitia mnapenda sana kuzingatia sheria kwa nini hakuna msitari unaogawa kati ya mambo binafsi na ya chama? Tukiwaambia CHADEMA ni chama cha Binafsi cha mbowe na familia yake mnakataa.Hiki mnachofanya ni ushahidi kuwa hicho chama ni mali binafsi ya mbowe
 
kwa hiyo na yeye atachangia gharama au ni hizihizi ruzuku(kodi zetu wananchi) za kuendeshea chama. Msifanye hilo kosa wakati kuna kijana juzi Lizabon alimuweka huku anataka kuuza kiwanja chake geita ili ajitibu kwa matatizo aliyoyapata kutokana na ujenzi wa chama chenu
 
Mmh mwenye nyumba kamwe hawezi kupanga ndani ya nyumba yake,just ni kuchagua tu chumba akipendacho ndani ya nyumba yake.
 
ULAJI WA ruzuku kijanja na ulaghai kwa wana CHADEMA.Hakuna separation ya CHama na Mbowe binafsi. .CHAMA ndio Mbowe na mbowe ndio chama/Mbowe ana kesi binafsi ya madawa ya kulevya.Badala ya kushtaki kibinafsi atumie pesa zake binafsi kwa mambo binafsi ya kesi kaamua kuifanya kesi ni ya kichama ili atumie pesa za chama kulinda tatizo lake binafsi.

CHADEMA mnajitia mnapenda sana kuzingatia sheria kwa nini hakuna msitari unaogawa kati ya mambo binafsi na ya chama? Tukiwaambia CHADEMA ni chama cha Binafsi cha mbowe na familia yake mnakataa.Hiki mnachofanya ni ushahidi kuwa hicho chama ni mali binafsi ya mbowe

Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wanaogopa nini? Kwanini wasimwambie Rais Magufuli kuwa na wao waliapa kuilinda Katiba ya nchi hivyo na yeye afanye hivyo.
 
kwa hiyo na yeye atachangia gharama au ni hizihizi ruzuku(kodi zetu wananchi) za kuendeshea chama. Msifanye hilo kosa wakati kuna kijana juzi Lizabon alimuweka huku anataka kuuza kiwanja chake geita ili ajitibu kwa matatizo aliyoyapata kutokana na ujenzi wa chama chenu
Katika hili tumejipanga kweli kweli…tutaungana na Mbowe katika kesi hii na tutampatia mawakili wa chama akiwamo mimi na tuko wengi,”alisema.

Profesa Safari

Kwani aliitwa akatowe ushirikiano au aliitwa kwasababu na yéyé anatuhumiwa kwakuuza? Acha aende mahakamani maana huko ndiko kunahaki
 
Nguvu zote za nini?si aende akatowe ushirikiano tu mbona anakuwa na wasiwasi kama yuko clean shida iko Wapi?
Tunatoa wito kwa wale wengine wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa, kuchafuliwa majina na au kudhalilishwa wafungue mashauri mahakamani, kwani hii ndio njia pekee ya kuzuia wengine wasifanyiwe uonevu kama huu siku zijazo,”alisema Profesa Safari.
 
Kutokana na hilo, hivi sasa tunaandaa orodha kamili itakayoainisha kesi zote za jinai ambazo ziko mahakamani na kuonyesha aina ya mashtaka na vifungo vilivyotolewa ambayo itawekwa wazi kwa vyombo vya habari na taasisi za ndani na nje ya nchi kuthibitisha kuwa kuna mpango wa kuwafunga viongozi wa upinzani kwa kusudi ili kuwadhoofisha,”alisema Profesa Safari.
 
Hao 78 hajawatoa ndani halafu anashauri wengine wakafungue kesi! Na wao watalipiwa mawakili? Za kuambiwa changanya na za kwako.

Kwani akipimwa kwa mkemia akakutwa hana si ndio tutajua amesingiziwa kuliko kuwa kichwa ngumu, tutaamini anayatumia.
 
Chadema lini walikaa wakakubaliana hayo? Hv chadema lini watafuata katiba kwa kuruhusu organ za chama zifanye maamuzi badala ya mtu mmoja kujidai ndo chama kwa style ya top down approach
 
Mwambie Mtakatifu wenu tutapambana naye kila mahali tutamshinda.
Alisema mpaka sasa jumla ya wanachama na viongozi 215 wamefunguliwa kesi zaidi ya 78 nchi nzima.

“Kati ya hao wengi wao wamenyimwa dhamana bila sababu za msingi huku wale ambao walipatikana na hatia walipewa adhabu za vifungo bila kupewa fursa ya faini.
Hao 78 hajawatoa ndani halafu anashauri wengine wakafungue kesi! Na wao watalipiwa mawakili? Za kuambiwa changanya na za kwako.

Kwani akipimwa kwa mkemia akakutwa hana si ndio tutajua amesingiziwa kuliko kuwa kichwa ngumu, tutaamini anayatumia.
 
Uwe unasoma kwanza kabla ya kukurupuka kuandika.
Akitoa maazimio ya kikao cha kamati ndogo ya Kamati Kuu ya Chadema jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdalah Safari alisema kamati hiyo inaunga mkono hatua ya Mbowe kumfungulia kesi ya kikatiba Makonda.
Chadema lini walikaa wakakubaliana hayo? Hv chadema lini watafuata katiba kwa kuruhusu organ za chama zifanye maamuzi badala ya mtu mmoja kujidai ndo chama kwa style ya top down approach
 
Nguvu zote za nini?si aende akatowe ushirikiano tu mbona anakuwa na wasiwasi kama yuko clean shida iko Wapi?
Wanataka ktk matumiz ya chama waandike hela ya mawakili million 10 ili wazifukie tumbon zote,,,wanapenda kesi ili wapige hela za chama au hujui
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Kamati ndogo ndo ipi na iliundwa lini na nani, na je ipo kwenye katiba ya chadema?
 
Mawakili washajigundulia deal chadema wanawapiga kwelikweli. Mbowe alifanya kitu cha hatari sana kukaa na Hawa watu, maana deal Zao ni kesi tu. Ndio maana mnataka kuichukua na TLS kabisa
 
Nilikua na kesi mshenzi ka ardhi nikamtafuta wakili mchovu kitaa kukata rufaa tu nilitoa m3, kuendesha kesi milion 5. Sasa najiuliza haya makesi ya CDM sijui yana cost kiasi gani. Wakati mwenyekiti wa BAVICHA Geita anauza kiwanja milion 3.5 kugharamia matibabu yake.
 
Back
Top Bottom