CHADEMA Kimandolu, Arusha mnatia aibu!

CHADEMA Kimandolu, Arusha mnatia aibu!

calculator

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
279
Reaction score
137
Salaam Wanajamvi,

Nijikite moja kwa moja kwenye hoja yangu. Mwenyekiti wa CDM kata yetu hii anautumia vzr wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu. Jana Ijumaa alinunuliwa pikipiki namba MC 249 AGN aina ya boxer na mtia nia Josephat Shio. Kama vile haitoshi ndugu Shio alimlipia mwenyekiti huyo bwana Renatus Kimario deni la LIFAN SACCOS alilokuwa anadaiwa jumla ya Tsh. 2,100,000/ (milion mbili na laki moja). Taarifa hizi zimetufedhehesha sana sisi wanachama na wapenzi wa Chadema kimandolu.

Aidha mtia nia huyo ndg. Shio amejinasibu kuwa ameiweka mfukoni kamati tendaji ya kata ambayo kikatiba ndio yenye jukumu la kumteua mgombea. Kwa mujibu wa mtoa taarifa aliyekuwepo na ndg. Shio kwenye bar ya Arena jana Ijumaa ametanabaisha kuwa wajumbe 10 wa kamati hiyo walipewa jumla ya shilingi milioni tatu na aliyekabidhiwa fedha hizo ni Mosses Msuya ambae ni mwenyekiti wa mtaa wa Tindigani kwa maelekezo kuwa awapatie Tsh. laki 3 kila mmoja.

Hizi ni taarifa mbaya hususan kipindi hiki kuelekea uchaguzi mwezi oktoba. Nawasilisha
 
Kwa kweli chadema kama haya n ya kweli basi mnatutia aibu sisi wadau wenu tutafanya nn?
 
Tuliza kalio wewe sindano isivunjikie.. kaa mitaani upate data
umeaibika kwa umbea wako. rushwa iko kwenye ilani ya ccm kwa hiyo uache umbea maana mwisho wa siku utaolewa bure bila hata senti 1
 
Nilitegemea ungemwelewesha zaidi na kuonyesha ugenuine wako, kwani katika kipindi hiki ni wazi kwamba propaganda za aina hii zio ili kuwapaka matope viongozi walio thabiti.

Kwa comment yako hii, unatufanya wengine tukubaliane na huyo aliyesema, kwamba Lumumba wapo kazini i.e. ni propaganda tu na hakuna ukweli kwa lolote ulilosema hapo juu

jebibay..
Hii ndio habari. Leo mwenyekiti huyo ndg. Renatus Kimario ameondoka kwenda Tanga na basi la RATCO akiwa na mjumbe ya serikali ya mtaa wa kijenge kusini aitwaye Jesca Pascal Mudogo..
 
Last edited by a moderator:
chaikavu..jifunze kuskiliza au kusoma hata vile usivyovipenda. Hii ndio taarifa. Hutaki unaacha..
 
Last edited by a moderator:
Mosea Msuya hii ni kweli? Lazima uko humu Jf na ujibu
 
calculator

Duh hizi siasa za bongo noma ndio maana mm nimeamua sitakuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa kamwe
Kwani siasa ni mchezo mchafu
 
Last edited by a moderator:
Kumbuka kuna post yako ilikuwa inamtuhum Diwani anakopa sana na anadaiwa sana Leo umekuja na Mwenyekiti wa CDM.Inaonekana wewe ni CCM na hicho unachofanya ni kujishushia kuaminika .
 
Kumbuka kuna post yako ilikuwa inamtuhum Diwani anakopa sana na anadaiwa sana Leo umekuja na Mwenyekiti wa CDM.Inaonekana wewe ni CCM na hicho unachofanya ni kujishushia kuaminika .

Mimi kuwa CCM/ACT n.k haibadilishi ukweli wa nilichoandika hapa.
 
Kama ni kweli badilikeni sio kupinga tu, nyie mkiambiwa ukweli hamkubali
 
Calculator ya Ngoswe mwachie Ngoswe na si vizuri kuwachafua watu kwa chuki ubinafsi au kwa maslahi ya kisiasa.
 
Dah.. wajasiriamali wa siasa wanafanya yao. Jamaa kalipiwa deni???? Hataree sana
 
Back
Top Bottom