CHADEMA Kila kona: Salum Mwalim yuko Moshi, Dr Slaa yuko Mbeya

CHADEMA Kila kona: Salum Mwalim yuko Moshi, Dr Slaa yuko Mbeya

MsakaGamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
392
Reaction score
141
Tafadhari Mods msiunganishe thread hii...itakuwa na updates

Wanabodi.

kama kawaida ya CHADEMA leo kinaendelea mikutano yake ya hadhara kwenye maeneo muhimu mawili. Naibu katibu mkuu Zanzibar kamanda Salum Mwalim yuko kanda ya Kaskazini Moshi mjini mkoani kilimanjaro ambapo atakuwa mgeni rasmi wa mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama, mashabiki na wapenzi wa CHADEMA wanao soma kwenye vyuo vikuu 5 mkoani humo.

Vyuo hivyo ni Mwenge university, Chuo cha ushirika na biashara (Muccobs), chuo kikuu cha kumbukumbu ya Stephano, chuo kikuu cha hifadhi na wanyamapori, na chuo kikuu cha uuguzi na tiba (KCMC). Mara baada ya mahafali hayo Salum Mwalim atafanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini hapo utakao endana na ripoti ya mafanikio ya utendaji wa halmashauri ya mji wa Moshi ambayo iko chini ya uongozi wa CHADEMA kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza kwa kuwa manispaa safi Afrika Mashariki.

Wakati huohuo katibu mkuu wa chama na nguli wa siasa za Tanzania kiboko cha mafisadi leo yuko Kanda ya nyanda za juu kusini, mkoa wa Mbeya ambapo amefanya ukaguzi wa vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR kijiji cha Ishiwinga na kijiji cha Hatelele wilaya ya Mbozi na jioni atafanya mkutano mkubwa wa hadhara Mbozi mjini.

Dr Slaa amelakiwa kwa shangwe kubwa alipoingia kitongoji cha Mlowo kwa kupokelwa na msusuru wa magari na pikipiki huku kina mama wengi na vijana wakimshangilia kwa nyimbo na vigelele "Raisi, raisi, raisi..."

Amewataka wananchi wa maeneo hayo kujitokeza na kujiandikisha ili waweze kuchagua serikali ya UKAWA itayo rejesha matumaini mapya na kuwaondoa kwenye lindi la dhiki na ufisadi wa chama tawala.

Naomba kuwasilisha.
 
Hakuna kulala , mpaka kieleweke ndio maana yake hiyo

Leo mafisadi wakiwa busy kumsubiria fisadi wanaye muogopa, Dr Slaa atakuwa anawapiga za uso huku akikumbushia orodha ya list of shame ambayo ilimgusa na fisadi wa richmond ambaye alijiuzulu kwa sakata la richmond. Tuna wakaba kotekote wao na vibaraka wao
 
Ukawa na chadema juuuuuuuu! Watatukoma mwezi wa kumi lazima wangoke tuu wametunyonya vyakutosha mpaka wamepoteza network. Mmemwona sits Leo bungeni alivyo zodelewa na h.mdee pale alipotia document ambayo indalili za ufisadi na ilisainiwa na naibu wake halafu yeye sitta Hana na akawa anbisha? Ni aibu waziri haelewi kinachoendelea kwenye wizara anayoingoza!no uzembe was hari yajuu huuu!:sad::confu
 
Kila la kheri Dr Slaa,Rais ajaye wa Tanzania anaetarajia kuapishwa mwezi October.
 
Back
Top Bottom