CHADEMA Kigoma wampania Zitto

CHADEMA Kigoma wampania Zitto

Status
Not open for further replies.

Makete Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2012
Posts
531
Reaction score
166
Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Mkoa wa Kigoma, limesema litamshughulikia Zitto Kabwe iwapo ataamua kugombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini badala ya Kigoma Kaskazini.

Akihutubia wakazi wa Kata ya Gungu mjini hapa juzi, mwenyekiti wa baraza hilo, Omary Gindi alisema wamejiandaa kushinda ubunge na kutetea nafasi ya kuongoza Halmashauri ya Kigoma Ujiji kama walivyofanya mwaka 2010.

Gindi alisema watambana baada ya Zitto kudai hatagombea kwenye jimbo alilokuwa anaongoza kupitia Chadema na badala yake amejipanga kugombea katika Jimbo la Kigoma Mjini kubadilisha na Peter Serukamba (CCM).

"Zitto aje tu hapa Kigoma Mjini. Tutamuuliza aliwafanyia nini watu wa jimbo lake kiasi kwamba amemaliza kero zao na kuamua kuhama, vinginevyo tutawaeleza wananchi kwamba hafai na amekimbia kwao kwa sababu wananchi wamemwambia hawatamchagua tena kutokana na kushindwa kushirikiana na wapiga kura wake," alisema Gindi.

Alisema watu wa Kigoma wanaipenda na kuiunga mkono Chadema kwa vile baadhi yao walifungwa jela, kupoteza mali, kujeruhiwa na kupata ulemavu na wengine kukosana na wake au waume zao, jambo lililowafanya kujiona ni sehemu ya chama hicho.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Shaaban Madede aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

"Lazima mhakikishe CCM inang'oka madarakani ili Chadema iweze kuongoza dola na kupigania masilahi ya watu, kwa vile sehemu nyingi kuna kero ya huduma mbovu za elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara vijijini, suluhisho pekee ni kuiondoa CCM madarakani," alisema Madede.

Source: Mwananchi
 
Acha kupoteza muda,Kigoma hakuna tena chama kinachoitwa chadema.

Kwa sasa Kigoma ukiskia mtu yupo chadema basi anataka fedha za mbowe kama ilivyo kwa wapambe wa Lowassa ambao wanampiga pesa tu halafu kimoyomoyo wana mdis
 
Ivi nini kimemkimbiza zitto kigoma kaskazini na kwenda kigoma Mjini?

Zitto sio mwanasiasa Jamii ya Mama ana Abdallah amvae ana miaka 45 bungeni.

Zitto aliahidi kuitumikia Kigoma Ks kwa 10 yrs.

Zitto ndio mwanasiasa ambae anaweza kwenda jimbo lilote Tanzania na kushinda uchaguzi.
 
Chadema kigoma haipo, Huko hakuna misukule kama yapale Ufipa
 
Mnafiki na mpenda sifa utamjua tu, kwao hajamalizana nao anavamia kwingine, kifuatacho ni kunyima kura akaangukie pua.
 
Makete Kwetu

Hivi Mbowe alishamaliza kero zote za wana hai? Slaa alimalizj za karatu? Mjika za ubungo kamaliza? Lema naye za arusha mjini kamaliza?
 
Last edited by a moderator:
anahaki ya kugombea jimbo lolote wamesha mpangia Serukamba aende kwake na yeye atete jimbo kwa chama tawala CCM Nawala si ATC
 
Waha huwa hawayumbishwi na siasa nyepesi ndio maana kina Kafulila na kina Machali walipofukuzwa CDM walienda NCCR na wakashinda bila Shida.
 
Makete Kwetu

Hivi Mbowe alishamaliza kero zote za wana hai? Slaa alimalizj za karatu? Mjika za ubungo kamaliza? Lema naye za arusha mjini kamaliza?
Umesahau kuuliza na Kikwete alishamaliza za Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Mnafiki na mpenda sifa utamjua tu, kwao hajamalizana nao anavamia kwingine, kifuatacho ni kunyima kura akaangukie pua.

Tulieni sindano iwaingie, mmemfukuza wenyewe. Suala la kutokugombea jimbo ni ahadi ya muda mrefu wala sio wazo la leo. Toka kampeini za 2010 aliahidi ndo kipindi chake cha mwisho kugombea Kgm Kaskazini, sa kinachowawewesesha mapema ni nini? Kgm mjini wako ladhi jimbo waendelee kulitoa sadaka kwa ccm kuliko kutawaliwa na wachaga. kwani mmewanyanyasa sana waha na kuwatukana vya kutosha hawana haja na nyie.
 
anahaki ya kugombea jimbo lolote wamesha mpangia Serukamba aende kwake na yeye atete jimbo kwa chama tawala CCM Nawala si ATC

ivi mbona mnakua mashapu kuweka uzushi hadharani pasi na shaka yeyote? ?
Yani mtu kudanganya wala haimtii hofu utadhan hana dini? ? halafu ati na wala si ATC???? yani pumbafu sana wewe mwanamke..
 
Tulieni sindano iwaingie, mmemfukuza wenyewe. Suala la kutokugombea jimbo ni ahadi ya muda mrefu wala sio wazo la leo. Toka kampeini za 2010 aliahidi ndo kipindi chake cha mwisho kugombea Kgm Kaskazini, sa kinachowawewesesha mapema ni nini? Kgm mjini wako ladhi jimbo waendelee kulitoa sadaka kwa ccm kuliko kutawaliwa na wachaga. kwani mmewanyanyasa sana waha na kuwatukana vya kutosha hawana haja na nyie.

a naye muunga mkono uyu msaliti majority ni ccm. kwann msimpe nafas a kawa Mwenyekiti wenu badala ya jk kikwete...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom