Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,998
- 20,359
Chadema Kigamboni kimelaani vitendo vya kihuni na vya udhalilishaji dhidi ya Mwenyekiti wetu Taifa vinavyofanywa na Mkuu wa Mkoa bwana Paul C. Makonda,
Chama kimetoa tamko kuunga mkono msimamo wa Mwenyekiti Taifa kwamba hataitikia wito wa kipolisi uliotolewa na Makonda kinyume na taratibu ambapo wito wa kipolisi unatolewq na Afisa wa Polisi.
Chadema kinaunga mkono vita dhidi ya madawa ya kulevya, lakini kinapinga kwa nguvu zote kile kinachoitwa vita ya madawa ya kulevya inayofanywa na Makonda, Chama kinaamini kwamba Makonda ana agenda ya kisiasa na pia anawalinda wauzaji wa madawa ya kulevya kwakuwatajataja watu hovyo hovyo bila kufuata utaratibu wa kiupelelezi na kiuchunguzi.