Chadema karibuni mtwara!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,671
Nimekuwa na masikitiko makubwa kutokana na nguvu ndogo ambayo chama cha maendeleo na demokrasia chadema wamewekeza katika mkoa Mtwara. Napenda ifahamike kuwa Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo CCM Haitakiwi kwa asilimia zote. Hii ni kutokana na dhuluma mbalimbali za wazi zinazofanywa na chama tawala. Pia napenda kuufahamisha uongozi wa Chadema utakapofika mtwara kwenye ziara maalum ujitahidi kuondoa sumu za udini zilizo pandikizwa na CCM. Sumu hii ni ile inayoonyesha kuwa CHADEMA wapo kwa maslahi ya kanisa. Ni wazi kuwa sumu hii imepandikizwa na CCM. Hivyo ni ombi langu kwa UONGOZI WA CHADEMA uandae ziara maalum ya kwenda kuwazindua wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na sumu hiyo mbaya ambayo inapandikizwa na CCM.

Nina Imani na CHADEMA kwani ni chama pekee ambacho kimeonyesha nia ya kweli ya kupambana na matatizo ya wananchi. Ziara hiyo itawasaidia CHADEMA kuelewa dhulma kubwa wanayofanyiwa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Mwisho napenda kurudia tena, CHADEMA karibuni sana MTWARA!
 
Mimi naamini siasa ni kama iman huwa inaweza kukua au kudorora. Sasa kwa upande wa Mtwara nadhani imani yao kwa CDM inazidi kukua na hivyo mabadiliko yako karibu sana kwa nchi hii.
 
ni vigumu chadema kustawi mikoa ya kusini kwa jinsi walivyojipambanua, kusini ni kati ccm na cuf. na ndio ngome ya cuf.
 
Nimekuwa na masikitiko makubwa kutokana na nguvu ndogo ambayo chama cha maendeleo na demokrasia chadema wamewekeza katika mkoa Mtwara. Napenda ifahamike kuwa Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo CCM Haitakiwi kwa asilimia zote. Hii ni kutokana na dhuluma mbalimbali za wazi zinazofanywa na chama tawala. Pia napenda kuufahamisha uongozi wa Chadema utakapofika mtwara kwenye ziara maalum ujitahidi kuondoa sumu za udini zilizo pandikizwa na CCM. Sumu hii ni ile inayoonyesha kuwa CHADEMA wapo kwa maslahi ya kanisa. Ni wazi kuwa sumu hii imepandikizwa na CCM. Hivyo ni ombi langu kwa UONGOZI WA CHADEMA uandae ziara maalum ya kwenda kuwazindua wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na sumu hiyo mbaya ambayo inapandikizwa na CCM.

Nina Imani na CHADEMA kwani ni chama pekee ambacho kimeonyesha nia ya kweli ya kupambana na matatizo ya wananchi. Ziara hiyo itawasaidia CHADEMA kuelewa dhulma kubwa wanayofanyiwa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Mwisho napenda kurudia tena, CHADEMA karibuni sana MTWARA!

mtwara wanateswa na mfumo wa divide and rule wa chama cha mapinduzi.

ipo siku watazinduka usingizini.
 
Nina imani kubwa kabisa kuwa watakuwa wamelipokea ombi lenu wana mtwara,big up kwa kuwaeleza ukweli kuwa watu wa mtwara wanahitaji mabadiliko ya kisiasa
 
Safi sana mkuu,najua wakuu wa CDM tunao humu ndani kila cku ni vema wakazingatia mawazo yako mkuu najua yakisemwa yale yanayosemwa maeneo mengine ya tz basi wana Mtwara watakubali mabadiliko tuu
 
Twaja huko kaka usihofu kwani tunajua watanzania wanahitaji ukombozi toka magamba
 
Back
Top Bottom