Chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA)Kanda ya kati inakusudia kufanya mikutano ya hadhara mkoani singida kuanzia tarehe 3 hadi 11 agoast mwaka huu,lengo kuu la mikutano hii nimuendelezo wa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wa mkoa huu kwa lengo la kuwajengea ujasiri wananchi wa singida kuondoa uoga katika kudai haki zao,akiongea na wanachama wa chadema na wananchi kwa ujumla katibu wa chadema mkoani hapa amesema mikutano hiyo itaanzia jimbo la singida kaskazini tarehe 3-5,singida mjini tarehe 6,manyoni tarehe 8-11,mikutano hiyo itakwenda sambamba na vikao vya ndani na ufunguzi wa matawi,utakaongozwa na makamanda wakanda ya kati chini ya uongozi wa kamanda Tundu lisu