Chadema kama Jones dhidi ya Padavatton

Pamputi

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
982
724
Habarini wanabodi
Naamni mu wazima wa afya tele, leo nimekaa chini nikajikuta nakumbuka kesi moja mashuhuri sana kwenye sheria nilipataga kuisoma wakati fulani nikiwa mwanafunzi wa sheria chuo kikuu fulani na pia kusimuliwa na walimu wangu wa sheria (Contract Law) mwalimu C, K. Mtaki na Abdallah Gonze (Legal method) kipindi hiko. Kesi ya Jones v Padavatton (jones dhidi ya Padavatton)

Basi hii kesi inahusisha binti Jones na mama ake Padavatton ambaye alimwambia mwanae Jones ambae alikua anafanya kazi katika ofisi za ubalozi wa india nchini marekani Aache ile kazi ili akasome sheria katika chuo kikuu cha London uingereza na kwamba atakua akimlipa £200 kila mwezi kutokana na kumkatishia kazi yake ile nzuri

Binti akaumia sana lakn mama ake ambaye alikua anaishi trindadi akazid kumsihi binti akubali kuacha kaz, mwisho wa siku binti akaacha kazi kwel ili kutimiza matakwa ya mama ake na akaamua kwl kwenda kuanza masomo ya sheria kwnye chuo kile. Katika siku za awali mama ake (Padavatton) akawa anatuma kile kiasi alichoahid kwa bintiye lkn sasa, yule binti akiwa katikat ya masomo yake mama ake akaacha kutuma ile pesa kama walivyokubaliana kwa sababu eti binti aliolewa akiwa masomoni n.k basi binti akaamua kwenda mahakamani

Akamshtaki mama ake kwa kuwa Alimuharibia kazi yake kwa makubaliano kwmba atakua akilipwa
Pili amempotezea muda kwa sababu kipind chote akiwa anasoma angeshafanya mambo mengi sana lkn mama ake kampotezea muda, kw hy kutokana na hayo yote binti akaamua kushtaki lakini mahakama baada ya kusikiiza maelezo toka pande zote wakaja na Conclusion kwamba

Makubaliano kati ya jones na Padavatton yalikua ni makubaliano ya kifamilia zaidi ambayo hayana mashiko kisheria kw hyo mama mtu hana kesi ya kujibu.

Binti akakosa option, kapoteza kazi, kapoteza muda, kapoteza marafiki, kapoteza mambo mengi sana lakini mwisho wa siku hata mahakama ikashindwa kumtendea haki,

Chadema wamepoteza muda na wamazidi kupoteza muda kwa kuukubali umaarufu wa muda mfupi, kwa kukubali kuburuzwa na mihemuko isiyotokana na dhamira halisi za mioyo yao, na naamin siku watapokuja kushtuka itakua tayari ni too late kiasi ambacho hakitakuja kutosha kupata kile ambacho wangepaswa kukipata kwa muda mrefu kama wangejikita katika kujijenga katika mifumo yao.

Watalia kilio kama cha Jones

Pamputi 255
 
Wana macho lakini awaoni...

Wana masikio lakini awasikii...

Watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa...

Upinzani tz |||
 
Back
Top Bottom