CHADEMA jimbo la Segerea yaanza ziara

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
TAARIFA KWA UMMA

Sekretarieti ya jimbo la Segerea inawataarifu viongozi wote wa kata,wanachama na wapenda mabadiliko kwamba,katika kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kila siku za chama,imeanza ziara kwenye kata nane za jimbo la Segerea kukagua utekelezaji wa kazi cha kila siku za chama kwa kupitia ripoti zote za chama na mabaraza(BAVICHA,BAWACHA NA BARAZA LA WAZEE) pia itapitia mihutasari ya vikao vyote vya kikatiba na vya dharura pamoja na kutembelea matawi na misingi kwa kujiridhisha yale yaliyoko kwenye maandishi kama yanakwenda sambamba na kwenye field.

Ziara hizi tayari zimeanzia Kata ya Segerea siku ya 1/12/2012 na zitaendelea tena siku ya tarehe 7/12/2012 ijumaa sekretarieti itakuwa kata ya Kinyerezi na tarehe 8/12/2012 itakuwa kata ya Kimanga na tarehe 14/12/2012 itakuwa kata ya Tabata.
Kwa kata za Vingunguti,Kipawa,Kiwalani na Buguruni taarifa itatolewa tena ikionyesha tarehe ya ziara kwa kila kata.

Sekretatrieti inaomba ushirikiano kutoka kwa viongozi wote kuanzia ngazi za misingi,matawi na kata husika.

Pamoja tutashinda-M4CImetolewa na Katibu wa sekretarieti ya Jimbo la Segerea
 

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
Tunashukuru,hapa kikubwa ni ushirikiano wa dhati,umoja wa dhati,na mikakati ya pamoja.ni zoezi ambalo litafanywa kwa umakini sana ambalo litasaidia kupata majibu ya maswali mengi ikiwamo mpaka sasa kuna idadi ya wanachama wangapi kwa kila kila kata na jimbo zima,pia tutapima ni wapi chama kinakubalika zaidi na wapi hakikubaliki ndani ya kata 8 zote.kisha tutapata intervention ya kupata wanachama wengi zaidi kule itakapooneka tuna wanachama wachache.na mengine mengi.tuko pamoja

M4C
 

Rugaijamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2010
2,942
1,288
Mi nawapongeza sana makamanda huko Segerea, ni mkakati mzuri mno huu...ni vema kujipanga na kuweka mikakati ya kuimarisha chama mapema hasa ktk ngazi za chini ili hatimaye 2014 tuzoe mitaa, vijiji na vitongoji vingi ili tujihakikishie ushindi murua kwenye uchaguzi mkuu 2015....... PEOPLES' POWER
 

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
Mi nawapongeza sana makamanda huko Segerea, ni mkakati mzuri mno huu...ni vema kujipanga na kuweka mikakati ya kuimarisha chama mapema hasa ktk ngazi za chini ili hatimaye 2014 tuzoe mitaa, vijiji na vitongoji vingi ili tujihakikishie ushindi murua kwenye uchaguzi mkuu 2015....... PEOPLES' POWER
Asante mkuu,tuendelee kuunganisha nguvu na tuchague njia sahihi ya kubadilishana uzoefu,kupeana ushauri na hata kukosoana kwa staha na sote tufanye kazi kwa bidii bila kujali ni kiongozi wa ngazi yoyote au ni mwanachama,tukubali kutenga japo masaa mawili kwa siku ya kufanya kazi ya chama.
M4C
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom