The Fixer
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 1,365
- 599
Wana JF,
Habari za jioni !
Kwa bahati mbaya sana mimi sio mfuasi wa chama chochoote cha siasa kwa hiyo haya nnayoyaandika ni mawazo yangu tu binafsi yasiyokuwa na " interest " kokoote katika vyama hivi vikubwa Tanzania
Leo tumeshuhudia ufunguzi wa kiwanda kikubwa cha Cement huko Mtwara kama ambavyo TBC walionyesha mchakato wake na Waziri mkuu Pinda akiwakilisha kutoka pande zile, huu ni mkakati wa siku nyingi wa CCM ingawa ulichelewa sanaa kwani CCM kama chama kongwe kilitakiwa kijijenge kiuchumi miaka mingi sana iliyopita kutokana na fursa nyingi za uwekezaji zilizopo hapa nchini ni bahata mbaya tu CCM wako Wachumi wakubwa lakini ni wachumi wa vyeti na sio / hakuna uhalisia katika kuonyesha juhudi hizo
CCM;
¤ Wamechelewa sana kujenga vitega uchumi kama " Shopping mall " katika miji mikubwa
¤ Wamechelewa kuwekeza katika bahari na maziwa makubwa
¤ Wamechelewa sana kuwakeza katika machimbo ya madini, mafuta & gesi
¤ Wamechelewa sana kuanzisha hata Mabenki ya kibiashara kwa wakati
¤ Wamechelewa sana kuanzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara
Sasa kwakuwa mahasimu wao kwenye Siasa wanaowanyima usingizi ni CHADEMA na wanatakiwa kuwa na uchumi mzuri wao kama chama ( CHADEMA ) ili wawe na uwezo wa kuwafikia wananchi wanaotaka mabadiliko katika mfumo huu wa CCM wa kuendesha nchi uliogubikwa na UFISADI wa kila aina na kwakuwa ruzuku peke yake haiwezi kutosheleza mahitaji haya ndio maana kwenye mikutano mingi wamekuwa na watu wa kutembeza bakuli ili kupata nguvu ya kuwafikia watanzania wanaotaka mabadiliko na kuuza sera zao huko basi huu sasa ndio wakati na wao WAWEKEZE KATIKA BIASHARA KUBWA !
Mambo ya kuwalalamikia CCM na Bw Dangote wao yamepitwa na wakati, CHADEMA wanatakiwa kuja na mpango kazi wa namna ya kuwa na HQ yenye kukidhi mahitaji na yenye heshima kwa maana halisi ya Makao Makuu ya Chama kikuu cha Upinzani kuwe na jengo la kisasa lenye parking ya kutosha na kumbi kubwa za mikutanao hata minne under one roof.
CHADEMA na wao watafute mwekezaji watakae ingia nae ubia kupitia kampuni yao wao kama Chama . Mwekezaji huyo awe wa mafuta ama hata gesi na waende kufanya survey mikoa ya Tanga na hata Ziwa Victoria waone namna watakavyopata chanzo cha mafuta na gesi kwa maana kazi ya ukombozi ni kubwa na inahitaji uchumi mkubwa sana
Sifahamu kwasasa kama CHADEMA wanampango wowoote wa kuwa hata na TV/ RADIO stations kwani TBC ama Tv stations zingine sio za kutegemea sanaa kutoa coverage katika mikutano yao mbalimbali na hasa ile ya M4C na ile mikubwa ya kampeni, habari hizi za ukombozi ( kama utakuwa ni ukombozi wa kweli ) basi ziwe rahisi sana kuwafikia watu wengi sana na kwa wakati
Sifahamu kwasasa kama WABUNGE wa CHADEMA wanajibana kiasi gani kukijenga chama na ruzuku za chama kama chama katika kujenga walao MAKAO MAKUU yenye nafasi na sio ile iliyojificha pale Kinondoni na kupata uwezo wa kuwalipa Makamanda wengine watakao fanya kazi za kawaida za kila siku katika Makao Makuu zao za mikoani na wilayani hizi habari za kuwa wadau / makamanda wafanye kazi kwa kujitolea kwa kuwa chama bado ni kichanga zimepitwa na wakati, mtu hawezi kuacha kazi zake na kuanza kukitumikia chama full time bila ya kuwa na ugali wa watoto nyumbani na hii pia itachangia kuwa na uwezo kifedha kama Taasisi na kuondoa zile njaa za kukubali kuhongwa na CCM ili kubadili matokeo katika chaguzi mbalimbali kwani baadhi ya maeneo CCM wamepita kwasababu ya njaa za wana CHADEMA wengi sanaaa
Haya ni mawazo yangu tu wana JF yanaweza kuwa yakijinga vile vile maana mie sio malaika, CHADEMA inahitaji nguvu kubwa sana kiuchumi kama vile CCM inavyojitahidi kujikuza kiuchumi ili kushinda katika chaguzi zilizombele yao na hii itakuwa ni njia nyingine ya kukuza ajira badala ya kusubiri Serikali kuja kuyatenda haya yoote !
CHADEMA;
¤ Wana mpango wowoote wa kujikuza / kujijenga kiuchumi hasa katika hizi biashara kubwa kubwa ?
¤ Kwani kuna dhambi kwa chama kama taasisi kujijenga kiuchumi ?
¤ Wana mpango wowoote wa kutafuta wawekezaji kwenda kujenga kiwanda cha kusindika matunda katika ukanda huu wa Tanga ?
Badala ya kuwaona CCM kama watafuna nchi katika miradi yao mbalimbali hadi ya " parking " na wao watafute namna ya kujijenga kiuchumi na kuwa taasisi yenye nguvu kiuchumi maana naamini kuwa SIASA & BIASHARA bado havijawa vitu haramu hapa Tanzania kwenda pamoja hasa kwa taasisi zenye dhamana ya kuendesha vitu hivi.
Fursa zipo tele tatizo ni mtaji.... Tutafute mitaji na tuwekeze badala ya kunyoosheana vidole ! CHADEMA wanaweza pia kuwa na makampuni ya Ulinzi ili makamanda wenye uchungu na nchi walinde rasilimali zetu zinaibwa kwaushirika wa CCM
Nawasilishaa !
The Fixer,
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums