CHADEMA Jibuni Hoja hii...!!


Hapo ndipo niliseposema kawakebehi Chadema kwa kudai hata yy kasomea uchumi na wachumi wa CDM wanapachika namba tu,(HII NI DHARAU KWA MTAZAMO WANGU) na kasema hayo live bungeni!!

Yeye kadai kwamba ukilipa hiyo laki 3.15 itafikia t. 7 na ushehe!! kwenye t 9 itabakia t 1 ambayo haiwezi kuongoza serikali... hii ndiyo hoja ya ghasia!! Ikanushwe kwa mchanganuo mzuri hapa CHADEMA.
 


Kama alisema hivyo alibugu stepu:
Tuseme watumishi wako 500,000 na wastani wa mshahara kwa mtumishi uwe 1,000,000 unapata 6,000,000,000,000 kwa mwaka....hesabu rahisi sana. Wakipunguza maposho na gharama zingine za anasa wanabaki na pesa nyingi tu
 

Mkuu uko sahihi sana, lakini kwa nini CHADEMA hawakanushi??ujue hii itawafanya wananchi wasiiamini CHADEMA??
Hizo fig za Ghasia nadhani kajumuisha wafanyakazi wa level zote na si kima cha chini pekeyake!!
 

Nakupa somo wewe na kilaza mwenzio Hawa bint Ghasia Mke wa Fujo!
Tanzania inawatumishi wa Serikali wasiozidi laki nne (400,000) lakini kwa mujibu wa mkuu wa magamba wako 350,000 (rejea speech yake ya maarufu ya mbayuwayu). Kwa vile kuna viwango tofauti tofauti vya mishahara na posho za lazima fanya kila mfanyakazi anapata Tsh laki saba (700,000/=) kwa mwezi.

Wafanyakazi 400,000 X Tsh. 700,000 X Miezi 12 = Tsh 3,360,000,000,000/= (Trillion 3.36)
Changanya na michango ya mifuko ya jamii na Bima ya afya haizidi 20% ya hiyo (Trillion 3.36) utapata Tsh. 672,000,000,000/= (Bil. 672)

Ukijumlisha vyote yaani Tsh 3,360,000,000,000 + 672,000,000,000 = Tsh. 4,032,000,000,000/= (Trillion 4.032/=) Hii ndiyo gharama zooote za mishahara ya wafanyakazi na posho zao kwa viwango tofauti tofauti kama kima cha chini kikiwa Tsh. 315,000/=. Huyo Hawa Ghasia yeye hesabu yake ilikuwaje akapata utumbo?

Wewe naye umekurupuka, kwanza unaonekana hujui hata kuandika tarakimu sawa na waliokutuma wakipewa hundi ina tarakimu tofauti na maandishi tena hadharani!
[TABLE="width: 152"]
[TR]
[TD="class: xl65, width: 152"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 152"]
[TR]
[TD="class: xl63, width: 152"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 


Anko Tham uthithahau hethabu janga la taifa.......tarakimu si mchezo bana
 
Kitu kingeni ambacho Hawa Ghasia hakukisema hiyo hesabu ya mishahara ya CCM inajumlisha pia wafanyakazi hewa. Serikali inapoteza karibu Tsh 2 trion kila mwaka kulipia wafanyakazi hewa. Haya sion maneno ya CDM. Jana wabunge wa CCM Suleima Jafu, Dr. William Mgimwa, Michael Laizer etc. wameyasema. Kama una shaka na hao wabunge tafuta report CAG.

Hilo tu hata kabla hatujaenda kwenye kupunguza posho, ukubwa wa baraza la mawaziri, etc. Kama CDM wanaweza kudhibiti wafanyakazi hewa wa CCM tayari watakuwa kibindoni wame save Tsh 2 trion. Kama hawa Ghasia anasema ukweli afanye mdahalo na Suzana Lyimo, halafu mtajua pumba ni zipi na mchele ni upi. Huyu mama kwanza amelidanganya bunge hana degree ya uchumi. CCM kazi kujipa usomi wasiokuwa nao kama yule mwizi wa taulo hotelini eti anajiita Dr.
 

Mkuu una nyodo sana!! Halafu acha dharau unapojibu michango ya mtu!! Hivi utawezaje kulipa mshahara kima cha chini hadi laki 3.15 na yule wa kima cha kati laki 3 usimjumishe?? ina maana wa kima cha kati anazidiwa na wa kima cha chini?? sasa piga hesabu zako wa kima cha kati (laki3-4) na wale wa kima cha chini 3.15 halafu njoo tena...p.umbavu wewe!!
 

Tempers!........could land you with BAN
 
Nimeamini jamaa hafahamu kabisa mahesabu. Ukisoma hapo chini, unabaki mdomo wazi na kupigwa na butwaa.

Muacheni masikini wa Mungu ambaye MAGAZIJUTO hakupitia kabisa. Naanza kuamini kuwa Degree ya Ghasia ilisimamiwa na Salma Kikwete (Maelezo juu) maana unashindwa kabisa kuelewa mtu anapewa mfano mdogo na yeye anarudi na maelezo ya WAGAGAGIGIKOKO.

 
naunga mkono hoja kwani umakini ni utuluvu pia
Watu Makini huwa hawakurupuki, wanakokotoa na kupitia vielelezo vyao ili wakijibu wasitoe siasa bali watoe vitu venye ushahidi wa kutosha
 
Sipendi sana huu mjadala kwani unaweza kuiumbua serikali zaidi ya inavyofikiri. Ni kwali huyu Ghasia anataka ashushiwe data? Anawajaribu CDM au yuko serious? Namwonea huruma kwani hata mwaka jana budget ya CDM ilidhihirisha uwezo wa kulipa 315,000, iweje leo wawe (CCM) na ujasiri wa kuwahoji! Naomba kushangaa, wakuu.
 

Safi sana. Hata mimi huwa nafikiria kwamba kima cha chini kinaweza kupandishwa kwa kuongeza difference ya kima cha chini cha sasa yaani 135000 na 315000 ambayo ni 180000 ukamwongezea kila mfanyakazi inatumia fedha kidogo badala ya kutumia mfumo wa ukokotaji kwa asilimia. Mfano 180000 X 500000 = 90,000,000,000/=. Si unaona ni 90 bil tu. Yaani magamba utadhani hawana akili vichwani kabisa
 
jamani huyu mama ana mawazo mgando na wafuasi wake wa magamba niwavivu kufikiria. hakika hawa ndio wale waliokimbia hesabu shuleni. CDM wanachosema nikupandisha kima cha chini hadi 315,000 na siyo kupandisha mishahara ya ngazi kwa hiyo percentage. Pia namuunga mkono mdau Mndeme yakua na mapato ya kodi yatazidi (PAYE). Nadhani taifa lianzishe elimu ya lazma kwa wanamagamba wote
 
Angewasifia CDM kibarua kingeota nyasi, anamtumikia kafiri ili apate mradi wake ati!
Lakini cha ajabu pamoja na kuwaponda mtasikia wametumia bajeti mbadala na sera
za CDM katika kuongoza serikali yao! Tunawajua kwa hilo.
 
Sizinga, soma vizuri mfano wa Anko Sam,

Ametoa mfano watumishi wote walipwe 700,000/=, yaani amechukua makadirio ya kati, kwani wapo wanaolipwa chini ya hapo na wengine juu ya hapo sasa huo wastani aliochukua unaweza kuwa ndio base ya calculation.

pia punguza Jazba Hoja za Ghasia ni Ghasia kama jina lake, hakufanya mahesabu kwa umakini na ndio maana kaja na pumba, Chadema wakitaka wamjibu ila wakipenda wamwache na ujinga wake maana wanachi wanajua kufanya mahesabu.
 
Mkuu ile haikuwa HOJA ni vijembe sioni kama ni sahihi Kujibu hata vijembe
 
CCM haina jipya kwa wannchi wa TANZANIA,imetufanya leo tuwe hapa katika dimbwi la umaskini,tunaichukia CCM,ILANIWE.
 
siasa za bungeni.... !!!
 
majibu rahisi kwa swali gumu, umewashika pabaya mkuu, ha ha ha ha ha ha

Mkuu, mimi ninadhani badala kushabikia kwamba wameshikwa pabaya, ungefanya utafiti wa hiyo mishahara ya watumishi wa serikali. Kwa mfano, wako wangapi kwa ujumla wake, na ktk kila salary scale kwa ujumla huo wako wangapi? Na it's obvious kwamba katika kupandisha mishahara watumishi wote hawawezi kupandishwa kwa equal percentage. Kwa hiyo inayosemekana nyongeza ni almost 133% sasa huwezi kuwaongeza wote kwa percentage hiyo hiyo. Hivyo anayefikiri CDM wamechemsha nadhani yeye ndiye amechemsha kwa kupiga simple arithmetic badala ya kukokotoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…