Chadema itoe Tamko kuhusu Tanesco, EWURA; Wizara ya Nishati/Madini na dira ya Taifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema itoe Tamko kuhusu Tanesco, EWURA; Wizara ya Nishati/Madini na dira ya Taifa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Not_Yet_Uhuru, Dec 22, 2010.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  TANESCO ni nini? EWURA ni nini? na Nchi yetu inapelekwa wapi na Taasisi hizi??

  Ni hali ya Masikitiko makubwa, Uchumi unavurugika, Wananchi wanazidi kudidimia ktk dimbwi la kukosa huduma, ziwe za muhimu hasa zile zinazotegemea uzalishaji mdogo mdogo kwa kutumia nishati ya umeme kama ujasiriamali, huduma za mahitaji ya vyakula na vinyaji baridi mfano maziwa, maji, samaki, nyama nk. Ajira binafsi kama saloon, uchomeleaji nk; Vyote hivi vimekuwa vikitegemea sana mahitaji ya umeme ijapokuwa umekuwa ukipatikana kimkanda-mkanda, ila watanzania wamekuwa wakivumilia tu na kujiendeshea maisha yao ya kuokoteza na kujikwamua kiujasiriamali.

  Kitendo cha Tanesco kuvurunda tena ktk usimamizi wa mitambo kuwa eti baadhi kusemekana umeharibika, na kusasabisha adha kubwa kwa Taifa nzima kwa kukata umeme kila mara ni aibu na jambo ambalo limekuwa likitokea kila mwaka na kila wakati bila wahusika kuwajibika bali wao huachiwa tu kutoa 'ufafanuzi wa kisanii' ambao mara nyingi ni 'porojo tu za kujilinda nafasi zao na maslahi wa waliowaweka madarakani'. Haifai tena!

  Hii ni dhuluma, na usaliti mkubwa mno kwa taifa na wananchi wanaohangaikia maisha yao kila kukicha. Wanavutwa nyuma na utendaji uliooza, na Hakuna maendeleo yoyote kwa mtindo huu. Nchi itazidi kuangamia kwa umaskini sababu ya watu wachache wanaolindana.
  Watanzania wanahitaji dira na Mwelekeo wa hali hii. Na EWURA pasipo kujali maisha ya wa tanzania yanavyodhoofika, nao wamekubali msukumo wa TANESCO kuongeza bei ya huduma za Tanesco kuanzia mwakani. EWURA ni kwa maslahi ya nani? Tanesco ni kwa maslahi ya nani na ni ya nini Tanzania? EWURA ina maslahi gani kwa Watanzania?

  TUNAIOMBA CHADEMA itoe TAMKO na dira kwa Taifa hili. Na hata kama inafaa itangaze rasmi maaandamani ya Amani kwa nchi nzima kupinga kuangamia kwa nchi yetu! Tanesco ivunjwe na Wahusika wa EWURA na Wizara ya Nishati na Madini wawajibike. La sivyo watanzania kwa kiwango kikubwa wanazidi kukata tamaa mno na hawatasikia la yeyote kwamba wanaye watetezi wa maisha yao.

  Mungu ibariki nchi yetu. Naomba kuwasilisha.
   
Loading...