Shukrani A. Ngonyani
JF-Expert Member
- Feb 23, 2014
- 1,182
- 2,021
Ni aibu na ujinga kudhani CCM watang'oka madarakani mwaka 2015, ni mwehu anayeweza kudhani CCM itakubali kukabidhi nchi mwakani kama vijana wa taifa hili bado tuko gizani namna hii.
Tukifanya rejea ya chaguzi zote za nyuma CCM wamekuwa wakishinda kwa mlungula na ubabe wa hali ya juu, leo sioni kitakachobadilisha hali hiyo.
Mwaka 2000 kule Zanzibar wenzangu wa CCM inasemekana walishindwa kama ilivyo mwaka 2010(kwa maelezo ya mzee Moyo), kama ilivyo huku bara mwaka 2010 pale "LE PROFESSOR" alipoangukia pua alipokutana na kisiki cha Willbroud Slaa, lakini CCM wakatumia tena ghilba wakachakachua matokeo kupitia kwa wakala wa CCM wanaojiita Tume huru ya uchaguzi
Mwakani tunaingia kwenye uchaguzi tena huku mioyo ya wengi wakitambua CCM imechokwa hivyo kuipigia kura ni ubatilifu, na wenye akili na wenye macho huenda wakasita kuweka vema kwenye sehemu ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi, "Labda yule ambaye ana ubongo usioweza kujaa hata kijiko cha chai anaweza kuweka vema sehemu yenye mgombea wa CCM". kwani hali ya uchumi na maisha kwa sasa inakatisha tamaa na huenda ikawa ni nauli ya kuipeleka CCM kuzimu.
JE CHADEMA IMEJIANDAA KULINDA NA KUPOKEA USHINDI?
Inavyoonekana hakuna dalili ya mwakani CCM kuachia ngazi, wataendelea tu na ubabe wao na wizi wa kura kupitia wakala wao tume ya uchaguzi,
kwani hadi sasa bado wameweka mazingira ya kutaka kuhujumu uchaguzi kupitia uandikishaji wa wapiga kura kwani inapigwa miluzi tu huku tume ya taifa ya uchaguzi wakiwa wameweka kwapani tu daftari lenyewe.
Vijana ndio hulinda kura na kudai ushindi wa kweli ktk chaguzi zote za Afrika ila hapa kwetu vijana hawajajiandaa vyema hasa vijana wa CHADEMA wanaotakiwa kulinda kura hawajawezeshwa vya kutosha.
CHADEMA ilitakiwa ifanye organisation mapema ya kulinda kura ktk uchaguzi wa urais sio kuishia kulinda kura za diwani na mbunge tu. Kuacha CCM wajifanyie tu mambo watakavyo ni kumsusia nyani shamba la mahindi. Hakika wataharibu mazao yote shambani.
CHADEMA ikikenua meno kwa hili, MWAKANI CHADEMA itashinda ila CCM itatawala
Shukrani A. Ngonyani,
Novemba 06, 2014,
Tanga,
00255 767 942 204,
Ngonyani@naij.com