CHADEMA isitishe maandamano

CHADEMA isitishe maandamano

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,179
Reaction score
37,475
Heshima sana wanajamvi wote.

Kwanza napenda kuwajulisha wanajamvi wote Ngongo si mwanachama wa chama chochote cha siasa Tanzania ila ni mpenzi wa siasa.Ninaposema ni mpenzi wa siasa nina maana ninapenda kushiriki,kusikiliza na kushauriana masuala yote yahusuyo siasa bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.Kwahiyo unapochangia mjadala huu ni vyema ukijikita zaidi katika hoja.

Ni jambo lililo wazi Tanzania inapita katika kipindi kigumu sana tangu kuhasisiwa kwa taifa hili.Vikao vya bunge maalamu la kutunga katiba mpya vinaendelea mjini Dodoma huku baadhi ya wajumbe (UKAWA) wa bunge hilo wakisusia vikao hivyo kwasababu ambazo kwa kiasi fulani hata mimi nakubaliana nazo.Sina haja ya kueleza kwanini tumefikia hapa kwakuwa najua wengi wenu tunazijua sababu hizo ingawa kumekuwa na juhudi kubwa za kimkakati/propaganda za kupotosha kwa maksudi sababu zilizopelekea UKAWA kususia bunge la katiba.

Vyombo vya habari hasa vile vinavyomilikiwa na serekali na chama tawala vimekuwa vikipotosha ukweli kwa makusudi ya kupandikiza taswira mbaya ya UKAWA mbele ya macho ya jamii ya kitanzania hasa wale wasiopenda kuchambua mambo kwa undani.

CHADEMA sijui kama UKAWA wamo katika hii hoja ya maandamano wamekuwa wakipaza sauti za malalamiko na sasa wanataka kuanzisha maandamano nchi nzima kama sehemu ya kuonyesha kutorizishwa na jinsi mchakato wa kuandika katiba mpya unavyopaswa kwenda.Ni kweli bunge la Bwana Sitta limekosa viwango,limekosa ushirikishwa wa mawazo ya wananchi,limejivika kazi za tume ya kukusanya maoni,limekosa mjumuiko wa makundi yote (wanaCCM wametamalaki),limekataa mawazo ya wananchi,limekumbatia mawazo ya watawala.halina maana kabisaaaaa.

Ukweli ni kwamba sababu za kuandamana zipo nyingi sana lakini Ngongo wa JF anakataa maandamano kwasababu ambazo nitazieleza.

Maandamano hayajawahi kuleta mabadiliko chanya Tanzania badala yake yameacha makovu makubwa ambayo hatujawahi kuona matunda yake hata kidogo. Mji wa Arusha ni mfano mzuri wananchi waliandamana kudai uchaguzi wa haki wa meya wa Jiji la Arusha mpaka leo bado meya ni yuleyule na ikumbukwe kuna wananchi walipoteza maisha yao kwaajili ya kuhakikisha haki inapatikana.

Kwanini nakataa maandamano sasa.Nakataa maandamano kwasababu wananchi waliopoteza maisha yao kwaajili ya kuitikia wito wa maandamano mpaka leo hawajatendewa haki.Kuna wanawake leo hii ni wajane wana watoto wanashindwa kupata elimu,afya,lishe stahiki kwakuwa hawana Baba wa kuwatunza.CDM kama chama mpaka leo hawajachukua hatua za kisheria kuhakikisha walioshiriki kutoa uhai wa raia wasiokuwa na silaha wanafikishwa mahakamani,sijasikia wanasheria wa CDM wakisubutu kuanzisha mchakato wa kuishitaki serekali ICC kwa mauaji ya raia.

CDM ilidai ina mkanda wa watu walioshiriki kurusha bomu uwanja wa Soweto Arusha,tena walidai polisi walishiriki kuhakikisha mrusha bomu hakamatwi na raia kwa kurusha risasi ili kumkinga asikamatwe.Siju huo mkanda umewekwa kwaajili gani wakati inajulikana kuna wananchi walipoteza maisha yao pasipo sababu za maana.Ikiwa CDM kweli ina mkanda ni kwanini mpaka leo bado imeukali inasubiri nini kwaajili ya manufaa ya nani au ndio mtaji wake mwaka 2015 ?.Vipi waliopoteza maisha au baada ya kuzikwa na kupiga mapicha za mazishi ndio basi.

CDM iache kucheza na maisha ya watanzania kama kweli inataka maandamano lazima watueleze wananchi walipoteza maisha wamefanyiwa nini ?.Tunajua upande wa serekali imefanya nini kwa makamanda wa mikoa yote yalipofanyika mauaji wengi wamepandishwa vyeo kwa kazi nzuri na njema ya kusimamia mauaji ya wananchi upande wa CDM watuambie familia za waanga wa maandamano na mikutano yake wamewafanyia nini ?.

Naomba kuwasilisha.
 
Daaah hizo aya 2 za mwisho!!!!! habari hii ina ukweli na ni vizuri kutokuwa biased. chdm ijibu hizo hoja kwanza maana ninachokiona ni kwamba kwa maagizo ya ccm, polisi wako tayari kuua raia kama walivyofanya hivyo niwazi kwamba njia hii itakuwa ni ya umwagaji damu.

Naishauri chdm wapige akili waje na mbinu mpya kama ya kufanya mikutano na kuelimisha umma juu ya kile kinachofanyika bmk. Mbinu hii italeta mafanikio makubwa sana kwani sasa ivi ni wengi wanaounga mkono ukawa. Nyerere hakuwahi kufanya maandamano lakn bado tuliupata uhuru. Tunahitaji kutumia akili zaidi kuliko nguvu

Asante mkuu kwa mawazo mazuri nadhani wahusika watapita hapa na kuyaona
 
Isitishe maandamano kwa faida ya nani? Mbona kila mmoja kaingia upepo? Fedha inayoliwa Dodoma ni nyingi sana .....haivumiliki......
 
Hamna haja ya kusitisha maandamano kwa ajili ya masilahi mapana ya nchi.
Hivi Ngongo hujajiuliza kwa nini nchi kama Iraq imeendelea na mapigano baada ya uvamizi wa Marekani? Au unaona Wairaq wangesurrender dhidi ya dhuluma wanayofanyiwa na mabeberu?
Nchi nyingi zimepata uhuru kupitia maandamano, na kama chama kikianza kushughulikia matokeo ya maandamano kama vifo na vilema kwa kiwango unchotaka wewe kingiweza kutokana na rasilimani fedha na watu ? Sio kwamba ccm wangekutumia mwanya huo ili kukiondoa chama kwenye Njia kuu na kukifanya kipoteze mwelekeo?
Badala ya kupinga maandamano,ni vizuri kupinga ccm na polisi kuzuia maandamano cha msingi yawe ni ya amani na yasiyoambatana na uharibifu wa mali za watu,
 
Mkuu Ngongo uko vizuri "You make my day" mawazo mazuri sana njiro kuna vichwa BIG UP....
 
Last edited by a moderator:
Kitu muhimu ni kuona hao waliochakachua maoni ya wananchi kama wana uhalali wa kufanya hivyo kwa kutumia wingi wao na siyo kuona umuhimu wa hoja. Wanaosababisha yote haya ni chama tawala kutumia mabavu kushnikiza mambo yenye maslahi kwa chama chao.
 
[h=2]Wapigwe tu ya Pinda, sasa ifanye kazi.[/h]
Natoa wito maalum kwa jeshi la polisi nchini na dola kwa ujumla, kuwa wahuni watakaoandamana na kuleta vurugu popote hapa nchini wapigwe tu. tumechoka. wafinywe ipasavyo...hii ni cheap politics kucheza na maisha ya watu. Washughulikiwe.​
 
Every revolution has sacrifices; hakuna mapinduzi yasiyokuwa na wahanga! mapinduzi yoyote dunia yamefanikishwa na watu jasiri wenye maonu mapana na mioyo mikubwa sio wenye roho biskuti kama wewe! siasa za hisia za kusikilizia kwa mbali unazofanya wewe hazitufai; kaa pembeni wanaume watende kazi utadandia bogi huko twendako. Bs.
 
Kaulize Syria wameandamana kwa muda gani na je haki yao imepatikana au bado. Haki haipatikani kwa gharama rahisi km unavofikiri ww. Wapigania Uhuru na haki duniani kote walitangaza hata mbele ya hadhara kuwa wako tayari hata kufa lkn sio kuishi kkt udharimu wa namna ile na ambao ndo tunauona kwenye utawwla huu wa ccm. Sinahaja kuwataja wapigania uhuru na haki waliouawa na kufungwa jela.
Mtu mm ww sanasana ni tunda la udhalimu tunaopinganao, siajabu ukawa Mtoto au ndugu au rafiki wa wasira kinana nape mwigulu kikwete sitta na wadharimu wengine wote
 
Maandamano yana faida ktk kuleta mabadiliko na hii imetokea dunia nzima ktk vita dhidi ya udhalimu .....lakini Chadema ambao ndio viongozi wa mapambano haya wameshindwa kusimamia kile ambacho watu waliotoa maisha yao,waliobaki vilema walitegemea ........mauaji ya Arusha yamesahaulika ........tumeambiwa kuna mkanda wa tukio lakini imebaki historia .......Lazima Chadema wafahamu matokeo ya vita hii ili kuwa tayari kupambana kuhakikisha haki itapatikana kwa wahanga badala ya kuishia kutoa matamko yasiyo na matokeo yoyote ......

Kama hatuwezi kudeal na matokeo ya maandamano kwa udhalimu wa CCM bora kutafuta njia nyingine ya kuleta mabadiliko ......naunga mkono maandamano lakini yatayokuwa yenye tija na mabadiliko yaliyokusudiwa .......
 
Kila chama kina washauri,hawaendeshwi na watu kutoka nje! Ishia kuumiza vidole kwa kubonyeza button tu
 
U have a point Ngongo...hii ni kwa kutokuwa biased kabisa...Naipenda CHADEMA lakini inatakiwa ifanye kitu kwa hawa watu waliotoa sadaka maisha yao
 
Daaah hizo aya 2 za mwisho!!!!! habari hii ina ukweli na ni vizuri kutokuwa biased. chdm ijibu hizo hoja kwanza maana ninachokiona ni kwamba kwa maagizo ya ccm, polisi wako tayari kuua raia kama walivyofanya hivyo niwazi kwamba njia hii itakuwa ni ya umwagaji damu.

Naishauri chdm wapige akili waje na mbinu mpya kama ya kufanya mikutano na kuelimisha umma juu ya kile kinachofanyika bmk. Mbinu hii italeta mafanikio makubwa sana kwani sasa ivi ni wengi wanaounga mkono ukawa. Nyerere hakuwahi kufanya maandamano lakn bado tuliupata uhuru. Tunahitaji kutumia akili zaidi kuliko nguvu

Asante mkuu kwa mawazo mazuri nadhani wahusika watapita hapa na kuyaona


mikutano gani jamani mnayotaka ifanywe na chadema kwa sababu hata hiyo mikutano wanawekewa ngumu kuifanya wakiambiwa wanachochea vurugu na kuondoa amani ya nchi sasa jema litakuwa nini? njoo na wazo jipya hili pia ulilolitoa lilishashindikana
 
walaumu polisi kwa kuwauwa raia,ushahidi unatunzwa na utatolewa tu kwa chombo huru
 
Kwanini chadema wanacheza na amani, Kwanini hawasubiri ulingoni mwakani?wameingiwa na mashaka gani kuhusu uchaguzi wa mwakani, na ni Kwanini serikali inasuasua kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi hawa,lawama kubwa itaiendea serikali kama itawaacha wafanye watakavyo.
 
Ni kweli mkuu wangu lakini waanga siku zote wanakuwa wananchi wa kawaida masikini ohoe hae sijasikia kiongozi wa CDM katwangwa risasi au huo ni mkakati wa hivi vyama kutuua raia tusiokuwa na hatia ?.

Every revolution has sacrifices; hakuna mapinduzi yasiyokuwa na wahanga! mapinduzi yoyote dunia yamefanikishwa na watu jasiri wenye maonu mapana na mioyo mikubwa sio wenye roho biskuti kama wewe! siasa za hisia za kusikilizia kwa mbali unazofanya wewe hazitufai; kaa pembeni wanaume watende kazi utadandia bogi huko twendako. Bs.
 
Back
Top Bottom