HOJA YA KIGWANGALA KUWATAKA CHADEMA WASIWEKE MGOMBEA ARUMERU MASHARIKI KAMA ALIVYOIBANDIKA KULE WANABIDII:
Ndugu,
Nimejifikiria sana na kuona kwamba uwezekano wa CHADEMA kushinda jimbo la Arumeru East ni mdogo sana. Wataishia kupoteza fedha zao nyingi, muda na kuathirika kisaikolojia. Badala ya kutunza nguvu zao na kujipanga kwa ajili ya 2015 wanatunisha msuli kupambana na chama dume CCM. Mimi nimejiuliza maswali; hivi hawa wakishinda wanakuwa wameongeza nini? Nikaona kwa CCM ni muhimu kwao kushinda jimbo hili ili kulinda heshima ya Marehemu Sumari aliyetangulia mbele ya haki. Nikaona kwa precedence hii kuna umuhimu wa CCM kuendelea kuliwakilisha Bungeni jimbo lile kwa lengo la kulinda heshima tu hiyo basi, maana hata wakishindwa haina maana yoyote kubwa kwenye demokrasia ya ndani ya Bunge, maana tayari CCM ina majority, na majority ndiyo inatawala! Gharama ya uchaguzi mdogo inakadiriwa kufikia takriban bilioni 19! Kwa sababu gani, hii ndiyo gharama ya demokrasia kwenye nchi yenye changamoto nyingi za kiuchumi kama Tanzania, kwa faida ya nani? Kwa nini sasa CCM wenyewe ambao walishinda uchaguzi uliopita wasipewe fursa ya kuteua mtu na kumuweka pale? Hata aliyekuwa wa pili kwenye kura za maoni wa wakati ule?
Hapo sasa inakuja hoja ya uzalendo. Nchi ina changamoto ya pesa na mahitaji makubwa ya wananchi, kwa nini tunai-expose kwenye kuingia gharama kubwa kiasi hiki leo hii ili kuweka mbunge mmoja tu? Pili, chaguzi ndogo zinapoteza attention ya wananchi na kila kitu sasa kinakuwa ni uchaguzi tu, kwa nini tusiliepuke hili na kutumia muda huu kama Taifa kujadili mengine ya maendeleo zaidi kwa nchi? Tayari CUF wametangaza kutoweka mgombea. Sijasikia vyama vingine vikiwa na ratiba ya kuingia kwenye mchakato zaidi ya CHADEMA, sasa kwa nini na wao wasiihurumie nchi wakaacha kuweka mgombea tuka-save gharama hizi?
Rai yangu, vyama vya upinzani tumieni busara, zuwieni pesa
Wakatabahu,
HK.