WANANCHI wametakiwa kutobabaishwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na chama hicho kutokuwa na nguvu ya umma, na badala yake wajikite zaidi katika kuijenga nchi kwa mshikamano bila kubagua itikadi za vyama.
Aidha, viongozi wakuu wa Chadema wametakiwa kushukuru angalau kwa kuambulia ushindi katika majimbo 23 kati ya 239 ya uchaguzi nchini wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka jana.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Stevin Kazidi, wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Kia wilayani Hai mkoani hapa, katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi na wanachama wa chama hicho kwa kuichagua CCM kuongoza nchi.
Kazidi alisema wananchi wanahitaji kutambua kuwa Chadema haina nguvu yoyote ya Umma, na kwamba chama chenye nguvu ya umma ni CCM kutokana na kuongoza nchi na kuwa na idadi kubwa ya wabunge.
"Watanzania hawajazoea vurugu kama za Chadema wanaotafuta madaraka kwa nguvu zote…uchaguzi umemalizika na kila chama kilipewa muda wa kufanya kampeni zake, wananchi walikata mzizi wa fitina nani anafaa na nani hafai ndo maana CCM ikashika
madaraka, kinachotakiwa ni kutekeleza mahitaji ya wananchi na si kuwaingiza katika malumbano ya siasa," alisema Kazidi.
Alikitaka Chadema kushukuru kwa nafasi walioipata ya kuwa na wabunge 23 kutokana na wananchi kupiga kura za hasira kutokana na CCM kusimamisha wagombea wasiokubalika na kuondoa chaguo la wananchi, na kudai kuwa wananchi hao hawakukichukia chama bali mgombea aliyesimamishwa kugombea.
"Mbowe na chama chake wana majimbo 23 kati ya majimbo 239 wakati usiku na mchana wanazunguka wakisema wana nguvu ya umma, je hapo kuna nguvu ya umma kweli…
"Wananchi mnatakiwa kutambua muda mwingi viongozi wa Chadema wanatumia
kuzunguka kwa maandamano bila kutekeleza ahadi zao, lakini serikali inayoongozwa na CCM inaendelea kuwahudumia wananchi wake bila kubagua ni wa chama kipi," alisema Kazidi Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga, alisema wananchi wanahitaji kujipanga
upya kwa kufanya maamuzi ya kutowachagua viongozi wanaosusia vikao vya Bunge ambavyo vinasikiliza kero zao, hatua inayowafanya kutotatuliwa matatizo yao kwa vile viongozi hao hawawasilishi malalamiko yao.
"Kazi ya viongozi wa Chadema ni kupinga maendeleo ya serikali yanayoletwa kwa wananchi pamoja na kususia vikao vya Bunge ambavyo hutoa fursa ya kusikiliza matatizo ya wananchi na kuzitatua.
"Tabia ya viongozi hawa inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi, ikizingatiwa sasa chama hicho kipo katika maandamano badala ya kuwahudumia wananchi," alisema Mtenga.
source: habari leo

Na tume ingekuwa huru mbona chadema ingezoa yote na urais mwaka huu!
Na hao washukuru kuww wao ndio wanaounda tume vinginevyo wangekuwa wamesahaulika huko...
Yaani uchaguzi umeisha miezi mitatu iliyopita CCM wako hoi,mpaka leo hii CHADEMA utafikiri ndo chama kilichopo madarakani,wabunge 23 wa CHADEMA wanawatoa jasho CCM yote kweli wingi sio hoja,hawajui kuwa jinsi wanavyozidi kuiongelea CHADEMA ndo wanazidi kuipa umaarufu.CCM wameingia choo cha kike.
Kwa kweli sioni kama 2015 chadema atafanikiwa hata viti vitano nchini hasa kwa mwendo huu.