Chadema iringa watafuta fedha kusaidia majeruhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema iringa watafuta fedha kusaidia majeruhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Averos, Jan 11, 2011.

 1. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Katika hatua nyingine, Chadema kimeanza kutembeza bakuli kwa wananchi kwa ajili ya kukusanya michango ya hali na mali ya kuwasaidia majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ili kupata matibabu ndani na nje ya nchi kutokana na hali zao kuendelea kuwa mbaya.
  Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mount Meru na Seliani jijini Arusha.
  Uamuzi wa kukusanywa kwa michango hiyo katika Manispaa ya Iringa ulitolewa jana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, Peter Msigwa, wakati akitoa tamko la chama hicho kulaani vurugu zilizotokea mkoani Arusha na kusababisha vifo na majeruhi.
  “Tunawaomba wananchi wa Iringa wenye nia njema na mapenzi kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema watuunge mkono kwa kuchanga fedha kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi waliolazwa,” alisema na kuongeza:
  “Wengi bado wanazo risasi mwilini na wanahitaji kupelekwa katika hospitali nyingine kubwa ndani na nje ya nchi.”
  Wakati huo huo, Chama hicho kimesema kimeshangazwa na hatua ya Pinda kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kuhusiana na vurugu zilizotokea mkoani Arusha na kudai kuwa kimya hicho kinaashiria kwamba serikali iliyopo madarakani imegawanyika na viongozi wake hawana dhamira ya kweli ya kuwaongoza wananchi.
  “Waziri Mkuu ana kigugumizi kuhusu sakata la Arusha,amekaa kimya na hajasema lolote wakati jambo hili liko katika mikono yake, Pinda kukaa kimya ni ishara kwamba serikali haina viongozi wenye dhamira ya kweli ya kuwaongoza wananchi...Idadi ya waliokufa ni zaidi ya iliyotolewa na hata mwisho wa siku hata hao Polisi watanufaika na haya tunayodai kwa haki,” alidai Msigwa, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini.
  Aidha, chama hicho kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, (RPC) Thobias Andengenye, na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo (OCD) kujiuzulu mara moja kutokana na kukiuka haki za binadamu.
  Mchungaji Msigwa alisema kuwa Chadema Wilaya ya Iringa ipo katika maandalizi ya kufanya maandamano makubwa kulaani unyama uliofanywa na Jeshi hilo hata kama hawatapewa kibali cha kufanya hivyo.
  “Tutaandamana hata kama wasipotupa kibali ila tutawapa taarifa kabla ya saa 48, hatutaogopa mabomu wala risasi…watawala wanapochoka kutatua matatizo au kutawala kibusara, historia inaonyesha kwamba hutumia nguvu (bunduki na mabomu), kwa hiyo sisi tunataka ukombozi na tutaandamana kwa amani,” alisema Msigwa.
  Nipashe
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  safi sana peter msigwa wewe ni mpiganaji wa kweli!!
   
 3. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Msigwa ni CDM au mwanaharakati? Mimi nafurahi kuwa CHM wametambua they are responsible for the incident, ubabe wa Mbowe na Lema hautasaidia chochote. Nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa ndani CHM kuwa hawakumruhusu Mbowe kwenda Mwanza kwasababu ni Mbabe na kwenye level ya uongozi aliyonayo hatakiwi kuwa mbabe anatakiwa kumwaga sera tu kama afanyavyo dr. slaa au zito na ndio maana zito akapewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa meya mwanza na alifanya kimyakimya in 1.30 hours ameshamaliza kazi. Ukweli ni kwamba CHM tutaambulia unaibu meya tu tena siyo leo ni mpaka uchaguzi mdogo wa kumchagua diwani mpya ufanyike maana kisheria ukishahama chama na udiwani umeuacha.
   
 4. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Well said!!!!!
   
Loading...