CHADEMA ipo hatarini

Mpaka sasa sijajua kinachojadiliwa ila nadhani nakiona kinachobishaniwa! Pole pole ndiyo mwendo TUTAFIKA TU!!

Hakuna mabishano, ila kulikuwa na sindano moja tu ndani ambayo wengi waliimeza wakidhani ni nofu ilipofika kwenye koo ikagoma kwenda, sasa wakawa wanatema mate au na kufanya wawezalo ili waiteme, si mabishano ila kutiana munkari.
 
Hakuna mabishano, ila kulikuwa na sindano moja tu ndani ambayo wengi waliimeza wakidhani ni nofu ilipofika kwenye koo ikagoma kwenda, sasa wakawa wanatema mate au na kufanya wawezalo ili waiteme, si mabishano ila kutiana munkari.
Utu uzima dawa na kabla hawajaliita jando ni tamaduni duni wengine tulikuwepo huko!! NAANGALIA!!

 
Mpululu, wewe ni kama yule aliyeanzisha uzi, huna tafiti lakini unataka kulazimisha kile unachokifahamu wewe ndio uwe utafiti, Dar Es Salaam watu wamejawa na woga kutokana na maisha na shughuli zao kila siku, lakini wanakipenda chama na wanakichangia chama mfano jimbo la Kinondoni na Segerea huko ambapo Tundu Lissu alikwenda Chadema ni kama haipo lakini ukifika wakati wa Uchaguzi chadema inajidhihirisha kutokana na matokeo ya kura

Jambo la msingi na ambalo linaigharimu chadema ni ulinzi wa kura, na najua viongozi wa chama wanalijua hili na wameshalifikiria na tayari lipo kwenye utekelezaji na ndio maana kuna mafunzo yanataraji kutolewa kwa vijana na wamama (BAVICHA & BAWACHA) naimani itakuwa agenda

Sitaki kukubali ushauri kwa chadema itafute mbinu za shortcut ili ishinde, kila jambo jema linafuata taratibu na ndio maana hata ngano haipandwi leo ikavunwa kesho itaanza jani, mche, suke, suke-pevu kisha mavuno sasa huyu anayelazimisha CHADEMA iache process hiki sio chama cha uhaini

Kuhusu matokeo ya chaguzi, imeonekana wazi na kama nilivyotangulia kusema hapo juu, chadema inachokikosa ni ulinzi wa kura, Chadema itakapotoa mafunzo na kukabiliana na kila uzandiki wa CCM, watu wa Daresalaam wakaacha woga, na wakajitokeza kulinda kura Chadema tunashinda 90%

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema

Joash R. Mussa
 

Mkuu ni vyema ukatuomba wana JF msamaha yakaisha; Thanx Lord, Dr. Slaa amekushtukia kwani mpango wako ulikuwa ni kututoa kwenye mstari;

UHASAMA wa taifa (TISS) ni vyema mkazingatia maadili ya kazi yenu kuliko kutumiwa na chama TWAWALA.
Hivi nyie hamfikirii baada ya uchaguzi mkuu unao tarajiwa kufanyika nchini kote mwaka 2015 mtaficha wapi nyuso zenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…