Tunashukuru uchaguzi umemaliza na mshindi ameshatangazwa. Pongezi CDM, pongezi Nassari, pongezi wana Arumeru kwa kushinda, mlistahiki - Hongera sana!
Lakini wakati wa kampeni, tuliwasikia viongozi wa vyama vikuu vilivyokuwa vinachuana kila kimoja kikidai kuwa na haki kuliko chengine, kiasi cha kutambiana "piga, ua (more or less), lazima tushinde na tukishindwa hatukubali".
Mshindi kapatikana, je CCM wameyakubali matokeo? Na hawatazua zengwe lolote?
Na kama ingekuwa kinyume chake, CCM walitangazwa washindi, CDM wangechukua hatua gani?
Naomba wanavyama, wapenzi na mashabiki husika watoe maoni yao.
Ushindi wa chadema Arumeru ni ushindi mkubwa sana kwa Jakaya Mrisho Kikwete na CCM kwa mwenye kufahamu.
Kupata jawabu la swali lako tuangalie historia
Kote huko waliamini haki haikutendeka, na kote huko hawakuleta vurugu japo hawakuridhika
- Chadema walishindwa Biharamulo
- Chadema walishindwa Kiteto
- Chadema walishindwa Busanda
- Chadema walishindwa Igunga
Historia hiyo inakuambia Chadema ni chama cha aina gani
KAma hapo juu.Hii inakubalika Mkuu!
Ni angalizo zuri.Haijashindwa kwa hiyo hakuna maoni....
Ikiwa kuna uhakika hakukupita uchakachuaji, huyasikii hayo. Mara ngapi CDM imeshindwa na pale wanapokuwa wanahakika wameshindwa kihalali huwasikii kusema lolote?ungesikia ccm wameiba kura.
Pengine suali ulilifahamika vibaya, lakini hayo uliyoeleza ndiyo ambayo nimekuwa nikiyaona na lengo langu lilikuwa kuwachokonoa wenye mawazo tafauti na hayo.Kupata jawabu la swali lako tuangalie historia
Kote huko waliamini haki haikutendeka, na kote huko hawakuleta vurugu japo hawakuridhika
- Chadema walishindwa Biharamulo
- Chadema walishindwa Kiteto
- Chadema walishindwa Busanda
- Chadema walishindwa Igunga
Historia hiyo inakuambia Chadema ni chama cha aina gani
Hapa mimi si katika ya hao wenye kufahamu. Ufafanuzi plz!Ushindi wa chadema Arumeru ni ushindi mkubwa sana kwa Jakaya Mrisho Kikwete na CCM kwa mwenye kufahamu.
Hili la mwisho nimelipenda. Licha ya kuwa CDM imeshinda, lakini kwa matusi aliyomwaga Lusinde, kuna ulazima wa kumshitaki ili iwe funzo kwa wale wote wanaohisi "mdomo choo ni mtaji."CHADEMA walishasema, kama watashindwa basi washindwe kwa halali na hawana shida juu ya hilo. Ambacho CHADEMA walisema hawakubali ni matokeo ya kuchakachua. Na ushahidi upo kwamba CCM walifanya kila mbinu kutaka kuingiza kura za bandia, ni bahati tu kwamba vijana wa CDM walisimama imara. Hii yaweza kuwa ni ushahidi kwamba hata Igunga, Biharamulo na Busanda pia CCM iliingiza kura za bandia. As far as CDM wameshajua mbinu ya CCM na wamejua namna ya kujilinda basi yafaa wadumishe mfumo waliouanzisha. Bila kusahau kumpeleka Lusinde mahakamani.
Pamoja sana Mkuu. Mara zote nimekuwa ni mwenye msimamo wa kuwa karibu na wapinzani wako ili kujua mbinu zao......nadhani ungeongeza kwa kumuelewesha muulizaji kuwa experience ni mwalimu mzuri sana. inamfundisha mtu kutorudia pale alipofanya makosa awali (kwa mfano kutozuia vema wizi wa kura). experience iliyotokana na hizo by-elections ulizozitaja hapo juu product yake ni hii success story ya arumeru!
Lengo langu mkuu lilikuwa/ni kusikia upande wa pili wangesema nini ili tupate kuwarushia madongo ya hoja; bahati mbaya inaonesha wamenuna kiasi ambacho leo JF wanaiona chungu.Sijajua lengo lako au pengine tumeishi kwa kudhani kuwa bila MAGAMBA tutakufa na jua kali. Jibu tumezoea kuonewa hivvyo tunge na tunaendelea kujipanga kwa 2015.