CHADEMA inaunga mkono Rasimu ya Katiba mpya - Mbowe

Serikali tatu si tu gharama bali pia ni ufukara wa mawazo ya kutatua matatizo yetu.serikali mbili pia si nzuri, zanzibar inaweza kutokuwa na rais na ikawa na mamlaka kisheria ya kuendesha mambo yake chini ya mamlaka fulan
 
Ben Saanane,

Ni ache hizo vipi ndugu yangu wakati mnatofautiana hata kuwayumbisha wafuasi wenu, kwa nini mlitaka Prof. Baregu ajitoe kwenye ujumbe, na kwa nini mlitishia kujitoa kwenye mchakato wa katiba.

Kwa hiyo mnataka CDM waipinge rasimu-katiba ili wawasaidie kufikisha ujumbe wa kuikataa?? safari hii tunashuhudia chawa tawala kikijipinga chenyewe.tume ya warioba ilitokana na uteuzi wa mwenyekiti wenu wa chama iweje leo mpinge wakati mwenyekiti tayari kasifia.tumieni bongo na si masaburi
 
kwani ni lazima kila mtu aunge mkono serikali tatu? Inawezekana wale wanaodai serikali moja wana hoja zaidi kuliko wanaodai serikali tatu. Kutofautiana huku haina maana wenye kudai serikali tatu basi wanaitakia tanzania mema zaidi kuliko wanaotaka serikali moja.


mwanakijiji hiyo serikali moja unayoipigania wewe haikuwezekana toka muungano uanze, serikali mbili ndiyo hiyo inataka kujinyonga wakinawarioba wanakimbia kuweka stuli au kukata kamba isife, serikali tatu ndio kuurudisha muungano hospitali kwa kunusurika kifo.

Usinganganie tu msimamo wako wakati hauna wafuasi.
 
hivi CDM si ilikuwa na mashaka na tume ambayo wao walikuwa wanaiita ya warioba?? leo imekuwaje?? au walikuwa misinformed? mana nakumbuka walimtaka prof baregu ajitoe, hadi wakamuundia na tume na kumkalia vikao bagamoyo!!! kukurupuka bwana, kweli hakuna faida............
 
Katika maswala nyeti ndani ya chama kwa mstakabali wa nchi kama hili la katiba, CCM huwa inaonyesha tofauti kubwa na vyama vingine vya siasa.

Hapa ndipo nidhamu ya chama inapotakiwa kufanya kazi ndani ya corrective responsibility. CCM kwa hili wanastahili pongezi.

Hata wale waropokaji ndani ya CCM huwezi kuwasikia kwenye maswala kama haya. CCM kwa sasa wako kimya kana kwamba hawajui kile kinachoendelea katika mchakato wa katiba.

Chama cha CHADEMA ambacho watu wangetegemea kiwe na nidhamu kutokana na kuwa na nafasi ya kuyajua makosa ya CCM na kujifunza, ndiyo kinakuwa na tatizo la political discipline. Mpaka sasa kauli mbali mbali za viongozi wake tumeishazisikia kuhusiana na rasimu ya katiba bila kujua kama ni kauli za chama au za kwao binafsi ikichukuliwa zinatolewa kwenye majukwaa ya siasa ili mladi kila mmoja anasema kwa kadri anavyopenda.

Ama kweli kijana ni kijana tu, na mzee ni mzee tu.
 
Back
Top Bottom