Kabla CCM haijaanza kufungua matawi nje ya nchi kitu cha kwanza kilikuwa ni kufanya marekebisho ya katiba ili ufunguaji wa matawi hayo ufanyike kwa kufuata katiba ya chama. Ndio maana katika katiba ya CCM sehemu ya tatu, Fungu la kwanza, 22 (1) (i-ii) kuhusu mashina ya chama, inaeleza kuwa kutakuwa na mashina ya ndani ya nchi na nje ya nchi. Katika fungu la pili, 31 (1) (d), imeelezwa kuwa kutakuwa na matawi ya nje ya nchi. Na imeelezwa bayana kuwa matawi hayo yatafunguliwa kwa indhini ya Katibu Mkuu wa chama. Ndani ya katiba ya CCM vikao vyote vya mashina na matawi ya nje ya nchi vimeelezwa kuwa vinafuata utaratubu upi wa uongozi.
Kwa upande wa CHADEMA, Katiba ya chama sura ya saba 7.2.1 inasema tawi litaundwa katika kila eneo la kijiji, mtaa au Shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa. Hata hivyo kinyume na katiba hii, katika mazingira ya "kimagumashi", viongozi wa CHADEMA wameanza kufungua matawi nje ya nchi! Haieleweki nani anatoa idhini ya matawi hayo kufunguliwa! Haieleweki matawi hayo yanamlolongo gani wa kiuongozi (wanareport kwa nani). Haieleweki nafasi ya viongozi wa matawi hayo katika uongozi wa chama! Kila anayeamua ananyanyuka na kwenda kufungua tawi nchi anayotaka, kwenye marafiki zake, kwa sababu zake!
Mkuu kuna mambo ya msingi zaidi katika katiba ya CCM ambayo hayafuatwi na katiba haijabadilishwa.
mfano:
4.
IMANI YA CCM.
Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:
(1) Binadamu wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
(3) Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
Sidhani kama bado CCM inaamini hayo. (1) na (2) kutokana na matabaka yanayojengwa na chama, ambayo ndiyo yanachangia hata migomo ya madaktari na walimu n.k., na kutokana na jinsi wanavyobagua watu wenye itikadi tofauti za kisiasa.
Hiyo (3) ndiyo kichekesho kabisa.
5. MADHUMUNI YA CCM.
Kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya CCM yatakuwa yafuatayo:-
(3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.
(9) Kuona kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa.
(16) Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na/au upendeleo.
17. SIFA ZA UONGOZI
Pamoja na kutimiza masharti ya Uanachama kama yalivyoelezwa katika Katiba, Kiongozi sharti pia awe na sifa zifuatazo:-
(1) Awe ni mtu
aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.
(2) Awe ni mtu anayependa kueneza matunda ya Uhuru
kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo
ya Taifa kwa jumla.
(3) Awe na sifa nyingine kama zilivyowekwa
katika Kanuni zinazohusika (ZIPI?).
18. MIIKO YA UONGOZI
Ni mwiko kwa kiongozi:-
(1) Kutumia madaraka aliyopewa ama kwa ajili ya manufaa yake binafsi au kwa upendeleo, au kwa namna yoyote
ambayo ni kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo.
(UFISADI)
(2) Kupokea mapato ya kificho, kutoa au kupokea rushwa, kushiriki katika mambo yoyote ya magendo au mambo mengine yaliyo kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo.
(UFISADI)
(3) Miiko mingine ya Viongozi itakuwa kama ilivyowekwa katika Kanuni zinazohusika.
na kadhalika.
Haya ni machache tu ambayo ni contradiction na namna CCM ilivyo na inavyoendeshwa kwa sasa.
Sasa kama chama chako hata imani na madhumuni yaliyomo kwenye katiba yamepitwa na wakati, mambo hayo ya kufungua matawi mbona ni madogo sana. Kama kweli una nia ya kuhakikisha chama kinafanya kila kitu kadiri ya katiba yake, anzia CCM tena kwenye mambo ya msingi zaidi.
TOA BORITI JICHONI KWAKO KWANZA! Ndipo uone kibanzi kwenye jicho la ndugu yako.