Ni kiri tu mimi ni muumini wa utawala wa majimbo. Ni sera hii ndo iliyonivutia hadi nikampigia kura Dr. Slaa katika uchaguzi wa mwaka 2010. Nashangazwa na ukimya wa CHADEMA katika kupigania na kudai utawala majimbo hasa katika kipindi hiki ambapo tuko katika mchakato wa kuandika katiba mpya. Badala yake wamejikita katika mjadala wa serikali mbili/tatu ambao kimsingi ni sera za CCM. CHADEMA kulikoni mnashindwa kudai na kutetea sera yenu iingizwe kwenye katiba?