CHADEMA imekuwa chama cha kutetea mafisadi

CHADEMA imekuwa chama cha kutetea mafisadi

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
8,133
Reaction score
20,370
CHADEMA wanataka kuwaaminisha Watanzania kwamba hakukuwa na mafisadi wala ufisadi kuanzia mwaka 2015 - 2020 maana wanasema kila aliyekamatwa alionewa!. Hata Rugemarila aliyethibitishwa na bunge kwamba aliitia hasara serikali zaidi ya billion 300, Chadema wanasema alionewa tu na Magufuli!!! Hata Acacia mtetezi wao mkubwa ni Chadema.

Kifungu cha 194H cha sheria ya mwendo wa makosa ya jinai kinatoa namna ambavyo plea bargaining itafanyika.

Hata kanuni zilizotolewa na jaji mkuu zipo wazi kabisa. Kuwa mtuhumiwa ataandika barua kwa DPP na baada ya hapo taratibu zitafuata na kama kwa sababu atakuwa amekiri kosa basi mzigo alioupiga utaenda serikalini.

Huyu Zitto anataka sifa za nini? Za kishamba
 
Huu uzi sijauelewa.

IMG-20221017-WA0004.jpg
 
Haitakuja kutokea kiongozi wa mfano wa....
Magufuli.(R.I.P) huyu alikuja kama nabii wa kuirudisha nchi kwenye mstari lakini mafisadi ilikuwa kazi kupambana nao tena kwa jeshi la mtu mmoja.
Huku ukiwa umezungukwa na wanafiki mchana na usiku!

Sababu walikwisha chimbia watu wao hadi kwenye kabati ya nguo ya JPM.
Wengine wakimrembulia macho mchana kisha usiku wanaingia kazini na #kigogo14.....

JPM alimlea na kumlisha chatu na chatu alipokuwa akaishia kummeza yeye mwenyewe!

Ila karma itawahukumu taratibu.
FB_IMG_1662448115677.jpg
FB_IMG_1665690688777.jpg
 
Tusiwachukie matajiri kwa sababu ya umaskini wetu. Hilo ndilo kosa kubwa ambalo Maguri alifanya. Alimuweka Rugemalira miaka 4 rumande na akiwa Mahakamani alishindwa kutoa ushahidi wa Ufisadi wa Rugemallira mpaka akafariki.

Nionyeshe kosa la James Rugemalira nikupe majibu hapa mara moja!! Otherwisw shut up your mouth
 
Wee ni kiazi haswa, eti alithibitishwa na bunge, kwani hapa tuna bunge au genge la wahuni wachumia tumbo walioingia bungeni kwa wizi wa kura
 
Tusiwachukie matajiri kwa sababu ya umaskini wetu. Hilo ndilo kosa kubwa ambalo Maguri alifanya. Alimuweka Rugemalira miaka 4 rumande na akiwa Mahakamani alishindwa kutoa ushahidi wa Ufisadi wa Rugemallira mpaka akafariki.

Nionyeshe kosa la James Rugemalira nikupe majibu hapa mara moja!! Otherwisw shut up your mouth
Hata yule mwizi wa simu mliyemchoma moto angepelekwa mahakamani huenda angeachiwa...lakini haya majizi yanayokwapua mabilioni mnayatetea sana...huyo Rugemalila kama angeachiwa watu naye angechomwa moto tu
 
Haitakuja kutokea kiongozi wa mfano wa....
Magufuli.(R.I.P) huyu alikuja kama nabii wa kuirudisha nchi kwenye mstari lakini mafisadi ilikuwa kazi kupambana nao tena kwa jeshi la mtu mmoja.
Huku ukiwa umezungukwa na wanafiki mchana na usiku!

Sababu walikwisha chimbia watu wao hadi kwenye kabati ya nguo ya JPM.
Wengine wakimrembulia macho mchana kisha usiku wanaingia kazini na #kigogo14.....

JPM alimlea na kumlisha chatu na chatu alipokuwa akaishia kummeza yeye mwenyewe!

Ila karma itawahukumu taratibu.View attachment 2389785View attachment 2389789
Nabii wa Chato na sukuma gang.
 
Hata yule mwizi wa simu mliyemchoma moto angepelekwa mahakamani huenda angeachiwa...lakini haya majizi yanayokwapua mabilioni mnayatetea sana...huyo Rugemalila kama angeachiwa watu naye angechomwa moto tu
Jibu lako lina akisi kiwango cha ufukara wa mali ambao umeathiri hata uwezo wako wa kufikiri. Kama unajuwa kosa la Rugemalira liweke hapa!! Kuchomwa moto hata wewe LUSOMYA usiye na hatia unaweza kuchomwa tu kwa mistaken identity.
 
Yaliyokupata yalistahili,wengi wamepoteza maisha kutokana na madhara ya vyeti fake kama wewe!
Na bada ninaishi na vyeti vyangu feki na mwenye vyeti halali anajibu mashitaka kwa Mwumba wake,hakupenda kuhojiwa ila leo anahojiwa na ataendelea kuhojiwa sana kwa sababu ambaye hakumkubali au kumpenda basi kwake ni Vyeti Fake,too sad.
 
Back
Top Bottom