CHADEMA Imekaaje?

MAFILILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,377
Reaction score
1,200
Nawaomba wadau wa CHADEMA watupe majibu kwa nini hawana diwani hata mmoja katika majimbo yafuatayo:-

Mtwara Mjini, Masasi, Newala, Mtwara Vijijini, Tandahimba, Nanyumbu, Lulindi, Lindi Mjini, Mtama, Liwale, Nachingwea, Kilwa Kaskazini, Kilwa Kusini, Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini, Mafia, Rufiji, Kibiti, Mkuranga, Kisarawe, Majimbo ya Pemba na Unguja, Tanga Mjini, Muheza, Pangani, Mkinga, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Bumbuli, Temeke, Ilala,Kigamboni, Kinondoni. Tunduru Kaskazini, Tunduru Kusini, Namtumbo, Mbinga Mashariki, Mbinga Magharibi, Peramiho

Wanazi wa CHADEMA leteni majibu
 
Pia Kondoa Kaskazini na Kusini hakuna diwani wa CDM kwa Lusinde nako CDM hawana uongozi wala hawajawahi kutia mguu
 

Hizi habari za Chadema, chadema, chadema vs CCM mpaka zinachosa sasa na kukera, kwani ulitaka CDM wawe na madiwani nchi nzima? inakuwa sasa kama chadema na ccm wanagombania mke au wamechukuliana waume? Khaa! kwanini usuwaulize hao madiwani waliopo whichever party they belong wamewaletea maendeleo gani katika hizo kata waliowachagua? we mtu saa tano za usiku bado unaiwaza chadema badala ya kulala ukafaidi usingizi wako, sasa wakishakujibu kwa nini hawana madiwani then what? inaudhiii.
 

Ni kwa sababu kura hazikutosha. Sehemu zilikotosha wana madiwani w/viti wa vitongoji na vijiji pamoja na wabunge. Asante kwa kuwakumbusha maeneo hayo yanahitaji M4C na CDM ni wasikivu watalifanyia kazi.
 
Kwasababu Chadema hakikuwa na mtandao mkubwa katika majimbo hayo, lakini kwasasa watasimamisha wagombea hata kama hawatashinda yote coz chama kimekuwa na umarufu.
 
Ni jambo linaloeleweka kwamba chadema ni chama cha siasa kinachokua, ccm walibahatika, maana wao hawakuwahi kufanya kampeni za kisiasa kujiuza kwa wananchi bali watu walilazimishwa tu kwamba nchi hii iko chini ya chama kimoja na kila mmoja ni sehemu ya chama, ile party supremacy bado haijawatoka baadhi ya watu na baadhi ya maeneo, lakini taratibu wataelewa, tanga wameanza kuelewa naamini mtwara itakuwa zaidi, so usihofu, demokrasia ni mchakato hatimae nchi nzima itafikiwa
 
Weka kiporo hilo swali hadi 2016 baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.
 
Hivi unalipwa kwa kila makala unayoanzisha juu ya Chadema? Umeanzisha Limevunda, bado siku haijaisha umekuja na hii.
 

Wewe ondoa longo longo zako. Unachokisema wala hukifahamu.

Kama bandiko hukulipenda, kwa nini unapoteza muda kusoma lote na ku-reply.

Usifiche ukweli wa jambo kwa mgongo wa marumbano ya kiitikadi.

Kwa akili zako unafikiri kila anatembelea au kupost JF basi yuko Tanzania.

Usitake kuleta dictatorial mentality hapa JF ili watu wafanye kile unachokitaka/kukipenda.

Kama huwezi kujibu na kuchangia hoja, una choice mbili, ignore or skip
 

imegusa penyewe?
 
Hivi huko kuna wakristo kweli?
 
Pia Kondoa Kaskazini na Kusini hakuna diwani wa CDM kwa Lusinde nako CDM hawana uongozi wala hawajawahi kutia mguu

Mbona mleta mada anaogopa kutaja maeneo yote, hata kwa MWIGULLU hawana chao.
 
Bora umeliona hilo mkuu, mimi kuna wabunge wa CDM nawafahamu ebwane, mtu alikuwa mama wa ndani lakini kwa vile anajuana na kiongozi wa CDM wilaya akaukwaa, hivi sasa kuna mvutano ndani ya hiyo familia baba kalalamika hadi kachoka.
 
labda tukuulize wewe muumini wa siasa za jussa ladhu

kauliza, mwenyeji wa huko atuambie manake maeneo yote yaliyotajwa inaonekana kama hakuna watu wa imani ile ambayo chama kimeanzishwa kupitia kwayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…