Naizungumzia NCCR ile iliyokuja kuibuka baada ya sakata la Mrema na Chavda! Naizungumzia NCCR iliyokuwa imemtunuku Mrema uenyekiti wa chama hicho mara baada ya kuihama CCM kwa mbwembwe(haijapata kutokea)! Naizungumzia NCCR ile ambayo Katibu Mkuu wake alikuwa Mabere Marando yule na sio huyu! Naizungumzia NCCR iliyokuwa na ma-striker hatari kama Dr. Masumbuko Lamwai ambae aliwasumbua CCM kuanzia Ubungo na kuja kuwachinjia Temeke! Naizungumzia NCCR iliyomsimamisha Mrema kama mgombea urais 1995 na kumtoa makamasi Mkapa licha kupita kupigiwa kampeni na Baba wa Taifa nchi nzima! NCCR ambayo (kama sikosei) ilipata takribani 27% ya kura za urais(Haijawahi kutokea tena)! Naizungumzia NCCR iliyokuwa kabla Mrema hajavumbua staili ya kukimbilia uvunguni mwa meza kukimbia kichapo!
Je, CHADEMA hii iliyonawiri maradufu baada ya kumtangaza Dr. Slaa kuwa mgombea urais imefikia hadhi ya NCCR ile niliyoizungumzia hapo juu?! Je, atavunja rekodi ya 27% (Binafsi sitaki politics, nazungumzia facts kwamba Urais hatapata) aliyokuwa ameipata Mheshimiwa Mrema?! Je, CHADEMA ina chochote cha kujifunza toka kwenye NCCR ile ambayo gari ya mgombea wake wa urais ilikuwa inasukumwa na mashabiki kila anapopita? Je, Marando ataishia kuwa mpiga debe tu kwenye chama chake kipya au atatumia uzoefu wake wa makosa ambayo waliyafanya ndani ya NCCR DUME?!