CHADEMA ilimaliza 2014 sasa ni zamu ya CCM

CHADEMA ilimaliza 2014 sasa ni zamu ya CCM

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224
Habari wadau.
Binafsi naushukuru sana mwaka 2014, Ni mwaka ambao uliamua hatma ya Upinzani na Chadema kwa ujumla.

Ni mwaka wa misukosuko ndani ya Chadema, Bila mwaka 2014 hakika tusingekuwa na chadema imara wala UKAWA. Kupitia misukosuko hiyo Uongozi wa chadema ulitumia fursa hiyo muhimu kujenga chama imara zaidi.

Mwaka 2015 chadema ipo imara zaidi kujiandaa na kazi za kisiasa. Wakati Chadema ikifurahia mazingira bora zaidi CCM ina kazi ngumu zaidi kubwa ni ile ya Makundi ya Uraisi, Kupoteza mvuto na tuhuma lukuki za ufisadi huku kukiwa na ushahidi usio shaka kabisa kuwa viongozi wake wakuu wamekwama.

CCM imeshindwa kusuluhisha makundi ya kisiasa kwa Miaka 10. CCM imekumbatia ufisadi kwa kiwango cha kutisha. Na sasa inaingia 2015 huku ikiwa haina hata tone la historia nzuri.

UKAWA INAPASWA KUTUMIA FURSA HII KUTUONGOZA WANANCHI KULETA MABADILIKO.
 
mkuu umenena vema sana sasa ni zamu ya kawa kutwaa dola
 
......ccm ni chama dhalimu ambacho kinaelekea ukingoni.Iko wapi KANU na mabavu same?
 
Usitegemee jipya lolote hapo kwa cc ya magamba! tumsubiri Mzee Tupatupa!
 
Wazee wa viporo ni shida. Jana nimesikia mh. Pinda anaahidi kukarabati meli za ziwa Nyasa mpaka meli za nchi Jirani!!
 
Umeeleza vema sana kamanda.Hata hivyo napenda nikufahamishe bila kumung'unya maneno kuwa CCM ni chama dhaifu kuliko chama chochote cha siasa hapa TZ. CCM ni chama kama chungu cha kupikia kilichoshikiliwa na mafiga haya 1).vyombo vya dola 2).serikali na matawi yake 3).Mafisadi au wafanya biashara haramu na wananchi wachache wasiojitambua.
Haya mafiga yote yakiondolewa CCM chini.
 
Leo Nipo Mwanza watu niwengi sana kweli palipokuwepo na Mungu shetani hasogelei. Nanuku kutoka kwa Mtumishi moja.. Chadema kimepata kibali chakuongoza nchi kwanzia october 2015. Mwishi wanuku
 
Umeeleza vema sana kamanda.Hata hivyo napenda nikufahamishe bila kumung'unya maneno kuwa CCM ni chama dhaifu kuliko chama chochote cha siasa hapa TZ. CCM ni chama kama chungu cha kupikia kilichoshikiliwa na mafiga haya 1).vyombo vya dola 2).serikali na matawi yake 3).Mafisadi au wafanya biashara haramu na wananchi wachache wasiojitambua.
Haya mafiga yote yakiondolewa CCM chini.

Ukweli mchungu kwa CCM sharti upakwe sukari ili usiumize mpokeaji, sasa wewe unapiga za uso halafu unavizia sio vizuri bwana!
 
Ukweli mchungu kwa CCM sharti upakwe sukari ili usiumize mpokeaji, sasa wewe unapiga za uso halafu unavizia sio vizuri bwana!

Mkuu labda nikuhakikishie jambo jingine ambalo sina shaka nalo ni kwamba hata hivyo vyombo vya dola vimewachoka sana ila tu sema katiba iliopo inawafanya waitii serikali iliyopo madarakani kwa wakati huo, pia kwa idadi ya watendaji wavyombo hivi wanaipenda CCM kutoka mioyoni mwao ni sawa na hakuna ila wanaoigiza kuwa wanaipenda ni wachache sana na hii ni kwa sababu ya kupiga milungula,na uzandiki mwingine.Wanaoichikia ni wengi sana hawa ni zaidi ya 90% wasiojitambua ndani ya vyombo hivi ni wachache pia.Na hii ni hata kwa watendaji wa serilali.
MAFISADI.hawa wala hawaipendi kabisa CCM.Hawa ni kama MALAYA tu wanaipendea CCM hela yake yaani (RASILIMALI ZETU).
WASIOJITAMBUA.hawa wala hawana tabu.Ni elimu ya uraia tu na wakati.
UHAKIKA WANGU.ni elimu ya uraia inayotolewa na CHADEMA na WANA-UKAWA, na nguvu ya UMA ni tiba tosha kwa mafiga matatu niliyoyataja hapo juu.Kwani elimu ya uraia sasa imepenya hadi majeshini na usalamani kote, imeingia shule za chekechea, kata,vyuo,misikitini,mahekaluni,makanisani,magengeni,vilabuni,safarini,misibani,harusini,kwenye nyumba za wageni, kwenye ma bar,ngomani,madansini, madiskoni,bichi,ikulu,mawizarani,kwenye jumuiya,kwenye mihadhara na madrasa na kila sehemu ambapo kuna zaidi ya mtu mmoja
 
Back
Top Bottom