- Mshikamano ndani ya chama ni muhimu, Migogoro mwiko. Matatizo yamalizwe ndani ya chama na pale mtu yeyote anakwenda kinyume na malengo na katiba ya chama muondoeni bila kujali hadhi yake. Hakuna aliye juu ya chama
- Elimu zaidi ya uraia kwa wananchi hasa wale wa pembezoni
- Ni vizuri mkawa na mtandao wa mawasiliano mfano redio au TV ili kuwafikia watu wengi zaidi kwa muda mfupi.
- Kuweni makini na propaganda za udini, ukabila na ukanda zinazoenezwa na maadui wa demokrasia Tz.
- Lazima muwe na watu makini katika mambo makini, wenye uwezo wa kufikiri kwa marefu na mapana kwa uhakika. Vilaza wa kutoa majibu mepesi kwa mambo muhimu
- Vita dhidi ya rushwa na ufisadi lazima iwe endelevu katika kufichua bila woga
- Mambo yanayohusu maslahi ya umma lazima yawe ndiyo kipaumbele kwenu
- Lazima mtambue kuwa muda uliobaki kufikia 2015 ni mfupi sana hivyo ni lazima mujipange vizuri ikiwa ni pamoja na kupata usimamizi wa dhati na uwakilishi majimbo yote TZ. Hii ni pamoja na kuwa na mawakala wa kuaminika
- Mtambue JINAMIZI la CCM ni kama nyani mzee asiyeishiwa na mbinu. Hivyo watatumia mbinu mbali mbali kuwavurugeni ikiwa ni pamoja na kuwaletea mamluki kama mzee wetu .........Maswa
- wadau mnaweza kuendelea.........................................

4 real nmeipenda comment yako, kazi kwa viongozi wa CHADEMA kwa hili kulifanyia kazi
First
nimekuwa nikijiuliza sana kwa kuwa chadema imeshindwa kufungua matawi kila kata basi hiki chama kingeanzisha utaratibu wa kuwa na makamanda wawili wa kila mtaa na wawe wanatambulika na chama kitaifa,mkoa,wilaya na kijiji na uanzishwe utaratibu wa viongozi kwenda kuwasimika makamanda hawa katika kila kona ya nchi na kazi yao kubwa iwe kupeleka elimu ya uraia kwa mtaa anaoishi na hawa wawe wanapewa majukumu yote kwa mtaa husika zikiwemo kadi na vitu vingine hii itasaidia kupunguza wimbi la ccm kurubuni viongozi wa chadema na kuwanunua sababu kutakuwa na mtandao mkubwa wa viongozi wa chadema na hapa itakuwa rahisi kupata viongozi wa kata/wilaya/mkoa au kijiji na pia uwekwe utaratibu wa makamanda hawa wawekwe kwenye website pamoja na information zao, kufanya watu wa makao makuu kuwasiliana nao moja kwa moja either kwa kutumia email au simu pia watumike kuchukua matatizo ya mtaa husika kuwasilisha kwenye ofisi ya kata/kijiji/wilaya/mkoa
second
kwa kufanya hivyo chama kitajenga mtandao ulionea nchi nzima bila kutumia gharama kubwa na litengwe fungu maalumu ambalo sio kubwa sana litumike kuwawezesha hawa makamanda liwe tofauti na lile la wilaya au mkoa hapa hakuna haja ya kufungua matawi bendera tu inatosha nikiweka kwenye chumba au nyumba, kwamba killa habari inayohusu chama kwenye ule mtaa itapatikana kwa makamanda hawa operation zao ziwe tofauti na zile za wilaya na mkoa na kazi ya kuwasimika hawa ifanywe na bavicha makao makuu wapite kila mkoa,wilaya,kata na kijiji ili kuwe na mtandao mkubwa nchini utakaowachanganya sana ccm washindwe kujua yupi wa kumnunua..hapa tupunguze kidogo habari za maandamano tutumie mwaka mmoja kujenga hiki chama na hapa ndo tutaona watu wanaokitumikia chama na wale vibaraka
peoplesssssss powerrrrrrrrrr
Mkuu Nakubaliana na wewe asilimia 90 lakini kwenye sanduku la kura mbona tunashinda sana lakini tunaibiwa sana . Toa ufafanuzi jinsi ya kulinda kura acha longolongo