Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Makene asambaza screenshot ya massage Mnyika kama kielelezo cha kukanusha TAARIFA inayosambaa kwa kasi inayo daiwa imetolewa na Mnyika. Leo gazeti.la Raia Tanzania limeibuka na habari hiyo katika ukurasa wa mbele ikisema "Mnyika ataka Lowassa ashitakiwe"
Kubwa zaidi, vijana wa UKAWA hususani wa CHADEMA tangu jana usiku wanakesha kukanusha hili, na leo hii baada ya Raia Tanzania kutoka na habari hiyo, wamehamishia majeshi ya kwa gazeti hilo wakitaka tulipuuze.
Nilipoona taarifa hizi za Mnyika dhidi ya Lowassa na leo hii kuziona katika ukurasa wa mbele wa gazeti Raia Tanzania, zimenifanya niingie katika Tafakuri nzito. Tafakuri yangu zaidi ilijikita kwa kuwatazama aina ya vijana ambayo CHADEMA inawatengeneza na kubwa zaidi nini taarifa ile iliyodaiwa ya Mnyika iliashiria.
AINA YA VIJANA WA CHADEMA.
Vijana hawa wamekuwa ni vijana wa kula kila kitu bila kutafuna kinachotoka kwa viongozi wao wenye mahaba nao, hata kama hicho kitu ni sumu na hatari kwa maisha yao, wao wanakula tu midhali kasema Mbowe au sahiba wa Mbowe. Hii ina maanisha nini?
Ina maanisha kwamba BAVICHA inathubutu kuinyoshea kidole serikali na chama tawala lakini haliwezi kuwaoneshea kidole vigogo wa CHADEMA. leo hii CHADEMA ikiunda serikali, na kwa kizingatia kasumba ya BAVICHA, haitaweza hata kidogo kuinyoshea kidole serikali inayoundwa NA CHADEMA.
VIJANA WA CHADEMA, zilipotoka habari kwa mara ya kwanza kabisa kuwa Slaa kajiuzulu na ya kwamba sasa haendi tena ofisini pale Ufipa, vijana hawa walipinga na kukanusha, walifanya hivyo sababu Mbowe alipinga na kukanusha taarifa hizo.
Vujana hawa walilishambulia Jenerali Ulimwengu katika mitandao kisa tu magazeti yake ndio yalio ripoti taarifa hizi. Hata hivyo waliona aibu baada Dk Slaa kutoka hadharani na kutangaza kujiuzulu kwake.
VIJANA WA CHADEMA, zilipo sambaa picha.za Lowassa kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya CHADEMA na picha hizo pia kuwekwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Raia Tanzania, hawa vijana hawakuwa nyuma kukanusha. Walikanusha kuwa Lowassa hakuhudhuria kikao kile. Walikanusha si kwamba walikuwa na sababu za kukanusha, walikanusha baada ya kumuona Mbowe amekanusha.
Baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA, na baada ya Dkt Slaa kuongea na wanahabari wakati wa kujiuzulu kwake, ukathibitika ni kweli kuwa Lowassa alihudhuria kikao cha kamati kuu ya CHADEMA. hawa vijana wetu wakaonekana tena warongo na wasio na msimamo, na magazeti ya Jenerali kuoneka yalikuwa na ukweli wa mambo.
VIJANA WA CHADEMA, ziliposambaa fununu za Lipumba kujiuzulua, vijana wa CHADEMA kwa kuungana na wenzao wa CUF chini ya UKAWA walikanusha, walikanusha baada ya kumuona Maalim Seif amekanusha. Hata hivyo, baadae ikatibitika ni kweli baada ya Lipumba kuongea na wana habari.
Kwa mara nyingine hawa vijana wakawa wakaonekana warongo, wakaonekana ni watu wa kutetea maneno ya viongozi wao hata kama hayo maneno ni pumba.
KWANINI NASEMA YOTE HAYA?
Makene na akina Malisa wanataka kuturudisha enzi za ujima, enzi za mgeni anatangulia kufika kabla ya barua aliyo iandika. Wanataka tuamini screwnshot ya massage ya Mnyika na tuache kuamini taarifa inayo daiwa ya Mnyika na habari iliyo andikwa leo na Raia Tanzania.
Mnyika ana acc ya facebook, na ana page, kubwa Mnyika ni mwepesi sana kutoa taarifa ya kumuhusu kupitia acc yake ya facebook, kwanini aishie tu kumtumia massage Makene na asikanushe kupitia ukurasa wake wa facebook?
Kwanini nasema yote haya? Nasema haya kuwakumbusha GENGE LA BAVICHA LA MTANDAONI kuwa ni mara nyingi watanzania na wanachama wa kawaida wa CHADEMA wamekuwa wakiwaamini na kulipuuza gazeti la Raia tanzania, lakini mwishowe gazeti huonekana limesema kweli, lakini Mbowe na genge la BAVICHA lilopo mtandaoni wanakuwa wamesema urongo. Tunasababu gani ya kuwaamini sasa ikiwa mwanzo tulifanya hivyo na ikawa mmetudanganya?
Hivi tutamini vipi kuwa screen shot inayosambazwa si mkakati wa urongo wa kumlisha maneno Mnyika kama ilivyo kuwa kwa Dkt Slaa na Lipumba?
TAARIFA ILE ILIASHIRIA NINI?
Niwaambie tu ile taarifa haikuzuka na kusambaa kwa bahati mbaya, kwavyovyote vile huenda kulikuwa na mradi maalum wa kuisambaza, na kama kweli ni mradi, hakika mwenye mradi wake amefanikiwa sana.
Ukizingatia ujio wa Lowassa CHADEMA kuliko fuatia na ukimya wa Mnyika, na kubwa zaidi msimamo wa Mnyika juu uchafu wa Lowassa, na kubwa zaidi kutoonekana ukaribu wa Mnyika na Mzee Lowassa, kwa vyovyote vile kuna uwezekano mkubwa ile taarifa ni mradi wa Mnyika mwenyewe.
Huenda Mnyika ameamua kutumia watu ili kuondoa dukuduku lake japo kwa kutumia mbinu ya kujilisha maneno na kisha atoke hadharani akanushe. Jina Magufuli kalichomeka Mnyika katika taarifa yake kwa kusudi maalum. Ile taarifa ingeishia kumshambulia Lowassa tu na kuelezea sababu za ukimya wa Mnyika, ama hakika viongozi wa CHADEMA wasingemuamini Mnyika pamoja na kukanusha kwake.
AU
Huenda ukawa mradi CCM wenye lengo la kumtoa Mnyika pangoni huku akiwa kahamaki kama mbogo aliyechubuliwa na risasi. Wanachotaka waone ukauzu wa Mnyika kutoka hadharani mbele ya media, akanushe taarifa ile iliyosambazwa na kisha azungumzie usafi au uchafu wa Lowassa.
Huu ni mtego kwa Mnyika, hapa Mnyika anapimwa kama ataweza au ana ubavu wa kusema kuwa Lowassa alikuwa chaguo sahihi la UKAWA na kubwa zaidi Lowassa ni mtu safi na ule ushahidi alokuwa nao juu ya ufisadi wa Lowassa si ushahidi bali ulikuwa ni mpango wa kumuangusha kisiasa Lowassa.
Tangu Lowassa aingie CHADEMA, na tangu Slaa ajiuzulu, Mnyika amebadilika, pamoja na kwamba inasemekana kuna kipindi alikuwa anaumwa, lakini ukimya wa Mnyika ni zaidi ya kuumwa. Mnyika CHADEMA imemtumbukia nyongo baada kumpokea Lowassa, hili litapingwa lakini Mnyika enzi za Slaa sio Mnyika wa sasa.
Dotto Rangimoto Chamchua.
call/whatspp 0622845394 Morogoro