CHADEMA iko mitandaoni na kidogo mijini na si vijijini

CHADEMA iko mitandaoni na kidogo mijini na si vijijini

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,471
Reaction score
1,578
Habari Wakuu

Nimefanya utafiti wangu kidogo tu katika vijiji vya Bariadi.

Hapa juzi kati nilitoka zangu Moshi na gari la Mgamba mpaka Shy mjini.Nimefika pale nikaenda Motel moja hapo iko Karibu na stand ya zamani ya shinyanga nikisubiri kesho yake niingie Bariadi kwa mzee Cheyo na Chenge.Nilijaribu kudodosa dodosa vijana wa pale shy mjini,kiukweli kwa maoni ya pale Magufuli aliongoza,sikuwa na nia ya kufuatilia kete ya ubunge maana hiyo wagombea hawakujulikana bado.

Kesho yake bana nikachukua Mombasa nikaelekea Bariadi,Maongezi ya kisiasa kwenye gari yalikua yanaongelea sana Lowasa kukatwa,UKAWA kutotangaza mgombea na Magufuli kuwa Rais! Kiukweli nilikua mdadisi kidogo lakini mwisho wa siku nilikuja kugundua Magufuli anaaminiwa sana akiwa Rais.Nimefika Bariadi nikafikia Soko mjinga Somanda,na route yangu ilianzia kule....

Nilitoka Somanda nikaenda vijiji vya Kilulu,Budalabujiga,Giriku,Lagangabilili,Mitobo,Ikindilo,Nguno,Ng'hesha,Ntobo Madilana,Mhunze,Migato Shishani na Longalombogo,Nilipitia Ndoleleji,Nangale Nanga,Senani,Laini hadi Mwamtani....

Nilitoka.kule nikarudi tena mjini hii ni baada ya wiki moja,Nilitoka Bariadi mjini nikaenda maeneo ya mji mdogo Luguru,nikaenda Inalo,Zanzui,Mahembe Sawida,Mwakilangi hadi Kabale....off coz ni vijiji vingi nilipita vingine hata sikuziandika,kule kote nimepita,kwa maoni ya watu waliokua wanongoza ni

1.Magufuli

2.Slaa

3.Lipumba.

Safari yangu ilienda mpaka sehemu moja inaitwa Mahaha na nikaishia jiji la Mwanza kesho yake nikaoandokabna Isamilo back to Arusha.

Nimefika Arusha sikutegemea maoni ya watu walivyokua wanaongea....ni Lowasa lakini plan B ndo Magufuli,japo watu wengi walikili MAgufuli watampigia kura ila ubunge obvious ni Chadema,nimetoka jana Arusha na sasa niko Moshi,jana nilikaa pale Moshi stand ninapga stori na watu wa pale karibu na sehemu ya kutokea Magari,kiukweli wengi wao walikiri watampgia kura Magufuli.

Leo niko huku Kibosho Umbwe,kwenye mashamba ya kahawa huku,Lowasa wanakiri kumpenda sana ila pia kuna.baadhi wanasema watampa kura Magufuli wengine wamekana kabisa ni ndoto ya mchana kumpgia kura Magufuli...

Lakini kwa mizunguko yangu mingi nakili kusema Chadema bado hawajajijenga vijijini wapo sana mjini.....yangu ni hayo tu,nakaribisha wenye mawazo nao waliojaribu kutembea tembea siku chache zilizopita.
 
Huwa nafurahi na kufarijika ninavyotembea mikoani na kukuta bendera za chadema vijijini,mfano iringa,mbeya,arusha,kilimanjaro,manyara,singida,simiyu,shinyanga,kahama,nk,,,sijui wewe hutembei.?..!..
 
Hahahaaaaaa ccm sijui huwa mnatumia akili za aina gani mnapoposti vitu. Sijui kwa kweli. Either mna uelewa mdogo au mmeshiba dharau na kiburi cha madaraka
 
aliyekudanganya amefaidi kweli ! maana ni raha sana kumdanganya mbumbumbu .
 
Ni kweli endelea kulala.....
UCHUZI SERIKALI ZA MITAA UKUFUMBUE MACHO WW ULIYELALA FOFOFO WKT WATZ WAMEAMKA
 
Ukweli nikuwa vijana wengi hum hawataki kuelezwa ukweli, wao wameshikiria ushabiki na kwakuwa viongozi wao wamejenga hali ya umungufulan ambao hawakosolewi wala kushauriwa hata wao nihivyo hivyo, hawataki mtu hum kupost jambo tofauti na matakwa yao walivyo vichwa vya chawa wanataka wote wawe kama wao. Watu wabadirike si muda wa kupenda vizuritu uwetayari na vibaya pia
 
Mkuu umenena,
 
Huyu mwandishi alikuwa anapambanisha mgombea wa CCM na wengine ambao hawajajulikana bado. Ni lazima uelewe kuwa ili uwe katika uwiano mzuri wa kitakwimu lazima ulinganishe vitu/watu wenye sifa zinazofanana. Sijui wewe ulikuwa unafanya utafiti wa namna gani. Subiri UKAWA wakitangaza mgombea wako uanze upya safari yako then uje na majibu.
 
Ukweli nikuwa vijana wengi hum hawataki kuelezwa ukweli, wao wameshikiria ushabiki na kwakuwa viongozi wao wamejenga hali ya umungufulan ambao hawakosolewi wala kushauriwa hata wao nihivyo hivyo, hawataki mtu hum kupost jambo tofauti na matakwa yao walivyo vichwa vya chawa wanataka wote wawe kama wao. Watu wabadirike si muda wa kupenda vizuritu uwetayari na vibaya pia
Rudi darasani, elimu ni muhimu sana.
 
CCM kuweni makini sana mlianza na CDM haipo! Itakufa, ipo kaskazini tu, sasa mtabaki na ipo Vijijini mkishambuliwa huko vijijini sijui mtasema nini?
 
Back
Top Bottom