Chadema ikishindwa wananchi tunaweza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema ikishindwa wananchi tunaweza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitalolo, Apr 4, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kwainavyooneka wananchi wengi wamekuwa na matumaini na CDM. na wengi wetu tunaitegeme kwa kutukomboa Taifa hapo mwaka 2015 kwa kuwakabidhi madaraka.
  swali ninalojiuliza Je Chedema Mko tayari? na je CCm watakubali kukabidhi madaraka kwa chama mmbadala kitakachopewa dhamana na wananchi? kwasasa chama kinachoonyesha mwelekeo wa kukabidhiwa dhamana ya M4C ni CDM.

  Je ikiwa CCM ikikataa kukabidhi madaraka kama tunavyoshuudia kwenye nchi nyingi za kiafrika viongozi kungangania madaraka mpaka nguvu ya umma itumike. Je wangapi tutakuwa tayari kuiwajibisha CCM kwa kutumia nguvu ya umma na kauli mbiu ya CAHDEMA ya peoples power?
  Ukiangalia kwasasa utagundua kuwa kuna baadhi ya wananchi wa baadhi ya mikoa wanauthubutu hata wa kufungu bendera ya chama cha upinzani bila woga lakini kwa baadhi yetu hata sasa kujitambulisha tu kuwa ni wapinzani wanaogopa je wanannchi tunaweza bila kuiachia Chadema majuku yote ya kulikomboa taifa?

  Na je Jiografia ya nchi yetu inaruhusu mageuzi kwa nguvu ya umma haswa ikizingatiwa ukubwa wa nchi na ile hali ya kujipanda kwaajili ya kuunganisha nguvu ya umma katika kuipinga serekali nganganizi ya ccm.

  Na je ni wangapi wako tayari kuikabidhi dhamana CCM kwa kipindi kingine cha miaka mitano au kumi ijayo kuanzia 2015?

  Na je CCM wanaweza kubadilika ikiwa tutawakabidhi dhamana ya kuliongoza taifa hili tena?

  NINI KIFANYIKE NA KIANZE VIPI NAFIKIRI INAHITAJI KUJIPANGA. NA IKIWA CCM IKIJUA WATU WEMEJIPANGA
  HAITATHUBUTU NA HAITAWEZA NA HAITAONGOZA TENA NCHI WATAONDOKA ASUBUHI NA MAPEMA KAMA WALIVYOFANYA KWA ARUMERU MASHARIKI.

  Nimeona nguvu nyingi iliyotumika kulinda kura Arumeru mashariki ndiyo inayonisukuma kuandika.
  ikiwa nguvu hiyo ilitumika kwa jimbo moja je nguvu hiyo inaweza kutumika kwa taifa kwenye Uchaguzi mkuu wa 2015?
  wananchi watakuwa tayari kulinda kura au inabidi kufanyike kampeni ya kuhamasisha wananchi kulinda kura sambamba na kampeni ya kuwanadi wagombea?

  Kuna mengi yanaisumbua akili yangu wakati nikitamani mageuzi ya haraka na ya kweli katika taifa langu.
   
Loading...