CHADEMA, huyu aweza kuwasaidia kesi ya Igunga!

CHADEMA, huyu aweza kuwasaidia kesi ya Igunga!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Igunga kuna kesi.Ni kesi ya ugaidi dhidi ya Makamanda mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Kileo wa Dar. Makamanda hawa wanatuhumiwa kumteka na kumwagia tindikali Tesha-wa-Igunga. Uhalifu aliofanyiwaTesha-wa-Igunga si wa kuushabikia. Ni ukatili dhidi ya ubinaadamu.Naulaani.

Lakini, udhalimu ule aliofanyiwa usifanywe mtaji wakisiasa na kupaka matope chama fulani. Sheria zipo;vyombo vya kisheria vipo.Viachwe vifanye kazi. Hakuna haja ya viongozi wa kichama kuwa walalamikaji,washtaki,na mashahidi. Hakuna haja ya kumfanya Tesha-wa-Igunga kama lulu kwa CCM na kumtumia kuombea kura. Kufanya hivi, ni kufilisika kisiasa.

CHADEMA,wakati wenu ni huu. Jilindeni dhidi na mnayoyadai kuwa ni 'mafilamu' ya chama tawala. Pamoja na kuwa na Mawakili wasomi wenye weledi,bado mnahitaji mashahidi. Mashahidi wanapatikana Igunga.Mmojawao ni kijana (aliyewahi kuwekwa Youtube yake humu) ambaye alihama toka CCM kwenda CHADEMA. Kijana huyu alisema jambo juu ya Tesha-wa-Igunga.

Alisema kuwa Tesha-wa-Igunga amemwagiwa tindikali nawana-CCM wenzake ambao aliwadhulumu pesa zao za posho ya kampeni. Kijana huyu atafutwe,alindwe na atumike kama shahidi. Kwa wafuatiliaji wa Igunga watakubaliana nami kuwa wakati wa kampeni filamu ilianza kutengenezwa. Ikadaiwa kuwa CHADEMA walivamia nyumba fulani na kuiteketeza kwa moto. Cha kushangaza,viliungua vitu vyote pamoja na nyumba husika lakini kuna kitu kikabaki.

Ni kitu kilichotarajiwa kuungua mapema kuliko vingine.Karatasi. Eti, ilibaki karatasi (kipeperushi) kilichodai kuandikwa kwa tambo na CHADEMA kuwa wao ndio waliochoma nyumba hiyo. Ngumu kuamini.

Kamanda Kileo na wenzake wanaimani na kuisubiri CHADEMA.Wamejawa matumaini ya kuoshwa dhidi ya kesi yao na kurudi ulingoni kupambana kisiasa. Kamanda Kileo na wenzake wanatamani kupata ushindi wa ki-Lwakatare. Amini nawaambieni, ipo siku Tanzania itakuwa na siasa safi na za ushindani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
Haya yoote yataisha tu..... Viko wapi visu vya IGP Mahita?
 
Wahusika Cdm plz fanyieni kazi ushauri huu mzuri. TUNAWAAMINI
Igunga
kuna kesi.Ni kesi ya ugaidi dhidi ya Makamanda mbalimbali wa CHADEMA
wakiongozwa na Kileo wa Dar. Makamanda hawa wanatuhumiwa kumteka na
kumwagia tindikali Tesha-wa-Igunga. Uhalifu aliofanyiwaTesha-wa-Igunga
si wa kuushabikia. Ni ukatili dhidi ya
ubinaadamu.Naulaani.

Lakini, udhalimu ule aliofanyiwa usifanywe
mtaji wakisiasa na kupaka matope chama fulani. Sheria zipo;vyombo vya
kisheria vipo.Viachwe vifanye kazi. Hakuna haja ya viongozi wa kichama
kuwa walalamikaji,washtaki,na mashahidi. Hakuna haja ya kumfanya
Tesha-wa-Igunga kama lulu kwa CCM na kumtumia kuombea kura. Kufanya
hivi, ni kufilisika kisiasa.

CHADEMA,wakati wenu ni huu. Jilindeni dhidi
na mnayoyadai kuwa ni 'mafilamu' ya chama tawala. Pamoja na kuwa na
Mawakili wasomi wenye weledi,bado mnahitaji mashahidi. Mashahidi
wanapatikana Igunga.Mmojawao ni kijana (aliyewahi kuwekwa Youtube yake
humu) ambaye alihama toka CCM kwenda CHADEMA. Kijana huyu alisema jambo
juu ya Tesha-wa-Igunga.

Alisema kuwa Tesha-wa-Igunga amemwagiwa
tindikali nawana-CCM wenzake ambao aliwadhulumu pesa zao za posho ya
kampeni. Kijana huyu atafutwe,alindwe na atumike kama shahidi. Kwa
wafuatiliaji wa Igunga watakubaliana nami kuwa wakati wa kampeni filamu
ilianza kutengenezwa. Ikadaiwa kuwa CHADEMA walivamia nyumba fulani na
kuiteketeza kwa moto. Cha kushangaza,viliungua vitu vyote pamoja na
nyumba husika lakini kuna kitu kikabaki.

Ni kitu kilichotarajiwa kuungua mapema
kuliko vingine.Karatasi. Eti, ilibaki karatasi (kipeperushi) kilichodai
kuandikwa kwa tambo na CHADEMA kuwa wao ndio waliochoma nyumba hiyo.
Ngumu kuamini.

Kamanda Kileo na wenzake wanaimani na
kuisubiri CHADEMA.Wamejawa matumaini ya kuoshwa dhidi ya kesi yao na
kurudi ulingoni kupambana kisiasa. Kamanda Kileo na wenzake wanatamani
kupata ushindi wa ki-Lwakatare. Amini nawaambieni, ipo siku Tanzania
itakuwa na siasa safi na za ushindani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es
Salaam.
 
Musa Tesha + Maccm = Mtaji wa kisiasa.
 
Wazo zuri,lakini wawahi kumuwekea ulinzi kabla hajauawa kwani chemba hachelewi.
 
Mahakama inaenda kwa ushahidi!
Na mbele ya Tundu Lissu, na Prof., Kibatala na wengineo sioni kesi hapa!
Namhurumia Tesha kama mtanzania mwenzangu ILA namlaani kama anajua waliomfanyia hivyo kwamba si wale anaolazimika kuwatuhumu!
Mungu atamlipa Tesha kama anashiriki dhuluma!
Yetu macho.
 
It's very true huyu mtu ni muhimu sana, naamini Prof Safari atapita hapa aone uwezekano. Pamoja na kwamba CCM wanajulikana kwa kutengeneza matukio kama ambavyo wameingiza Tishet na kofia za M4C bado inatakiwa kuwa na ushahidi ili kuwaumbua jambo ambalo naamin CHADEMA wanalifanyia kazi,,,,

Jamani hata wafanyeje 2015 CCM hawaoni ndani,,,tujiandae kisaikolojia kupokea ukombozi wa pili kupitia CHADEMA mwaka 2015 si mbali...Ahsante sana mzee tupatupa wa lumumba
 
Kitu kingine cha muhimu nashauri CDM wafanye tathimini ya kina juu ya washitakiwa hao wale vijana wa Igunga waliojumuishwa kwenye kesi hiyo waangaliwe kwa pande mbili nahisi hawako mbali sana na alichokifanya Rudovick kwani ni vizuri CDM wakafuatilia historia yao na kujua wanajipanga vipi na hili.
 
Majuzi Obama aliwaambia demokrasia si tu kufanya uchaguzi bali hata namna mnavyovichukulia vya pinzani na hoja zao lakini kwa hapa kwetu hili limekuwa gumu sana kueleweka wapinzani wataitwa magaini mara watekaji,wahuni kila kibaya kinafanywa na wao so hata hili sishangai sana
 
Nadhani ndani ya CCM kuna tatizo kubwa, ambalo sijui kama wao wanaliona? ukitizama mambo machafu mangi yanajirudia rudia kwa mtindo wa kufanana, na mitndo wanayo tumia kuichafua chadema inakuwa ni dhahifu sana, yaani ni rahisi sana kwa mtu anayefikili kujua hii ni serikali ya CCM inahusika, sasa najiuliza labda wana jiamini kwasababu wanajua mahaka iko chini yao hivyo wana fosi ata sehemu ambayo inaonesha dhahiri ni kuchafua watu wengine?
 
Nashangaa polisi wako bize kutafuta wa tindikali lakini waliofanya hili hatujaambiwa wako wapi..
wakalacdm2.jpg
Huyu alikuwa wakala wa chadema, Green Guard wakamfanya hivi​
wasiwasi wangu ni kuwa yule jamaa alie weka ushahidi wake youtube kuwa walimumwangia tindikali ni ccm wenyewe sijui kama atakuwa hai kwani
 
Mzee Tupatupa mi nilidhani hii ingekuwa siri ya kesi na ingetokea kama supprise, sasa kwa kuliexpose humu sio supprise tena na jamaa watajipanga kuhujumu! Better ungefanya ushauli kwa meseji binafsi kuliko humu, manaake humu hata shetani hupitiapitia!
 
Mkuu Crashwise huo wasiwasi wa yule kijana aliyetoa ushahidi wake youtube kama yupo hai nami ninao sana.
 
Last edited by a moderator:
Igunga kuna kesi.Ni kesi ya ugaidi dhidi ya Makamanda mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Kileo wa Dar. Makamanda hawa wanatuhumiwa kumteka na kumwagia tindikali Tesha-wa-Igunga. Uhalifu aliofanyiwaTesha-wa-Igunga si wa kuushabikia. Ni ukatili dhidi ya ubinaadamu.Naulaani.

Lakini, udhalimu ule aliofanyiwa usifanywe mtaji wakisiasa na kupaka matope chama fulani. Sheria zipo;vyombo vya kisheria vipo.Viachwe vifanye kazi. Hakuna haja ya viongozi wa kichama kuwa walalamikaji,washtaki,na mashahidi. Hakuna haja ya kumfanya Tesha-wa-Igunga kama lulu kwa CCM na kumtumia kuombea kura. Kufanya hivi, ni kufilisika kisiasa.

CHADEMA,wakati wenu ni huu. Jilindeni dhidi na mnayoyadai kuwa ni 'mafilamu' ya chama tawala. Pamoja na kuwa na Mawakili wasomi wenye weledi,bado mnahitaji mashahidi. Mashahidi wanapatikana Igunga.Mmojawao ni kijana (aliyewahi kuwekwa Youtube yake humu) ambaye alihama toka CCM kwenda CHADEMA. Kijana huyu alisema jambo juu ya Tesha-wa-Igunga.

Alisema kuwa Tesha-wa-Igunga amemwagiwa tindikali nawana-CCM wenzake ambao aliwadhulumu pesa zao za posho ya kampeni. Kijana huyu atafutwe,alindwe na atumike kama shahidi. Kwa wafuatiliaji wa Igunga watakubaliana nami kuwa wakati wa kampeni filamu ilianza kutengenezwa. Ikadaiwa kuwa CHADEMA walivamia nyumba fulani na kuiteketeza kwa moto. Cha kushangaza,viliungua vitu vyote pamoja na nyumba husika lakini kuna kitu kikabaki.

Ni kitu kilichotarajiwa kuungua mapema kuliko vingine.Karatasi. Eti, ilibaki karatasi (kipeperushi) kilichodai kuandikwa kwa tambo na CHADEMA kuwa wao ndio waliochoma nyumba hiyo. Ngumu kuamini.

Kamanda Kileo na wenzake wanaimani na kuisubiri CHADEMA.Wamejawa matumaini ya kuoshwa dhidi ya kesi yao na kurudi ulingoni kupambana kisiasa. Kamanda Kileo na wenzake wanatamani kupata ushindi wa ki-Lwakatare. Amini nawaambieni, ipo siku Tanzania itakuwa na siasa safi na za ushindani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.

CC Dr.W.Slaa , Tumaini Makene , Mikael P Aweda , Ben Saanane , John Mnyika
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom