CHADEMA hili la migogoro ndani ya chama msilikubali kamwe!

CHADEMA hili la migogoro ndani ya chama msilikubali kamwe!

Lordita

Member
Joined
May 11, 2017
Posts
16
Reaction score
16
Wanachama kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa za vyama vingi hususani nchi zinazoendelea ambazo watu wake hawajakomaa kwa kila nyaja ya maisha ya mwanadamu iwe kisiasa au kiuchumi.

Awe mwanachama wa kawaida, awe kiongozi mwandamizi wa chama, awe kiongozi wa serikali kupitia chama au hata mwasisi wa chama kama anahama chama mwacheni ahame tu.

Awe ameamua mwenyewe, awe amerubuniwa, awe amehongwa, awe ameahidiwa chochote kitu au awe msaliti ilimradi amehama chama mwacheni ahame kwani kuhama chama si jambo geni katika siasa za nchi kama yetu.

Ila mgogoro ndani ya chama kamwe msiukubali wala kuuruhusu utokee, kwa gharama yoyote chama kilindwe dhidi ya migogoro ndani ya chama.
 
Hakuna mgogoro wowote utakaotokea Chadema , si leo wala kesho .
 
Back
Top Bottom