CHADEMA hii ni vita,tushikamane kuliko wakati wowote

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,075
114,591
Chama kinapitia katika wakati mgumu sana katika awamu ya Tano. Upinzani kwa ujumla hautakiwi nchi hii,ni basi tu wenye dola hawawezi kusema wazi badala yake ni kukandamiza haki ya vyama na wanachama.

Mengi yamefanyika sihitaji kuweka orodha hapa.Lakini Leo hii mwenyekiti kachafuliwa. Hadhi ya mwenyekiti ampake pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni imetikiswa.

Ni shabiki mandazi pekee anayeweza kukubaliana na hili LA "Philemone" Mbowe kuuza madawa.Kwa mtu anayejua ugumu wa kuwa kiongozi wa chama kikubwa kama Chadema sio rahisi kabisa kushiriki kwenye biashara harama yeyote halafu ukabaki salama kipindi chote hiki. Na ni mwanachama mjinga pekee anayeweza kuamini kwamba "eti kutajwa na Makonda" ndio ushahidi kwamba Mbowe anahusika na madawa.Just kutajwa na Makonda!!!!!!

Tunajua hii ni vita kama vita iliyojaa hujuma,kama unaweza kumdhalilisha Tundu Lissu kiasi hiki,utashindwaje kumdhalilisha Mwenyekiti Mbowe??

Nawasihi makamanda wangu makini kushikamana imara kama tulivyoshikamana kipindi kigumu cha Uchaguzi wa 2015. Tumuombee kamanda wetu Mkuu ashinde kadhia hii

NITAKUWA WA MWISHO KUAMINI MH.MBOWE NI DEALER
 
Hupaswi kumuamini mtu kiasi hicho wala hupaswi kulichukulia hili swala kisiasa, ye ameitwa aende akasikilize ameitiwa nini baada ya hapo ndipo tutajua sasa nini kinaendelea hajaonewa mtu hapa!

Huo mshikamano unaoutaka sijui ni upi sasa! mtaandamana au! and for what!!? mwisho wa siku every man at himself! usipigane vita visivyokuhusu.
 
Hata mkewe hawezi kutoa ushahidi 100% kuwa mbowe hausiki biashara hii inaweza fanyika hata pasipo familia kujua ni kama ujambazi tu pont ya msingi kuwa kati tu usitetee au kushutumu ni mahakama pekee ndio itayotoa jibu kama ni kweli au si kweli
 
Guys huu ndo wakat muafaka wa kuitikisa CCM wameshacross de line breakin rules
Mnaonaje na nyie mtoe list yenu ya wanaomsaidia makonda kujenga na kusafiri na jnci walivyoconnected na mapowder kwenye press confrence. waache kuwadanganya wabongo
*** Strike back hard ****
 
Hupaswi kumuamini mtu kiasi hicho wala hupaswi kulichukulia hili swala kisiasa, ye ameitwa aende akasikilize ameitiwa nini baada ya hapo ndipo tutajua sasa nini kinaendelea hajaonewa mtu hapa!

Huo mshikamano unaoutaka sijui ni upi sasa! mtaandamana au! and for what!!? mwisho wa siku every man at himself! usipigane vita visivyokuhusu.
Nice...
 
Hivi Serikali ikitaka kuimaliza chadema inashindwa kweli? Serikali ya JMTZ ambayo pia inaongoza Bunge la JMTZ iamue kuiondoa chadema Tanzania itashindwa? Nani anailipa chadema ruzuku? Serikali inashindwa nini kuiundia chadema zengwe na kuinyima ruzuku? Seriklai ikituma tu Mkaguzi wa Mahesabu kuhusu matumizi ya fedha zake chadema hiyo ni sababu tosha ya kuinyima chadema ruzuku tena kisheria kabisa, Acheni ujinga, Mbowe ana tuhumumiwa aende kujisafisha akitoka msafi, ndiyo muongee!
 
Halafu he mtu yeyote akimtaja Makonda au yeyote wa juu yake kuwa anatumia,au anajihusisha,je aliyetajwa atakamatwa? najiuliza sheria inasemaje kuhusu kutajaaa!
 
Cha kufanya sasa hivi. Mbowe aitishe Press conference awahutubie watanzania. Nchi iko kwenye shock kubwa sana wakati huu.
 
Back
Top Bottom