Its Tesha
Senior Member
- Oct 6, 2025
- 168
- 604
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kitazungumza na waandishi wa habari saa nane kamili mchana.
Pia Soma >> CHADEMA: Gari la Makamu Mwenyekiti limeshambuliwa kwa risasi za moto Oktoba 18
View: https://www.youtube.com/watch?v=ZtFOeA1qkhk
Updates
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa mawasiliano CHADEMA, Brenda Rupia amesema kuwa Taarifa iliyotolewa na idara ya uhamiaji kuwa John Heche amevunja sheria kwa kwenda nje ya nchi bila kufuata utaratibu si ya kweli na inapotosha kwani Heche bado yupo nchini.
Amesema kuwa taarifa hiyo iliyotolewa na Uhamiaji ni sababu ya kutaka kumuweka Heche kizuizini hadi tarehe 29 Oktoba itakapopita, hivyo taarifa hiyo ni ya kupika.
Amefafanua kuwa chama chao hakitaweza kuhudhuria mazisihi ya Raila Odinga kwa sababu serikali ya CCM imewazuia kuvuka mpaka wa Tanzania na Kenya.
Brenda amegusia pia kuwa toka Passport yake pamoja na ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Amani Golugwa hazijarudishwa toka zilipochukuliwa kwa nyakati tofauti walipotaka kusafiri miezi michache iliyopita. Wameitaka serikali iwarudishie passport zao.
Ameeleza kuwa siku ya oktoba 18, 2025 gari la mwenyekiti wa chama hicho John Heche lilishambuliwa kwa risasi za moto na kupasuliwa matairi kisha kuvutwa hadi polisi ambapo wanamshikilia na dereva na wamekataa kumpa dhamana.