Ukifuatilia kwa makini, utagundua chama cha harakati [CHADEMA] hawajui wanahitaji nini ili kufikia malengo ya ajenda yao ya NRNE.
Leo hii, akiibuka mtu yoyote kutoka chama chochote na kusemea kuhusu ajenda ya No Reforms, No Election basi watapanda gari lake na kusema ni shujaa wao.
Hii ni kwa sababu, CHADEMA kama chama cha kisiasa hakina watu wenye haiba ya uongozi wenye uwezo wa kusukuma mabadiliko ya kisiasa, ila wana kundi la watu wenye haiba ya harakati kwa wananchi.
Ndio maana, ni rahisi kuwafahamu vijana wenye matusi wa CHADEMA kuliko kuwafahamu viongozi wanaoweza kujenga hoja ndani ya chama.
Sasa ajenda za mabadiliko zinatakiwa zijengwe na viongozi wenye haiba ya uongozi kwa wananchi wake, watanzania hawajawahi kuwapokea vizuri wanaharakati, ndio maana akitokea kiongozi wa chama kingine wanamrukia na kumgeuza shujaa, ilihali huyo kiongozi anawatumia CHADEMA kisha mambo yakikaa vizuri kwenye chama chake, anarudi anaendelea na majukumu yake.
Ndugu yangu inaonekana hujui hata maana ya agenda.
Agenda kuu kwa sasa ni kutokubali nchi yetu kuendelea kusimama katika laana ya dhuluma ya haki, ikiwemo haki za kuchagua viongozi, haki za kutoa maoni bila kudhuriwa, na haki za kuishi.
Kwenye haki za uchaguzi, kaulimbiu ni No Reforms No Election.
Hivyo kwa CHADEMA, bila ya kujali mtu ni wa chama gani, wa dini gani, wa jinsia gani, wa kabila gani, wa eneo gani, alimradi anazungumzia haki ya wananchi kuwa na mamlaka ya kuwachagua viongozi wao, huyo ataungwa mkono, kwani anaongelea haki.
Hata ikitokea Samia leo hii akampokea Roho wa Mungu, akabadilika, akaiendea haki badala ya dhuluma, CHADEMA na wapenda haki wote watamwunga mkono. Kwani kinachoangaliwa ni agenda, siyo nani katamka. Hata CCM nzima ikajitenga na shetani, ikatangaza kuwa mwelekeo mpya wa CCM ni kuona haki, uhuru na uwazi vinakuwa mwongozo katika kila jambo, wapenda haki wote wataunga mkono tamko hilo, na hata vyama vyote vitaweza kuja pamoja na kufanya makubaliano ya namna ya uendeshaji wa chaguzi zetu kwa kuzingatia miongozo hiyo. Maana kwa sasa, kikwazo kikubwa cha kutendeka haki nchini mwetu, ni CCM na watawala.
Kumbuka ni furaha na faraja kubwa ikitokea mdhulumu haki mmoja akabadilika na kuwa mpenda haki kuliko hata 10 ambao siku zote wamekuwa wapenda haki. Mabadiliko yatakuja kwa wengi wadhulumu haki watakapobadilika na kuiendea haki.