CHADEMA: Hatutakoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Hatutakoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Serayamajimbo, Dec 15, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na Mwandishi Wetu
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kamwe hakitaacha kumkosoa Rais Jakaya Kikwete na serikali yake katika mambo ambayo hafanyi vizuri, sambamba na kuwataka Watanzania wasimchague kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2010, kwa sababu zipo dalili za wazi zinazoonyeha kuwa utawala umemshinda.
  Kimesema kauli ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyotangazwa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, kuwa kauli zinazotolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuhusu uwezo wa Rais Kikwete kuongoza nchi zinalenga kumdhalilisha, haikubaliki kwa sababu inapingana na wosia wa muasisi wa chama hicho, hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye chama hicho kimekuwa kikihubiri kumuenzi.
  Msimamo huo wa CHADEMA dhidi ya kauli ya CCM ulitolewa jana na viongozi wawili wa chama hicho.
  Wa kwanza kueleza msimamo huo alikuwa Mbowe wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibara uliofanyika jana kwenye mfululizo wa mikutano ya CHADEMA.
  Mbowe alisema amefikia uamuzi huo baada ya kauli ya kejeli iliyotolewa juzi na John Chiligati kuwa anawapotosha Watanzania.
  “Napenda kumwambia Rais Jakaya Kikwete kwamba simuogopi, nitaendelea kumkosa hadi siku ya mwisho ya utawala wake, lakini namheshimu kama rais wangu wa nchi… hatukubali kuona taifa linapotea huku tukiwa kimya, hiyo itakuwa si kazi ya vyama vya upinzani,” alisema Mbowe.
  Alisema kutokana na dhamira yake ya kuwakomboa Watanzania, hatakuwa tayari kucheka na kiongozi yeyote wa chama tawala huku wananchi wakiendelea kutaabika bila msaada kutoka serikalini.
  “Siko tayari kuchekea kiongozi yeyote wakati hali za wananchi wetu zinazidi kuwa mbaya kila kukicha, kila kona unayopita wananchi wanalia hali ngumu ya umaskini,” alisema Mbowe.
  Alisema moto uliowashwa na chama chake utaendelea kuwaka hadi kieleweke na kuridhika kuwa nchi inabadilika na kurudi kama ilivyokuwa kwa muasisi wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.
  Mbowe alitumia fursa hiyo pia kuwatumia salamu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati kwamba atabanana nao hadi mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu.
  “Natumia nafasi hii kuwatumia salamu, Waziri Mkuu, Pinda, Makamba na Chiligati kwamba nitaendelea kupambana nao tu.... nasema kwamba hawa ninao tu ndugu zangu,” alisema Mbowe.
  Aliishutumu CCM kuwa kipindi kirefu imekuwa haitaki kuambiwa ukweli kutokana na makosa mengi inayofanya tangu taifa lilipojipatia uhuru mwaka 1961.
  “CCM imekuwa bingwa wa kukutaa kukosolewa pale inapofanya makosa...imegeuza Watanzania kuwa kitega uchumi chao huku wakibaki maskini wa kutupwa, angalieni leo hapa Mwibara mmeshindwa hata kuvua samaki,” alisema.
  Kwamba hali ya umaskini imesababisha wananchi wengi wa Kanda ya Ziwa kula mabaki ya samaki, maarufu kwa jina la ‘mapanki’ huku minofu yake ikisafirishwa kwenda nchi za Ulaya.
  Akisisitiza msimamo wake wa kuendelea kuwakosoa viongozi walioko madarakani, alisema kutokana na serikali kupoteza mwelekeo, wafanyakazi wa serikali wakiwemo walimu wana haki ya kugoma na kudai masilahi yao kwa nguvu zote kwasababu ni haki yao ya msingi.
  Wa pili alikuwa Mkurugenzi wa Vijana wa chama hicho, John Mnyika, alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu msimamo wa chama hicho baada ya Mwenyekiti wake, Mbowe kushambuliwa na CCM kwa kauli zake dhidi ya Rais Kikwete.
  Akiongea kwa sauti kali, Mnyika alisema kamwe CHADEMA haitaacha kutoa kilio cha umma na kwamba viongozi wa chama hicho wako tayari kukamatwa na hata kufungwa gerezani kwa ajili ya kutetea wanyonge.
  Alisema kauli za CCM hazitawatikisa CHADEMA wala kuwanyamazisha kwa vile wanatambua kuwa mara nyingi viongozi wanaoshindwa kujibu hoja hutumia mamlaka yao kuwanyamazisha wananchi wenye hoja za msingi za kukosoa watawala.
  Alitoa mfano kuwa hata Rais wa Kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere aliwahi kushitakiwa na serikali ya kikoloni kwa kusema ukweli ambao ulitafsiriwa na watawala hao kuwa ni uchochezi.
  Mnyika, alisema kauli zinazotolewa na Mbowe kuhusu uongozi wa Rais Kikwete ni kauli za umma na kwamba zina ukweli ambao unasemwa na wananchi walioelemewa na ugumu wa maisha, wakiwemo wasomi, wanaharakati na viongozi wa dini.
  “Heshima ya kiongozi inalindwa na matendo yake, wapo Watanzania wanaoona kwamba Rais Kikwete anashindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi na kutekeleza ahadi alizotoa, ndiyo maana wanamsema.
  “CCM wameanza kutaharuki kutokana na Operesheni Sangara kwa kuwa ufisadi unaotajwa unaigusa CCM na baadhi ya viongozi wake. Wananchi wameanza kupinga hali hiyo, jambo ambalo halikutarajiwa na viongozi wa CCM, ndiyo maana wameanza kuhaha,” alisema Mnyika.
  Mnyika alimtaka Chiligati kuacha kutoa kauli zinazolenga kumpotosha Rais Kikwete na kwenda katika mwenendo anaoutaka rais, wa kukosolewa na kushauriwa kila inapobidi.
  Alisema kauli ya Chiligati ya kumpamba Rais Kikwete hata katika mambo anayoonekana hajafanya vizuri na Watanzania anaowaongoza wananung’unika, zinaweza kuzaa udikteta wa kukwepa kubadilika.
  “CCM inaelekea kwenye kuminya fikra mbadala; ililifungia gazeti la MwanaHalisi kwa sababu ambazo hadi sasa zinatia shaka miongoni mwa Watanzania na sasa imemkemea Mbowe ambaye anazungumza kile kilichopo. Hali ikiendelea hivi, itageuka kwa wakosoaji wengine. CHADEMA tunasema CCM, na hasa Chiligati, wasome wosia wa Julius Nyerere ‘tujirekebishe’ utawasaidia kukubali kukosolewa,” alisema Mnyika.
  Alimtaka Chiligati aache kupoteza muda kufanya propanda za kisiasa, badala yake aeleze hatua alizowachukulia watu walio katika orodha ya mafisadi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anayoingoza, ambayo alikabidhiwa na mtangulizi wake.
  Kauli hiyo ya Mnyika imetolewa siku moja baada ya CCM kueleza kukasirishwa, kukerwa na kusikitishwa na kauli ya hivi karibu ya Mbowe ya kumshutumu Rais Kikwete kuhusu uwezo wake wa kuongoza kuwa zinaonyesha kumdhalilisha na kumkosea adabu na heshima mkuu wa nchi. Tamko hilo la CCM lilionekana kama kujibu mapigo dhidi ya kauli ya Mbowe kwa Rais Kikwete; lilikwenda mbali zaidi kwa kumkejeli na kumdharau Mbowe, kwa kumhusisha na upigaji disko na uchezaji wa kamari.
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mwenzake inamshinda nchi, yeye chama tu kinasambaratika, akipewa nchi je? Nafikiri njia nzuri ya kumkosoa Rais iwe ni pamoja na kumpa alternatives. Sasa sisi tunasema tuuu, tunataja matatizo mengi tu ya chama tawala, leta mapendekezo yako sasa. Wabunge wa upinzani tunao bungeni na nchi inakwenda hovyo na wenyewe wakiwemo humohumo na wengine ni member wa kamati za fedha na uchumi, kwanini wasilete mabadiliko huko. Unafiki tu, hamna lolote!
   
 3. b

  bigilankana Senior Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lawama lawama lawama. toeni mbadala
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nyie mnaona mambo ni sawa hivyo kwamba watu wasilaumu?
  Toa mbadala wako wewe kwanza unaoona kabla ya kulaumu wengine.
  Kama ni mbadala mbona wameambiwa siku nyingi sisi m? wewe mgeni hapa nchini nini?
   
 5. b

  bigilankana Senior Member

  #5
  Dec 16, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya, mimi naomba kura mpaka nitoe mbadala? wanaotaka kura yangu nataka waniambie mbadala.

  Ndio mimi mgeni, sina haki kuhoji? Toeni mbadala mmeshasema sana miaka minne tumewasikia na hakuna jipya. Tuambieni sasa nyie mtafanya nini?
   
 6. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Bagilikana
  Join Date:
  Tue Dec 2009
  Posts: 17
  Thanks: 1
  Thanked 0 Times in 0 Posts
  Rep Power: 0 [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]

  Mwaka huu tutaona mengi sana hapa ya kuitetea CCM hasa kwa wana JF waliojiunga wiki iliyopita;Bagilinkana karibu sana jamvini na sera zako endelevu za Lumumba street!

  "Uwe una hakikisha kila ukitoa andiko la kuwatetea unaenda kudai chako right away,maana hawa watu ni wajanja sana,wakikutumia wanaweza wakakuona na wewe worthless kama walivyowafanya wenzako waliotangulia"
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hakuna sera mbadala Tanzania ila kuna nia ya kuondoa personalities na vyama fulani basi!

  Ni sawa na kubadilisha chief...kama ni hivyo si ccm na wenyewe watatuwekea mtu mwingine 2015

  waambieni wananchi mtakachofanya kwenye maeneo ya elimu, afya, uchumi tofauti na wanavyofanya ccm...mnatumia media na resources zenu vibaya shame
   
Loading...