CHADEMA: Hatuna ugomvi na Polisi

CHADEMA: Hatuna ugomvi na Polisi

smigon

Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
8
Reaction score
0
Wakati kukionekana kuwapo kwa mvutano mkali kati ya Jeshi la Polisi nchini na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chama hicho kimesema kuwa hakitakubali kukaa kimya wakati baadhi ya watumishi wa jeshi hilo wakitumiwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa kukandamiza raia.

Chama hicho kimesema hakina ugomvi na jeshi hilo kwa ujumla wake, isipokuwa askari wachache kiliodai wanatumiwa vibaya kuhujumu haki za binadamu na demokrasia nchini, kikisema hao ndiyo wanalipaka matope jeshi hilo na kuzidi kulikosesha imani kwa wananchi.

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara Tabora mjini, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema chama hicho hakitarudi nyuma kutetea haki na matumaini ya Watanzania.

Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi, ukiwa ni sehemu ya kukamilisha kuzindua Kanda ya Magharibi (mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi), ikiwa ni mkakati wa chama hicho wa kujiendesha kwa kanda.

“Ndugu zangu watu wa Tabora, wanachama na wapenzi wetu wa Kanda ya Magharibi, katika mapambano haya ya kuing’oa CCM na kuleta mabadiliko makubwa ya mfumo na utawala ndani ya nchi yetu, tumefika mahali utetezi wa haki na matumaini ya wananchi umegeuzwa kuwa ni vurugu au fujo…kila leo mnasikia chama chenu ambacho kimezidi kuwa na ushawishi miongoni mwa Watanzania wengi wenye kiu kubwa ya mabadiliko, kinafanyiwa vituko, kimoja baada ya kingine,” alisema.

Alisema hivi sasa wafuasi na wapenzi wa chama hicho wanatekwa, wanateswa, kupigwa na hata kuuawa.
“Matukio ya namna hii yanazidi na sisi tumesema hatuwezi kuendelea kulalamika na kulialia kwa vyombo husika. Tutajilinda,” alisema.

“Tunatambua umuhimu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Taifa linawahitaji wawe waadilifu, watimize wajibu na kutenda haki kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. CHADEMA tunawatetea hawa ndani na nje ya Bunge, lakini hatutakubaliana na askari wanaotumika vibaya, kwa kupewa amri za hovyo, kama kwenye tukio la bomu Arusha,” alisema Mbowe.

Akizungumzia suala la mjadala wa rasimu ya Katiba Mpya, Mbowe alisema mapema mwezi Agosti, mwaka huu, chama hicho kitaanza kuzunguka nchi nzima kwenye operesheni M4C-Katiba Mpya; na kitaendesha mabaraza yake kwa uwazi kwenye mikutano ya hadhara.
 
Kuna Polisi wazuri tu, Nimegundua hata OCD wa Morogro ana akili sana. Mkutano wa mwisho wa Dk ulisimamiwa vizuri sana. Wangeiga mfano wa huyu afande, awape semina.
 
mchaga na pesa? anahiyari watu wapoteze maisha ili apate mradi wake.
 
wakati kukionekana kuwapo kwa mvutano mkali kati ya jeshi la polisi nchini na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), chama hicho kimesema kuwa hakitakubali kukaa kimya wakati baadhi ya watumishi wa jeshi hilo wakitumiwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa kukandamiza raia.

Chama hicho kimesema hakina ugomvi na jeshi hilo kwa ujumla wake, isipokuwa askari wachache kiliodai wanatumiwa vibaya kuhujumu haki za binadamu na demokrasia nchini, kikisema hao ndiyo wanalipaka matope jeshi hilo na kuzidi kulikosesha imani kwa wananchi.

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara tabora mjini, mwenyekiti wa chadema, freeman mbowe, alisema chama hicho hakitarudi nyuma kutetea haki na matumaini ya watanzania.

Mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa chipukizi, ukiwa ni sehemu ya kukamilisha kuzindua kanda ya magharibi (mikoa ya kigoma, tabora na katavi), ikiwa ni mkakati wa chama hicho wa kujiendesha kwa kanda.

"ndugu zangu watu wa tabora, wanachama na wapenzi wetu wa kanda ya magharibi, katika mapambano haya ya kuing'oa ccm na kuleta mabadiliko makubwa ya mfumo na utawala ndani ya nchi yetu, tumefika mahali utetezi wa haki na matumaini ya wananchi umegeuzwa kuwa ni vurugu au fujo…kila leo mnasikia chama chenu ambacho kimezidi kuwa na ushawishi miongoni mwa watanzania wengi wenye kiu kubwa ya mabadiliko, kinafanyiwa vituko, kimoja baada ya kingine," alisema.

Alisema hivi sasa wafuasi na wapenzi wa chama hicho wanatekwa, wanateswa, kupigwa na hata kuuawa.
"matukio ya namna hii yanazidi na sisi tumesema hatuwezi kuendelea kulalamika na kulialia kwa vyombo husika. Tutajilinda," alisema.

"tunatambua umuhimu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Taifa linawahitaji wawe waadilifu, watimize wajibu na kutenda haki kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Chadema tunawatetea hawa ndani na nje ya bunge, lakini hatutakubaliana na askari wanaotumika vibaya, kwa kupewa amri za hovyo, kama kwenye tukio la bomu arusha," alisema mbowe.

Akizungumzia suala la mjadala wa rasimu ya katiba mpya, mbowe alisema mapema mwezi agosti, mwaka huu, chama hicho kitaanza kuzunguka nchi nzima kwenye operesheni m4c-katiba mpya; na kitaendesha mabaraza yake kwa uwazi kwenye mikutano ya hadhara.

ni vizuri chadema tuandae orodha ya polisi wanaotesa na kuwaua wanachadema.tuwachukue na video kabisa.kuna siku itatusaidia !!
 
Wapo polisi wanaojali taaluma yao na kufanya kazi zao kwa uadilifu na haki kama aliekuwa RPC wa mwanza kamanda SIRRO,baadae aliondolewa pale,kama kawaida ya serikali mtenda haki hadumu!
 
Kuna Polisi wazuri tu, Nimegundua hata OCD wa Morogro ana akili sana. Mkutano wa mwisho wa Dk ulisimamiwa vizuri sana. Wangeiga mfano wa huyu afande, awape semina.

Ni kweli mkuu. Ila naungana na mmoja wetu hapa kuchukua list ya polisi watumwa wa ccm wanaoua watu, na si ivyo tu ni vizuri kuratibu nyendo zawanaodhamini na kusababisha vifo vya watu maana hao ndo wakushugulikiwa. Hatuhitaji watanzania kuchukiana wakati waanzilishi wa chuki wapo na ndo wakuwajibishwa.
 
Wakati kukionekana kuwapo kwa mvutano mkali kati ya Jeshi la Polisi nchini na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chama hicho kimesema kuwa hakitakubali kukaa kimya wakati baadhi ya watumishi wa jeshi hilo wakitumiwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa kukandamiza raia.

Chama hicho kimesema hakina ugomvi na jeshi hilo kwa ujumla wake, isipokuwa askari wachache kiliodai wanatumiwa vibaya kuhujumu haki za binadamu na demokrasia nchini, kikisema hao ndiyo wanalipaka matope jeshi hilo na kuzidi kulikosesha imani kwa wananchi.

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara Tabora mjini, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema chama hicho hakitarudi nyuma kutetea haki na matumaini ya Watanzania.

Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi, ukiwa ni sehemu ya kukamilisha kuzindua Kanda ya Magharibi (mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi), ikiwa ni mkakati wa chama hicho wa kujiendesha kwa kanda.

"Ndugu zangu watu wa Tabora, wanachama na wapenzi wetu wa Kanda ya Magharibi, katika mapambano haya ya kuing'oa CCM na kuleta mabadiliko makubwa ya mfumo na utawala ndani ya nchi yetu, tumefika mahali utetezi wa haki na matumaini ya wananchi umegeuzwa kuwa ni vurugu au fujo…kila leo mnasikia chama chenu ambacho kimezidi kuwa na ushawishi miongoni mwa Watanzania wengi wenye kiu kubwa ya mabadiliko, kinafanyiwa vituko, kimoja baada ya kingine," alisema.

Alisema hivi sasa wafuasi na wapenzi wa chama hicho wanatekwa, wanateswa, kupigwa na hata kuuawa.
"Matukio ya namna hii yanazidi na sisi tumesema hatuwezi kuendelea kulalamika na kulialia kwa vyombo husika. Tutajilinda," alisema.

"Tunatambua umuhimu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Taifa linawahitaji wawe waadilifu, watimize wajibu na kutenda haki kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. CHADEMA tunawatetea hawa ndani na nje ya Bunge, lakini hatutakubaliana na askari wanaotumika vibaya, kwa kupewa amri za hovyo, kama kwenye tukio la bomu Arusha," alisema Mbowe.

Akizungumzia suala la mjadala wa rasimu ya Katiba Mpya, Mbowe alisema mapema mwezi Agosti, mwaka huu, chama hicho kitaanza kuzunguka nchi nzima kwenye operesheni M4C-Katiba Mpya; na kitaendesha mabaraza yake kwa uwazi kwenye mikutano ya hadhara.
Huh!
Mbowe amekabwa nii?
What took him so long to sat that?

Inajulikana wazi kuwa , kwa kuamua na kwa mipango, Polisi ni spaaring partners wa CHADEMA!
Why say it now?
 
Hivi unapofikia hatua unatukana Majeshi hasa JWTZ na vyombo vingine vya usalama unakuwa una maana gani? Hivi siku ukiwa rais au mwenye mamlaka utavitazama na kuviamrisha kwa jicho gani?
Wachaga bwana, kweli wana agenda ya siri.
 
Ni kweli mkuu. Ila naungana na mmoja wetu hapa kuchukua list ya polisi watumwa wa ccm wanaoua watu, na si ivyo tu ni vizuri kuratibu nyendo zawanaodhamini na kusababisha vifo vya watu maana hao ndo wakushugulikiwa. Hatuhitaji watanzania kuchukiana wakati waanzilishi wa chuki wapo na ndo wakuwajibishwa.

1. chagonja
2. kamuhanda
3. andengenye
 
Hivi unapofikia hatua unatukana Majeshi hasa JWTZ na vyombo vingine vya usalama unakuwa una maana gani? Hivi siku ukiwa rais au mwenye mamlaka utavitazama na kuviamrisha kwa jicho gani?
Wachaga bwana, kweli wana agenda ya siri.

Haya uliyoandika hayakusadii pamoja na nia yako mbaya. CDM inajari na kuthamini vyombo vya dola pindi tu vinapotimiza wajibu wao vizuri. Wachache ktk vyombo hivyo niwaku-black list maana wametumiwa kuua raia. Kwa taarifa yako wengi ktk vyombo hivyo si wajinga. Wameona, wametathimini na kugundua sism ni janga la taifa. Wako tayari kwa lolote. Nani anawezavumilia upuuzi wenu . Sasa mnachonganisha watzn kwa udini, ukabila na ukanda bado tu mmetutafutia maadui ndani na nje ya nchi. Kama ilo halitoshi mnawaangaiza vijana kwa madawa ya kulevya. Subiri 2015...tutavumilia wakati kidogo.
 
CDM lazima sasa waanze kujiweka ktk mstari kwa kufanya mapping.wabaya wajulikane na kuwafanyia mapping wakati huu wazuri nao wape map yao.

I can observe CDM are in the process of being vetted by the good institutions.Good move
 
Good observations Lu.ma.ga! Sasa hivi niko vijijini (baadhi amevitembelea Rais siku mbili zilizopita), ni bendera tu za cdm zinapepea! Hata hivyo nyingine zimezeeka na niombe tu cdm walitambue hilo ili wasambaze nyingine(majimbo ya kyerwa na karagwe).
 
Kuna Polisi wazuri tu, Nimegundua hata OCD wa Morogro ana akili sana. Mkutano wa mwisho wa Dk ulisimamiwa vizuri sana. Wangeiga mfano wa huyu afande, awape semina.

Mkuu angalia tusije tukamkuta "amejinyonga" kama yule mwingine..
 
Back
Top Bottom