Ben Saanane, Habib Nchange, Juliana Shonza, Mwampamba, Exaud Mamuya, Gwakisa, Sanga na Zitto ZK
Nimejitahidi sana kupitia post zilizowekwa humu jukwaani, kwa mtazamo wangu hawa vijana hapo juu wapo katika kundi maalum lililoandaliwa kuihujumu na kuiua CHADEMA nayasema haya kwa sababu zifuatazo
1. Tumeshuhudia kundi moja likitoa maelezo likijionyesha moja kwa moja linatumika na viongozi wakuu kwa ajili ya kumuangamiza Zitto ikiwa ni pamoja na kutaka kumuua tuuma ambayo ni kubwa sana na ni mbaya sana kwa uhai wa chama
2. Pia tumeona kundi lingine likiwa limeegemea upande wa Zitto na likionyesha mbinu na mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika eti kuleta Demokrasia katika Chama na hili likionyesha Zitto alikuwa akubaliana na viongozi wenzake wa Juu (Mwenyekiti na Katibu Mkuu)na akiwa katika mbinu ya kuanzisha chama kingine (CHAUMA)
3. Hii inaonyesha hawa vijana wamejipanga vyema kulitumia hili jukwaa ili kuuchonganisha uongozi wote wa Juu wa CDM na mwisho wa siku wakose kuaminiana, kuheshimiana.kwani haiingii akilini kama kweli ni mwanachama muadilifu wa CHADEMA watoe maelezo kama haya tuliyoyasoma humu ambayo yalitakiwa yawe siri na utatuzi wake ufanyike kwenye vikao vya ndani vya chama.
4. Pia ningependa kukumbushia ile kauli ya Ndg. Steven Wassira kuwa CDM itakufa kabla ya 2013 hii inajionyesha haya mambo yamepangwa na waliopewa jukumu hilo ni hawa vijana akiwemo na ZITTO kwani tumeshuhudia wengine wakiingiza suala la Ukanda ambalo limezungumzwa sana na Viongozi wa CCM wakati wakiishambulia CDM
5. Pia nimeshuhudia pale Ben Saanane alipokuwa akisakamwa na hawa wenzake yeye alikuwa anagonga Like! Ikimaanisha anawaunga mkono kwa kutoa hicho walichopanga.
** Wito na maoni yangu Uongozi wa Juu wa chama ulitafakari hili na ikiwezekana kuchukua maamuzi magumu ambayo yatakitetelesha chama kwa muda mfupi lakini kukifanya kuwa Imara kwa muda Mrefu na kuheshimika kuliko kama ilivyo sasa ambapo chama kimekuwa kama jumuiya ya Kambale hajulikani baba, mama wala mtoto wote wana masharubu.
Nawasilisha!!!!
[napenda kukupongeza mkuu kwa mada tenye tija na muono wa maendeleo ambayo umeitoa. ki ukweli hoja hii ni nzito na tena inahitaji uwezo mkubwa kuichambua (conscious mind) kimsingi sina maneno na vipengele ambavyo umeviweka ila ninataka kuiangalia zaidi point namba 4 ambayo iko highlighted in red.
ni ikweli ulio thabiti tena haupingiki kwamba CCM imekuwa ikiamini kuwa iko a next step ever.....na ndiyo maana nashawishika kusema mkakati na mpango wote unaoendelea unakila sababu ya kuhusishwa na mkono wa chama hiki kikongwe. kimtazamo siasa nyingi za nchi znazoendelewa zimejazwa kila aina ya ulaghai na matukio ya kupangwa ndani ama juu ya chama kingine (UPINZANI) na hapa ndipo usemi wa politics a date game huthibitika.
Aidha kauli ya WASSIRA juu ya uhai wa CDM ni tata na ambayo inatakiwa iangaliwe kwa mashika tena kwa sura ya undani. kimtazamo hakukuwa na sababu ya chama kinaachoongoza dola kutoa kauli ambazo hazna tija kama hizi tena waziwaz huku kikitoa na wakatii kama si chenyewe ambacho kinatekeleza mkakati fulani unaolenga KUKIBOMOA, KUKIUA, NA HATA KUKISAMBARATISHA kwa njia yoyote chuini ya matakwa yake.
mwisho namnukuu mhshimiwa ZZK aliyewahi kuandika kupitia JF kuwa " hhuwezi kum-maliza zito kisiasa bila kuiua CDM ama kuiua CDM bila kum-maliza zitto,,,,,,,, kauli kama hii inathibitisha mawazo kuwa ZZK asingekuwa mshenzi kufkiri kuihujumu CDM huku akiamini mtaji wake kisisasa unafadhiliwa na kudhaminiwa na CDM.
HITIMISHO
jambo hili lapaswa litzamwe kwa undani san la sivyo litaathiri na kukisambaratisha chama hchi kikuu cha upizani na strugle yao yote ku-end up in vain,,,,,I believe being mor wise and precise CDM wont allow this.]