Chadema hakuna mgogoro wowote

Sio kweli, Ile ni hulka ya Lissu, tuacheni kukuza mambo ambayo hayapp
Watu tunatofautiana sana uwezo wa uoni wa kuona mbali. Mbowe ni compromised na ame surrender kwa Mama, wakati Lissu ni mtu wa no retreat, no surrender!. Iwapo 2025 ni Samia atagombea urais kupitia CCM, the campaign mood would be no offensive politics, kitu ambacho watu wa no compromise, no retreat and no surrender hawawezi kukubali!, moto lazima utawaka!.
P
 
Viongozi wa CHADEMA wasipuuze kwa maana Lisemwalo lipo kama halipo linakuha / Panapofuka moshi kuna moto / Dalili za mvua ni mawingu
 
Ok, ok! Hebu twambie karopoka nini maana inaonekana una akili sana wewe!
 
Kwa hiyo akina P na Ze umoja party watakuwa upande wa no retreat no surrender sio 🤔
 
Nimekuelewa
 
Mungu ibariki Chadema. Chadema ni mpango wa Mungu
 
Kwamba Mbowe ame surrender kwa mama ni uongo wa mchana

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Mwanasiasa akikwambia hainyeshi nje ,Toka na mwamvuli wa dharura.
 
Mbowe ni compromised na ame surrender kwa Mama, wakati Lissu ni mtu wa no retreat, no surrender
Haya ni mawazo Yako, nayaheshimu ila Mbowe ameshinda pakubwa na Samia ndio ame-surrender! Let's be honest, huu mtanange kura zinaenda kwa Mbowe na Chadema! CCM ndio walikua hawataki maridhiano Wala katiba mpya Wala tume huru ya Uchaguzi, leo haya yatafanyika (at least kwa kuzungumzwa) kwa muktadha huu nani amekua compromised?
 
Kwamba Mbowe ame surrender kwa mama ni uongo wa mchana

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Wewe kama bado unadhani Mbowe ni mpinzani, endelea kudhani hivyo, ukweli ni kuwa Mbowe ni compromised na msharika wa CCM kwenye maridhiano, Tanzania sasa tunafanya siasa za maridhiano ambazo upinzani ni urafiki na ushirikiano na sio upinzani uadui, na panapo majaaliwa, Tanzania post 2025, wapinzani watakuwa integrated into the government, na bara tunaanzisha GNU yetu huku.
P
 
sasa unaandika na kujichanganya mwenyewe , kama wapinzani hawapo hao watakaoingizwa kwenye GNU ni akina nani ?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Haya ni mawazo Yako, nayaheshimu
Asante sana kwa kuyaheshimu mawazo yangu, na huu ndio ustaarabu wa mijadala, unaheshimu mawazo kinzani hata kama hukubaliani nayo, thanks for this.
ila Mbowe ameshinda pakubwa na Samia ndio ame-surrender! Let's be honest, huu mtanange kura zinaenda kwa Mbowe na Chadema!
Nakubaliana na wewe ila angalia Samia amemtendea nini Mbowe Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye? ombi hili likajibiwa na Mama kufanya jambo kupitia DPP, sisi watu wa shukrani, tukashikuru, Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito! na Mbowe baada tuu ya kuachiwa unajua alikwenda wapi, kwa nani na kufanya nini?. He was indebted!.

Na baada ya hapo mara ghafla Chadema ikapata uwezo wa kuitisha mikutano, mara Mbowe ana piga trips za ulaya na America, do you know who was behind?. Wajuvi wa siasa za ndani, wanamjua nani ni shujaa wetu wa kweli wa siasa zetu, kama unaamini ni Mbowe, endelea kuamini hivyo...
CCM ndio walikua hawataki maridhiano Wala katiba mpya Wala tume huru ya Uchaguzi, leo haya yatafanyika (at least kwa kuzungumzwa) kwa muktadha huu nani amekua compromised?
Hapa pia nakubaliana na wewe, CCM Magufuli ilikuwa na wahafidhina wengi, kazi ya kusafisha safisha inaendelea, CCM Samia ni CCM moderate.

Kwenye win win situation, hakuna mshindi wala mshindwa, they have all won!.
P.
 
sasa unaandika na kujichanganya mwenyewe , kama wapinzani hawapo hao watakaoingizwa kwenye GNU ni akina nani ?
Tanzania tangu tumeanza mfumo wa vyama vingi, we have never had any serious opposition, hivyo hao wanaitwa wapinzani, actually ni kama wapinzani, hivyo watakaoingizwa kwenye hiyo GNU ya 2025 ni hao hao ni kama!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…