Chadema funika kombe mwanaharamu apite. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema funika kombe mwanaharamu apite.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Jul 2, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kuna kila dalili kwamba mkakati mzito umepangwa kukidhoofisha chama cha demokrasia na maendeleo (chedema) kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Baadhi ya mambo ambayo yanatokea hivi sasa ndani ya chama hicho ni dalili tosha za mpango mkakati huo ambao si ajabu umeandaliwa kiufundi na chama tawala. Mgogoro uliopo kati ya madiwani wa mkoani Arusha na uongozi wa taifa wa chadema umeibua sintofahamu ndani ya chama hicho, na umeguka kuwa mtaji mkubwa kwa wabaya wa chadema pamoja na magazeti yenye mtazamo hasi na chadema kiasi cha kuonesha kwamba chadema sasa ni mapande mapande. Naamini chadema ni chama makini na viongozi wake hawana tabai ya kukurupuka katika kufanya maamuzi mazito. Nawashauri viongozi wa chadema watumie hekima na busara kutatua tatizo lililopo ili kutowanufaisha maadui zake ambao wanasubiri kwa hamu kubwa kuona jinsi chama kitakavyo tetereka ili wapate cha kuzungumza na kuandika. Historia inaonesha chama cha mapinduzi kimekuwa na mbinu nyingi za siri za kudhoofisha vyama ambavyo vinatishia uhai na utwala wa chama hicho. Mfano mzuri ni kile kilichotokea kwa NCCR-Mageuzi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995. Si ajabu mgogoro unaoendelea kati ya uongozi wa chadema katika upande mmoja na madiwani wa chama hicho mkoani Arusha na uongozi wa chadema na John Shibuda kwa upande mwingine ukawa umesukwa na chama tawala ili kutimiza malengo yao ya kisiasa. Ukweli ni kwamba CCM kwa sasa kiko kwenye wakati mgumu na kinapata changamoto kubwa sana kutoka CHADEMA ambazo hakijawahi kuzipata tangu chama hicho kianzishwe miaka 34 iliyopita. changamoto hizo zikiambatana na matatizo mbalimbali yanayoikumba nchi kwa sasa ni dalili mbaya kwa chama tawala. Wakati huohuo CHADEMA kwa sasa kinaungwa mkono na wananchi wengi mijini na vijijini na hii imedhihilishwa baada ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo CHADEMA wameweza kuongoza baadhi ya halmashauri za mijini na vijijini ambako pengine ccm hawakutarajia kama ingeweza kutokea. kanda ya ziwa hasa mikoa ya Mwanza na shhinyanga ambayo kwa miaka mingi imekuwa ngome kubwa ya chama tawala sasa imegeuka kuwa ngome ya CHADEMA baada ya chama hicho kuzoa majimbo 7 ya ubunge katika mikoa hiyommiwili. Hii si dalili njema kwa chama tawala. CCM wanatambua kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha na pia wanafahamu kuwa hata ROMA haikujengwa kwa siku moja, hivyo chadema sasa kiko kwenye mkakati wa kujijenga na ndio maana kimekuwa kikikusanya watu wengi kwenye mikutano yao ya hadhara mijini na vijijini, hali ambayo inakiogopesha chama tawala. Ushauri wangu kwa CHADEMA wawe makini katika kutatua sintofahamu iliyopo na kama ikiwezekana WAFUNIKE KOMBE MWANAHARAMU APITE na kuwanyima ajenda wabaya wake.

  Nawasilisha.
   
Loading...