Chadema. Chalinze

Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,864
5,672
Poleni sana ndugu zangu wana Chadema kwa matokeo ya Kalenga.
Ni kipindi kingine kigumu baada ya kazi nzito ya kampeni ya wiki nne mfurulizo,
Kwa maoni yangu wana Chadema ni kipindi cha kukaa chini na kutafakari mlipojikwaa, kwani pamoja na kuwashilikisha makamanda wote pamoja na chopa lakini kula zimekataa na kukaribia asilimia 20 tu!
Kwa maoni yangu, Chalinze ni pagumu sana afadhari hata Kalenga, hali ya kifedha ya chama kwasasa ni mbaya sana hasa nguvu kubwa mnayotumia ya kampeni ya kushirikisha na Chopa ambazo zinavuta watoto tu ambao hawajafikia kupiga kura, ambayo ni gharama sana, nawashauri jimbo la Chalinze mjitoe tu kwani ni kupoteza fedha tu na energy za watu halafu muambulie patupu tena na kurudi vichwa chini kama Kalenga!
Nawashauri ndugu zangu Chadema muachane na jimbo la Chalinze.
Nawakilisha.
 
Ushauri wa hovyo kweli. Yaani kwako wewe ugumu wa Chalinze nini? Mbona ni Tanzania au kwa kuwa amegombea fisadi mtoto wa fisadi? Hilo lisikupe shaka katika uchaguzi huwezi kujua lolote laweza kutokea, lakini hata wasiposhinda hiyo si ndo nafasi ya kutangaza sera za chama na kukiimarisha? Kumbuka Chadema kwa sasa ni all weather na sio chama cha msimu kwa hiyo lazima kionekane katika matukio yote ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom