Chadema, CCM Na Nchi Iliyomwagiwa Petroli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema, CCM Na Nchi Iliyomwagiwa Petroli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Nov 13, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  It is always seems impossible until it is done- Anasema Nelson Mandela.


  Kwa lugha nyingine, Mzee Mandela anaamanisha hakuna lisilowezekana kwa maana zote, njema na ovu.


  Na tunavyoenenda sasa ardhi ya nchi yetu ni kama vile imemwagiwa mafuta ya petrol. Katika hali hiyo, tuna lazima ya kuwa makini na wenzetu wachache wanaotembea na vibiriti mifukoni. Nchi ikilipuka, basi, sote tutaathirika.


  Kuna jamaa yangu aliyenifuata kuniomba ushauri juu ya ugomvi wake na mkewe. Kwamba nyumbani kwao hawasikilizani na anafikiria kumpa talaka mkewe aende zake. Nikamwuliza; “ Katika ugomvi wenu mkeo anataka nini?”.


  “ E bwana , ni ujinga mtupu, hakuna cha maana anachoniambia!”


  Nami nikamwambia jamaa yangu aliyeniomba ushauri. Kuwa aje na mkewe kabla sijatoa ushauri wangu. Akafanya hivyo.

  Nikamwuliza mkewe; ” Katika ugomvi wenu mumeo anataka nini?”

  Naye, kama mumewe, akanijibu; ” Yaani shemeji, ni ujinga mtupu, mimi sioni cha maana anachoniambia!”

  Nikawaambia, katika U-wili wenu huo, tokeni kinadharia, kila mmoja wenu aende akakae kwenye kiti kitupu kilichokuwamo chumbani. Ni kiti cha kufikirika. Akae kitini pembeni kama mtu wa tatu akiwangaalia mke na mume wanaolumbana ambao ni nyinyi wawili.
  Hivyo, myakumbuke yale ambayo huwa mnabishana kila siku na kuwafanya msisikilizane nyumbani. Baada ya muda niwawauliza, ni kipi walichokiona.

  Wote wawili wakakiri, kuwa hawana kikubwa wanachogambania, isipokuwa, hakuna anayemsikiliza mwenzake. Hivyo basi, tatizo lao sio kuwa hawasikilizani nyumbani, bali, kila mmoja anajisikiliza mwenyewe.


  Wawili wale walikuwa wanashindwa kukutana katika hoja na kuelewana. Kila mmoja alijichimbia handakini, hakutaka kushindwa bali kushinda tu. Na malumbano mengine ya hoja si lazima mmoja ashindwe. Wote mnaweza kushinda au hata kukubali kushindwa.


  Mwanadamu ukikosa empathy kwa maana kujaribu kuingia kwenye nafsi ya mwenzako na kumwelewa, basi, utakosa pia sympathy- hali ya kumwelewa mwanadamu mwenzako na hata kumwonea huruma.


  Na moja ya mbinu za dola za dunia katika kukandamiza wenye kupinga watawala ni kumdhalilisha anayepinga. Usiku mmoja hivi majuzi nikiwa na watoto wangu, niliona aibu sana, na naamini sikuwa peke yangu, usiku ule tulionyeshwa kupitia runinga namna Dr Slaa, wa CHADEMA na mwenzake Tundu Lissu wakiteremshwa kwenye karandika la polisi.


  Haikuwa kitu kingine bali ni kitendo cha kudhalilisha. WaTanzania wengi, tusingependa, hata siku ile Chadema wakiingia madarakani, kuona wakiwadhalilisha viongozi wa CCM. Ni vema na busara kuwa na staha kwa viongozi wa kitaifa wa kisiasa. Kufanya hivyo ni kuwaheshimu pia wapiga kura. Kuheshimu wananchi.


  Hata Nyerere aliwahi kushtakiwa na wakoloni kwa kuandika makala ya uchochezi. Lakini, hakupata kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na mahakamani kwa namna ya kumdhalilisha. Hulka hii ya dola kudhalilisha wapinzani mara nyingi haitoi matokeo tarajiwa, bali kinyume chake. Kuwaongezea umaarufu wanaodhalilishwa na kuongezeka kwa chuki ya wananchi dhidi ya watawala hasa pale wengi wanapokuwa kati kati ya hali ngumu za maisha


  Na hili la CCM na Chadema kimsingi linahusu mgogoro wa kisiasa na hususan kuwania mamlaka ya kuongoza dola. Uchaguzi Mkuu uliopita umechagiza zaidi mgogoro huu.


  Siku zote, wanasiasa hawagombani bali hugombania maslahi ya kisiasa . Kugombana na kugombania maslahi ya kisiasa ni vitu viwili tofauti. Cha kujiuliza hapa; kinachogombaniwa ni maslahi ya nani? Je, ni nini athari ya kinachogombaniwa kwa jamii pana?


  Wanadamu siku zote tunaishi na migogoro, iwe majumbani na wapendwa wetu, iwe makazini, ndani ya vyama vya siasa, vilabu vya michezo na sehemu nyingine za jamii. Tukumbuke pia, kuna washika dau wa migogoro maana, kwao, kuendelea kuwapo kwa migogoro huwa kuna maslahi kwao.


  Siku zote, mgogoro unajenga hofu, lakini unavuta pia. Ni hulka ya mwanadamu kuogopa kuingia moja kwa moja katika mgogoro, lakini atapenda akae pembeni afuatilie mgogoro husika. Ndio, mgogoro huvuta. Kuna wanaofurahia kufuatilia habari za migogoro.
  Ndio maana mtu atakwenda kwenye meza ya magazeti na kuulizia gazeti au magazeti yaliyoandika habari za ’ Vita ya Chadema na CCM’. Atarudi nyumbani na kuburudika, kwa kusoma Chadema imewajibu nini CCM na kama Chadema imerusha ‘ kombora ’lingine kwa CCM. Kwa watu kama hawa, kwao ni burudani, hawafikiri sana juu ya madhara ya mgogoro husika kwa jamii ambayo nao ni sehemu yake.


  Katika dunia hii kuna nadharia ya mgogoro ‘Conflict theory’. Mgogoro una tabia zake ambazo mapema mno hujitokeza sambamba na mgogoro unapoibuka. Una pia hatua zake unazopitia .
  Mwanadamu unahitaji muda kuelewa chimbuko la mgogoro, kupima hoja za pande mbili, kisha kuchagua upande au kuitafuta busara ya kusuluhisha mgogoro husika. Na kwa walio ndani ya mgogoro wakati mwingine wanahitaji kutoka nje ya mgogoro na kujitazama wakati wakilumbana. Ndio mfano wa jamaa yangu wa hapo juu na mkewe.

  Kimsingi mgogoro ni mgongano kati ya watu wawili,vikundi, wanachama, makabila, vyama vya siasa au hata mataifa. Mgogoro ni dhana kongwe,imekuwapo tangu mwanzo wa mwanadamu. Neno mgogoro kwa Kiingereza linaitwa ‘Conflict’linatokana na neno la Kilatini ‘conflictus’.

  Mgogoro una sura nyingi, unaweza kuwa na sura ya kifamila au ya kijamii. Si kila mgogoro ni tatizo. Mgogoro waweza kuwa jambo la siha katika jamii. Huweza pia kutoa fursa ya kuwafahamu zaidi wahusika katika mgogoro.


  Ni jambo la hatari sana mgogoro wa watu wawili au kikundi kidogo cha watu unapochukua sura ya kijamii au kitaifa. Kunatakiwa haraka kuwapo na kitu kinachoitwa ‘ conflict management’. Ni namna ya kuuelekeza mgogoro mahali ambapo hautawagawa wanajamii na hata kufikia hatua ya kupandikiza chuki miongoni mwa wanajamii. Iwe ni chuki za kidini au kikabila. Kama mgogoro hauna maslahi mapana ya kijamii, basi, jamii ifahamishwe haraka hivyo, na wahusika katika mgogoro wafahamishwe pia.


  Miongoni mwa tabia za mgogoro ni kwa wahusika wa mgogoro kutafuta wadau ama washirika wa mgogoro ‘alliance’. Mwenye washirika wengi anajiona ana mtaji mkubwa katika mapambano ndani ya mgogoro huo. Kama mgogoro umebeba sura ya kijamii, basi, wahusika hutafuta kuungwa mkono na makundi mbali mbali ya wanajamii.


  Kwa hili la CCM na CHADEMA tufanye nini?
  Huu ni wakati wa kujikusanya kuizunguka bendera yetu ya taifa. Tuyatangulize maslahi ya nchi yetu. Twendeni tukazifanyie kazi busara za Askofu Laizer na Sheikh Darwesh. Na kwa waliyoyanena viongozi hawa wawili wa kidini, napendekeza Askofu Laizer na Sheikh Darwesh waandae kikao cha chai cha wao wawili na kuwakaribisha Makatibu Wakuu wa CCM na CHADEMA; Dr Slaa na mwenzake Wilson Mukama.

  Naamini, kikao cha chai na mazungumzo cha wanne hao chaweza kutoka na kauli nzito ya kutusaidia kutuongoza katika kuitafuta suluhu ya mgogoro wa CCM na Chadema. Hivyo basi, kuchangia juhudi za kurudisha utulivu Arusha na kwingineko.

  Maana, mgogoro wa CCM na Chadema bado uko katika hatua ambayo, kwa njia ya mazungumzo, tunaweza kuinusuru nchi yetu isiingie kwenye maangamizi. Kutoipeleka nchi yetu kwenye mgogoro kama ulivyokuwa wa CUF na CCM Zanzibar. Kuna waliopoteza maisha kule visiwani. Leo Maalim Seif na Dr Shein wanakunywa chai pamoja. Kule Zanzibar tulichelewa sana. Kwa yanayotokea huku bara hatuna sababu ya kuchelewa kuchukua hatua.

  Ni katika mazungumzo ya kindugu kati ya CCM na Chadema ndipo pale Chadema inaweza kuwasikiliza CCM na kuwaelewa CCM wanapoingiwa na hofu pale Chadema wanaposema kuwa nchi haitatawalika. Maana, katika uhalisia tulio nao sasa, nchi lazima itawalike, vinginevyo, hata wao Chadema, wakija kuingia madarakani hawataweza kuitawala.


  Ni katika mazungumzo ya kindugu kati ya CCM na Chadema ndipo pale CCM inaweza kuwasikiliza na kuwaelewa Chadema, kuwa kuna mambo ya msingi yanayopaswa yafanyiwe kazi na kuwa hata Chadema nao, kupitia kura za wananchi wanaweza kushika uongozi wa dola na CCM wakawa chama cha upinzani.


  Ni vema na ni busara yakajengwa mazingira ya kusamehe yaliyopita na kusameheana kama wanadamu. Tufanye hivyo ili kupisha njia ya kufungua ukurasa mpya kwa taifa letu. Hii ni Nchi Yetu. Tupingane kwa hoja. Hakuna mantiki ya kupigana na kujibu mapigo, maana, tutakuwa tukijipiga wenyewe kama taifa. Ona leo hali ya kukosekana kwa utulivu inavyoathiri kwa haraka uchumi wetu.


  Na Askofu Laizer na Sheikh Darwesh wamesema nini?


  Kwa nyakati tofauti, wamekaririwa na gazeti la Mwananchi Jumapili ya leo wakitamka haya;
  ” [FONT=&quot]Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Arusha, Abbas Ramadhani Mkindi ‘Darweshi,’ kwa pamoja waliwataka viongozi wa serikali na vyama vya siasa mkoani Arusha, kuacha ubabe, vitisho na kuhasimiana badala yake waonyeshe nia ya kweli kumaliza mgogoro huo.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]“Hali ni mbaya Arusha katika nyanja zote. Kisiasa kuna machafuko yanayotuathiri wote, waliomo na tusiokuwemo. Katika matatizo na machafuko haya, huwezi kunyooshea kidole mtu au chama chochote cha siasa, muhimu hivi sasa ni kufanyika majadiliano bila ubaguzi wala kudharauliana ili turejeshe amani mjini mwetu,” alishauri Askofu Laizer alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Askofu huyo, alisema Arusha inahitaji viongozi makini wanaozingatia utawala wa sheria, diplomasia na wenye staha katika kushughulikia changamoto zilizopo, kama mgawanyiko mkubwa wa kiitikadi ulioibuka kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kongozi huyo wa kidini mwenye ushawishi na msimamo usioyumba katika mambo yanayohusu jamii, alisema vitisho vya watawala na matumizi ya vyombo vya dola haviwezi kutatua tatizo la Arusha, bali vinaweza kupooza kwa muda na baadaye mambo hayo yataibuka kwa nguvu na mbinu mpya na kusababisha vurugu zaidi.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Alionya kuwa si busara kupuuza madai ya Chadema na kuwashauri viongozi wa Serikali kuacha kutumia nguvu yadola kutunishiana misuli na chama hicho kwani Arusha inaelekea pabaya na likitokea la kutokea, wote watangamia. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]''Lazima busara itumike kwa kusikiliza hoja za pande zote husika bila kubezana.'' Alishauri.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Bila kutaja jina, Askofu Laizer alisema kauli za vitisho zinazotolewa na viongozi wa serikali Arusha, zitachochea harakati za wanaodhani wanaonewa, kutafuta haki na pengine kutumia njia za machafuko zaidi na kuchafua hali ya hewa kuliko livyo sasa.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Askofu Lazier alivishauri vyama vya upinzani kuepusha shari kwa kudai haki zao kwa njia ya amani hata kama wanahisi kuonewa, kama ilivyo kwa Arusha ambapo vijana wa CCM (UVCCM), waliandamana na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali cha polisi, lakini Chadema walipojaribu kufanya hivyo, walikamatwa na kushtakiwa[/FONT]
  [FONT=&quot]kwa kusanyiko lisilo halali.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]“Vyama vya upinzani vikwepe pale sunami au upepo mkali unapovuma dhidi yao, wainame kidogo kimbunga kipite halafu waendelee mbele. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]"Vitumie wataalamu na wasomi waliojaa ndani ya vyama hivyo kutatua matatizo na migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani na utulivu,” aliasa Askofu Laizer.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema tatizo linalojitokeza nchini hivi sasa ni vyama vya upinzani kutopewa fursa ya kutekeleza na kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa uhuru kama ilivyo kwa CCM. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, alivashauri vyama hivyo kufuata sheria na kanuni katika kudai na kutafuta haki yao .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa upande wake, Mkindi alisema viongozi serikalini wasijidanganye kuwa wanaweza kulinda amani kwa mtutu wa bunduki na kushauri vyama vinavyohasimiana vya CCM na Chadema kukutanishwa ili vijadili na kuondoa tofauti zao ili kurejesha amani na usalama Arusha.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]“Arusha imechafuka, hakuna amani. Biashara imekufa, hata mikutano ya kitaifa na kimataifa haifanyiki hapa tena kwa wingi kama ilivyozoeleka. Ufumbuzi ni watu kukaa mezani wazungumze, waadiliane na kutatua tofauti zao.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]''Chadema wasidharauliwe hata kidogo kwa sababu wana watu wengi wanaowaunga mkono ambao wako tayari kusikiliza na kutekeleza lolote wanaloambiwa,” alisema Mkindi. ( Mwananchi Jumapili, Novemba 13, 2011.)[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Naam, It always seems impossible until it is done![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Nahitimisha.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Maggid Mjengwa[/FONT]
  [FONT=&quot]Iringa[/FONT]
  [FONT=&quot]Jumapili, Novemba 13, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
  [/FONT]
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  Huenda ikawa wana masikio ya kusikia japo sidhani kama CCM watajishusha! Ni waongo na wababe ila wanazidi kubaki peke yao na wananchi walio wengi wanazidi kuuona ukweli
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti;

  Umejitahidi sana kuonesha busara iliyotukuka kwenye conflict management. Tatizo si ugomvi na kudhalilishana tatizo kuu hapa ni kulinda masilahi binafsi hivyo hata siku moja usitarajie CCM itakuwa na busara ya kuweka mbele masilahi ya Taifa wakati kwenye vikao vyao wanaambiana masilahi ya chama kwanza.

  Kwa wengi ndani ya CCM uongozi na kushika madaraka ni kibarua kinachowaweka mjini na si kutumikia Taifa. Ingekuwa ni kutumikia Tifa mgogoro wa Arusha usingetokea, wizi wa kura kwenye chaguzi usingetokea ila kwa kuwa kwao wao CCM hii ni career ya kujitajirisha harakaharaka hawatakusikia ila kama masilahi yao ya nchi ni kwa wao kuwa victors.

  Nirudi kwa CDM nao, Kama chama cha siasa chenye malengo ya kushika uongozi wa nchi haiingii akilini kuona wanakubali kupindishwa kwa taratibu eti kwa sababu kupinga si masilahi ya Taifa. Kama tumejiwekea taratibu zetu wenyewe tuwe tayari kuzisimamia hata kama zinatukata mikono, Hebu angalia jinsi ambavyo CCM inajitwalia madaraka ya mchakato wa katiba bila kushirikisha wadau wote unatarajia kwenye mambo kama haya wapinzani wakubali tu kwa sababu kupinga si masilahi ya Taifa?.

  Pale CCM na waliomo humo watakapoona kuwa CCM ni chama tu ila sisi wote ni watanzania na malengo yetu yawe kuiendeleza nchi. Na wao pia wanaweza kupata uongozi wa nchi kupitia chama chochote mbali ya CCM. Wakijua kuwa 'Brand CCM' is now obsolete na kuwa watanzania wanataka mabadiliko basi hakuna haja ya kuwawekea usiku. Wakubali kuwa uongozi ni dhamana na siku wenyewe wakisema basi huna budi kukubaliana nao. Tatizo la CCM wanajipa ownership of Tanzania hapo ndipo kuna mgogoro, yaani chama chochote kile kinachoonekana kuwazidi wanakiona kama adui anayetaka kuwanyang'anya halali yao. Kulikuwa hakuna haja hata kidogo kupindisha sheria za uchaguzi wa umeya Arusha. Who is Mayor? while you are occupying the state house?. Hapo ndipo CCM inapokosea na as long as this fracas continues the winner is CDM regardless what they do to Dr Slaa et al.
   
 4. m

  maggid Verified User

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hofstede,

  Asante sana. Nami nakushukuru kwa mchango wako.

  Maggid,
  Iringa.
   
Loading...