naoma wajipange vizuri tu kuweza kufika hasa kule matawini/vijijini, ile style yetu ya HELIKOPTER iendelee kwani itakuwa rahisi kufikia maeneo mengi kwa muda mfupi........sisi wa mitandaoni tupo pamoja nao na sisi wengine tupo kuwasaidia kukampeni na kuhamasisha ikiwa wakiamua kutuita....
Nchi inachukulika kirahisi tu kama uteuzi wenyewe ndio huu wa DR.SLAA...sioni kama kutakuwa na shida kiasi hicho nasisi wengine tumejipanga vilivyo kuhakikisha hakuina'' UCHAKACHUAJI WA KURA''
PAMOJA DAIMA KAMA VODACOM VILE....
Asante sana Hekima Ufunuo nashukuru tena kwa kunielewa kuhusu Kanda za uchaguzi. Kuhusu madaraka ya Meneja wa kanda nilikuwa na maana ya yeye atakuwa amepewa limits na kitengo kikuu wewe umekiita Kamati kuu ya uchaguzi, limits ambazo ni za uwanja wake wa kijidai, akitaka kuvuka pale lazima apate ridhaa kutoka kwa kampeni meneja mkuu au kamati kuu ya uchaguzi. Kufanya hivi kutamfanya ajiamini na kuifurahia kazi yake ambayo mara nyingi huwa ni za kujitolea zaidi.Kwanza nakupongeza kwa ushauri mzuri ambao naamini unahitaji kufanyiwa kazi zaidi ili kurefine hii idea ya kanda. Lakini kwa ujumla wake ni jambo jema.
Kitu kimoja ambacho mimi naona kina shida ni kanda kuwa na mamlaka ya makubwa kabisa ya kutokuingiliwa kwa meneja wake. Hapa nashauri kiongozi anayeongoza kanda awajibike kwa kamati kuu ya kampeni ambayo ndiyo itakuwa inaunganisha na kusimamia kampeni kwa nchi nzima.
Najua kutakuwa na maswali magumu kama ya kugawanya resources zilizopatikana, hii kamati kuu ya kampeni, kutokana na taarifa zinazopatikana kutoka kwenye kanda ndiyo itakayoratibu maswala yote ya mahitaji muhimu kwa kanda. mfano, Wakati kanda inayohusisha Shinyanga na Mwanza inahitaji usafiri wa aina fulani kufika eneo fulani, kanda inayohusisha Arusha na Moshi usafiri wa aina hiyo hauhitajiki. Sasa hapo ndipo kamati kuu inapochambua na kuamua.
Respect wakuu.
SikongeMie napendekeza kitu kimoja kuwa:
Hadi leo, CHADEMA na Dr. Slaa mwenyewe watakuwa wameshasoma au kufanya ka uchunguzi ka haraka haraka ka watu gani hapa JF wamekuwa wakimtaka Slaa kuwa mgomea kwa siku nyingi. Sidhani kama hawa watu walifanya kwa kutania.
Itakuwa vema watengeneza Mtandao au Chumba maalumu cha kuwaunganisha Watanzania hao wote. Wakifika huko sasa ndiyo haya mawazo yaanze kutolewa. Au watengeneza EMAIL maalumu ambayo watu wataandika na hata namba ya simu ambayo itarekodi mazungumzo yote. Mawazo yao kwa kipindi kama wikimbili yakusanywe na timu iliyochaguliwa ikae na kuyajadili. Kwa CCM wanavyopenda kuiga, sintashangaa wakiiga. Hapa sasa itabidi kucheza chenga za mwili, kufeki na kuweka PLAN A, B, C na D ikibidi.
Vinginenevyo, nakubaliana sana na wewe Luteni na pia member aliyeandika kuwa TUSIMWAGE MTAMA kwenye kuku wengi.
Sikonge said:
Kwa wale wanaodhani CCM haiwezi kushindwa, tuwaambie mbona KANU na UNIP ziliweza kushindwa? Watanzania sio mambumbumbu. Wanajua fika kwamba hali ngumu ya maisha waliyo nayo haitabadilika kama wataendelea kuwachagua watu wale wale. Kama alivyosema Baraka Obama: "You can't do the same thing over and over and expect a different result".
Kwa sasa, nyongeza yangu kwenye mchakato ni hii:
(1) Lazima kuwe na uwezo wa kuwafikia watu wengi kwa haraka. Chadema iwe na undugu na radio station kadhaa. Itabidi hotuba za Dr. Slaa zisikike redioni kila siku.
(2) Simu za mikononi zitumike kwenye kampeni. Kuwe na uwezekano wa kutuma matangazo na ujumbe toka CHADEMA kwenye list kubwa kabisa ya simu za mkononi. Ushirikiano na kampuni za simu za mikononi ujengwe.
(3) TV advertisements hazitawafikia wengi sana, lakini zina uzito mkubwa. Itabidi kutafuta wataalamu watengeneza commercials chache zitakazoonyesha uozo wa CCM, na kuzirusha wakati muafaka. This will cost money, but it will be money well spent.
(4) Kuwe na umoja wa waliochoka na ukiritimba wa CCM. TANU na mwanaye CCM wamehodhi madaraka kwa miaka 50 bila kuweza kuleta ahueni kwa Watanzania, na bado wanang'ang'ania. CUF ialikwe kushirikiana na Chadema.