CHADEMA bila UKAWA kuelekea 2020 mmelifikiria hili??

Pamputi

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
982
724
Kwa namna yoyote ile vyama vikubwa vya siasa nchini yaani CCM,Chadema n.k vina malengo makubwa sana ya kuwa na ushindi mkubwa sana katika uchaguzi mkuu ujao 2020 japo kwa sasa tunaeza kusema bado ni mbali sana, lakini nimeona pia si vema hawa watani CHADEMA wakiweza kulitathmini hili la uwezo wao halisi wakisimama wao kama wao dhidi ya Magufuli 2020 kama itakua hivyo.

Ni wazi kabisa kwamba ule upepo, kimbunga na mafuriko ya ukawa havitakuepo tena kuelekea 2020 kwa kuzingatia uhalisia wa hali ya vyama ambavyo viliunda umoja ule kwa sasa, CUF inachechmea, NCCR imekufa kbs limebaki jina tupu,NLD sio lolote sio chohote na hivyo kubakiwa na ukweli wa wazi kabsa kwamba UKAWA haipo tena hata sasa kabla hata ya hiyo 2020, na ni hapa ndipo napata swali kwamba JE CHADEMA BILA UKAWA 2020 MMELIFIKIRIA HILI??

2015 Chadema kwa mgongo wa ukawa yaan vyama vinne waliweza kupata kura milioni 6 sambamba na majimbo kadhaa ya uchaguz ambayo mengi walishinda kwa kutumia upepo na nguvu ya vyama hivi na ushawishi binafsi wa watu kadhaa, kwa mfano chama kama CUF ambacho ni chama chenye kuaminika sana kwa upande wa pwani na visiwani kwa nafasi na utashi wake naeza amini kwamba kilichangia sana katika upatiknaji wa kura million sita za urais ambapo naamini kwa uwezo wake wa kuaminika kwa upande wa pwani na maeneo mengne basi huenda CUF pekee ikawa ilichangia kura si chini ya milioni 2 katika zile 6 sasa kuelekea 2020 hakuna CUF ndan ya UKAWA je Chadema mmeliona hili??

Lowassa na kundi lake na ushawishi wake kwa 2015 huenda alichangia kupatikana kwa kura million 2 zingne na majimbo kadhaa , lakini mvuto na ushawishi wake kufikia 2020 hauwezi kuwa the same, JE chadema mnaliona hili??, Kwa hyo ukirudi katika common sense uwezo wa chadema pasi na ukawa na utashi wa watu binafsi unaona kwa wazi kabisa uwezo wao kushinda au kuongeza asilimia ya ushindi 2020 dhidi ya ule wa 2015 ni finyu mno.

ukijaribu kujiuliza maswali kadhaa mpaka sasa kwamba ni nani kutoka chadema ambae kwa hakika anaeza iteteresha ngome ya CCM mpaka sasa hamna, ukujiaribu kuwaza uwezo na nguvu ya chadema wao kama wao kufikia 2020 unaona pia ni mdogo sana, uwezo wa kuibua mijadala yenye sense ya kitaifa hakuna, hata uwezo wa chadema kumobilize watu kwa sasa ni mdogo sana, uwezo wao kifedha dhidi ya chama tawala ni mdogo, uwezo wa kuwa na matamko yenye kutekelezeka ni empty pia, uwezo wao kwenye propaganda ni chenga pia, umimi na umwinyi na kuishi kwa matukio ya kudandia ndio chadema tuliyobakiwa nayo, Sasa Je kueleka 2020 huku ukiwa na uhakika 100% ya kusimama pasi na mbeleko ya UKAWA chadema mmejipangaje?
 
UKAWA yanini? Wakati imejaa akina Lipumba,chadema waende alone.
 
,,sana watakuambia tundu lisu anafaa kuwa rais mtu wa majigambo na misifa na umimi, ngoja waje wenyew wakujibu
 
Subiri povu lao hapo na uvumilie matus yao maana ukwel huwa unaumiza
 
Kila siku hamkai huko kwenu mnawaza chadema. Inawahusu nini, tangu lini mkaiombea kheri chadema. Ikifa si ndiyo furaha yenu??
 
UKAWA YETU NI CCM YA JK NA WENZAKO ALAFU TUTAWANYOONSHA NA MFANYE KM MLIVOFANYA ZNZ MTAONA MBAVUUU
 
Back
Top Bottom