Great Thinkers, niseme yanayonikera nchi hii. mimi naangalia matatizo ya nchi hii na jinsi nchi inavyokwenda naona hatuna dira wala mwelekeo uanaoeleweka. Kinachosikitisha ni kwamba vyama vya siasa havina mwelekeo wala mwonekano unaotakiwa kuwapambanua viongozi wake moja kwa moja mbele ya jamii yetu. Jina kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo au CCM, halitoshi kukielezea chama, je hawa ni wajamaa au mabepari? wanafuata siasa zipi? Hii itasaidia kujua watatekeleza vipi sera zao, kijamaa au kibepari? Tutaendelea kuwa watumwa wa IMF na WB? Kiitikadi hasa wanafuata siasa za mrengo upi? kwangu hili ni muhimu na silioni.
Jingine ni kutenganisha chama na serikali, hili ni balaa lingine. Tutajaongozwa na wahuni hapa tusipoangalia. Uwepo mfumo unaotenganisha vitu hivi viwili. haiwezekani rais aogope kufanya mambo ya kitaifa kisa wanachama,eti nitawaudhi wanachama. upuuzi huu.