CHADEMA Asilia v/s CHADEMA Pesa

CHADEMA Asilia v/s CHADEMA Pesa

View attachment 299401

Huyu Daktari historia baadaye itamtambua kama taa ndani ya giza nene lililoingia kwenye Chadema.

ALIKATAA kabisa KUKAA NA MWIZI. Maisha mema na marefu unaporudi nchini Marekani kuendelea na maisha.
 
Mtaimba mipasho ya kila rangi mwaka huu. MABADILIKO KWANZA hizo ngonjera nyingine mkawaimbie Lumumba maana wao na wasanii kama nyie huwa ni damdam.
 
Lowasa atakuwa namba mbili kama alama ya chama chake
 
baada ya kufungua mlango na kuwaleta walewa pesa waje na kufanya watakavyo kwenye chama, ni muda madhubuti wa kukaa chini na kutathmini ni uharibifu na hasara kiasi gani wamesababisha.
 
Ni kweli na dhahiri kwamba ujio wa Lowassa umeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama cha mabadiliko. Chama kimebadilika kweli kweli..

Inasikitisha kuona chama kilichofanya kampeni ndefu zaidi ya vyama vyote, yaani miaka 7 na miezi minne leo hii kimegeuka kuwa kituko..

Leo tuangalie tabia za wanachadema ASILIA (watoto wa Mungu) na Chadema PESA (Mkapa aliwaita malofa), chini ni listi ya tabia zinazoashiria makundi haya:-

CHADEMA ASILIA:
* Hawa ni WAZALENDO na hawanunuliki hata kwa milioni 300
* Hawa ni wasomi na watu makini sana na huwezi kuwaona kwenye mikutano ya Lowassa
* Hawa wanajua CCM sio tatizo bali tatizo ni kiongozi, wakati wa Nyerere na Mwinyi hakukuwa na udokozi wa hali hii
* Hawa wanajua HAWAWEZI KUMCHAGUA MTU aliyekuwa kwenye LISTI OF SHEM.
* Hawa wanajua ndani ya CCM, Warioba, Msuya, Mwandosya, na wengine wengi sana sio mafisadi bali ni watu wachache wasiozidi kumi
* Hawa HAWAJAPOTEZA kumbukumbu, wanajua MWIZI NI MWIZI TU na hawababaishwi na MACHOZI ya MAMBA.
* Hawa wanajua maendeleo hayaletwi leo wala kesho na kwao cha muhimu ni Maendeleo bora na sio bora maendeleo
* Hawa watazienzi harakati za Zitto na Dr Slaa na kamwe hawatateteleka
* Hawa wanajua umaskini anaochukia Lowassa ni umaskini wake mwenyewe

CHADEMA PESA:
* Hawa kwa kiasi kidogo cha shilingi 1,000 mpaka 2,000 wako tayari kuvaa shati na kofia ya CCM na kushangilia sana!
* Hawa huwa hawataki kuongelea sera maana hazipandi
* wengi wao huwa wanaonekana wajanja mpaka pale wanaposema serikali imeuza twiga wote!
* Wanamchukia sana Dr Slaa na kila anachosimamia kwa sasa
* Hawa wengi HAWANA KUMBUKUMBU ya kampeni ya kuuwa ufisadi nchini au wamejitoa akili hivi majuzi
* Hawa wanamwita Lowassa MPAKWA MAFUTA!
* Hawa wanadhani CCM ni pepo badala ya chama
* Hawa wanadhani CCM ni mkapa, ridhiwani, Raisi kikwete, tibaijuka na chenge
* Hawa wanadhani watumishi wote serikalini wanatibiwa India.
* Hawa NI WATU WA MATUSI TU, hawawezi kuandika bila kuteleza na tusi

SWALI:
JE WEWE NI CHADEMA GANI??? (Kura yako ni Siri yako)


Mkuu Umenena,

Ila kwenye CHADEMA Pesa Umewasahau Walio-nacho, i.e. Akina Mengi, Mbowe, Ndesamburo, Rostam n.k. ambao kwao CHADEMA ni kitega uchumi.
 
CHADEMA hatuna mpasuko wala mgawanyiko kama ilivyo CCM maana CCM ndio imegaqanyika na hata Rais Mstaaf JK juzi kati alishasema CCM inawenyewe WENYE CCM vs WAPENDA CCM
 
Asilia tumetembeza viboko vya kutosha kwenye sanduku la kura kukiadhibu chama chetu na kwa sasa hatuko mitaani kushangilia ushindi wa CCM ila tunawaangalia CCM wanavyosheherekea ushindi tuliyo wasaidia kuupata na tunampongeza sana Dr.Magufuli kuwa rais wa5 wa jamuhuri ya Muungano. SALAM ZIMFIKIE DR.SLAA POPOTE ALIPO. TUMEMALIZA KAZI.
 
Historia inaonyesha chama kikienda kinyume na "principle zake" huwa wananchi wanakiadhibu kisawa sawa. Tuangalie miaka inayokuja sijui itakuwaje, naona kama ACT ndio watakao ibuka kuwa alternative, chama cha option.
 
nendeni act kwa nini mnaing'ang'ania chadema?. hamieni act mkaendeleze koko nyie.
 
Unaonekana kuumia sana na hicho chama chenu kwaani si uondoke uende hata act au ccm kuliko kuumia roho kwaani CDM ndy imekuzaa
 
Waliojiita chadema asili walikuwa wanatumiwa na Masaburi kuandamana mkaishia viboko na kumtaja aliyewatuma.
 
CDM imekuwa makapi, na wabunge wao wakisema ufisadi na rushwa tutacheka sana.
 
Muda wa Dr.Slaa kukumbukwa ni sasa.
naona wenye akili wameanza kukaa chini na kufikiria hili, ila kusema ukweli na nadhani wengine wamelisema, Dr. Slaa labda alikuwa sawa au hakuwa sawa kuondoka.

Waliojiita chadema asili walikuwa wanatumiwa na Masaburi kuandamana mkaishia viboko na kumtaja aliyewatuma.
walijiita, hawakuwa asilia kweli, wale asilia kweli walikuwa wamekaa nyumbani wanasubiri tarehe 25 Oct wafanye kweli
 
Habari ndio hiyo sasa. Tunarudia kutoa tangazo kwa niaba ya chadema asilia, tunajua Mbowe unalijua hili. Tunakutaka ujipime mwenyewe na ujiuzuru haraka iwezekanavyo wewe pamoja na group lako ambao mliwapokea mafisadi ukawa kwa tamaa zenu tu. Wapo wengi wanamudu nafasi zetu kwa hiyo msidhani nyinyi ni miungu watu, wengine hawatazimudu kuzisimamia
 
Back
Top Bottom